Hichi ndicho alichokiandika Yule Mwanume alifanya Mauaji Ilala ndani ya Facebook
Anaitwa Gabriel Munissi mkazi wa Mwanza ambae Polisi Ilala Dar es salaam ilithibitisha kwamba ndio amehusika kufanya mauaji ya watu wengine wawili kabla ya yeye kujiua huku ikiaminika ni kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kama hukuipata hii taarifa ni kwamba Gabriel alikwenda Ilala na kusimama nje ya nyumba moja iliyokua na fensi na geiti jeusi kusubiria atoke Mwanamke anaetajwa kuwahi kuwa mpenzi wake na kisha baada ya Mwanamke huyo kutoka huku akiendeshwa na mwanaume mmoja kwenye Toyota Surf na kukiwa na abiria wengine wawili kwenye gari, Gabriel ndio alianza kufyetua risasi ovyo.
Shahidi alieshuhudia hili tukio mwanzo mwisho anasema waliamini kabisa kwamba Gabriel hakuwa jambazi kwa jinsi alivyoshambulia na kuendelea kubaki eneo la tukio bila kuwadhuru watu wengine waliokuwemo karibu, vilevile kama angekua jambazi isingekua rahisi kwa yeye kujiua.
Shuhuda anasema Gabriel alipiga risasi mpaka zilizokuwa ndani zikaisha ikabidi aongeze nyingine na kuendelea kushambulia huku akiwa hana nia ya kuwaua wale abiria wengine kwenye gari baada ya kuwajeruhi isipokua Mwanaume aliekua anaendesha pamoja na Mwanamke anaetajwa kuwa mpenzi wake ambae alikua amekaa pembeni ya dereva.
Hiki hapa chini ndio kitu cha mwisho alichokiandika Gabriel kwenye ukurasa wake wa facebook.
Gabriel Munissi