Mwanaume Mchawi mwenye "MATITI" Aanguka Mchana Kweupe.
Mwanaume anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 ambaye anasadikiwa kuwa ni mchawi, juzi Jumatano alikutwa pembeni ya Mto Okrudu eneo la Kaimebre, sehemu ambayo ni karibu na soko jipya la Kasoa kwenye jiji hilo lililopo katikati mwa nchi ya Ghana.
Jamaa huyo, ambaye alisema kuwa anaitwa Charles Atta, alionekana akiwa hoi huku matiti yakionekana kama ya msichana mdogo.
Mwili wake ulikuwa umetapaka michanga na matope kutoka kwenye mto huo pembeni na alipokutwa, inaaminika jamaa huyo alianguka toka kwenye ungo akiwa kwenye safari zake.
Ndugu wawili ambao ni mtu na kaka yake Liberty Obeng na Innocent Obeng, walisema kuwa walisikia sauti ya ya mtu wasiyemfhamu akilia kutaka msaada.
Kwa mujibu wake, anasema yeye na wenzake walikuwa wanapaa kwenye usawa wa Kanisa ambao unalindwa na Malaika usiku kucha na ndipo alipojikuta ameanguka kwenye eneo hilo la Shule ya Kimataifa ya Watumishi wa Wafalme.
Dc.