TOVUTI KUU NA MPYA YA SERIKALI KUZINDULIWA LEO


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kesho tarehe 29, Novemba 2013 anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Uzinduzi wa Tovuti Kuu hiyo inayopatikana kwa anuani ya www.tanzania.go.tzutahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,  Wananchi, Wafanyabiashara, Washirika wa Maendeleo, Taasisi zisizo za Serikali na Wawakilishi kutoka vyuo Vikuu. 

Tovuti Kuu hiyo ni mojawapo  ya juhudi za Serikali  katika kuhakikisha kuwa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa urahisi,  wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya nchi. Tovuti Kuu hiyo pia  ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma zinazotolewa na Taasisi  za Serikali kwa urahisi.

Taarifa na huduma katika Tovuti Kuu hiyozimegawanywa katika maeneo makuu sita ya ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya Nje inalenga kutoa huduma mbalimbali kama upatikanaji wa nyaraka zote za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.

Huduma nyingine katika Tovuti Kuu hiyo imetengwa katika ukarasa wa Nifanyeje? ambao  unamjengea uwezo mwananchi wa kufahamu taratibu za upatikanaji wa huduma zinazotolewa na taasisi mbali mbali za Serikali kama nifanyeje kupata pasipoti, kibali cha kazi, TIN, Cheti cha kuzaliwa na mikopo ya chuo.

Aidha tovuti hiyo pia inalenga kuziunganisha Tovuti na mifumo ya Taasisi mbali mbali inayotoa taarifa na huduma kwa wananchi na wafanyabiashara katika dirisha moja.

Tovuti Kuu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na kupatikana kwa anuani ya www.egov.go.tz chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Tovuti hiyo iliboreshwa na kuunganishwa na iliyokuwa Tovuti ya Taifa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz mwaka 2012 chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger