Park, Mwanamke Mwenye Muonekano wa Kiume, awatesa wachezaji wenzake.



Huyo ni Mshambuliaji kutoka nchini Korea ya Kusini, Park Eun-Seon ambaye kwa muonekano wa nje utaamini ni mwanaume bila shaka. Mwanadada huyo ambaye amekuwa akiwakosesha Raha wachezaji wengine kiasi cha kutakiwa kufanyiwa kipimo maalumu cha kuangalia Jinsia yake ya halali ni ipi hasa baada ya kufunga magoli 19 katika mechi 22 katika ligi ya wanawake ya kitaifa msimu huu.


Akioneshwa Kusikitishwa na Hali ambayo watu wanamuonesha, Park aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba " Wapo watu wamekusudia kumuona akianguka na kupoteza mafanikio yake, hii si mara ya kwanza kuambiwa akafanye vipimo vya kuhakiki jinsia yake, walimfata kipindi cha Olympics, Kombe la Dunia na Mashindano mengine kadhaa"

Wafuasi wa Park wamekitafsiri kitendo hicho kama ni unyanyasaji wa haki za kibinadamu.


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger