SAMSUNG yawalipa APPLE $ Bilioni 1 kwa kupeleka Malori 30 yaliyojaa Senti 50


Baada ya Mvutano wa zaidi ya Mwaka, Mahakama iliamua kampuni ya SAMSUNG kutoka Korea ya kusini kuwalipa APPLE zaidi ya Trilioni 1.6 za Kitanzania kama faini inayotokana na Kokopi kwa Teknolojia bila kibali husika.

Cha kufurahisha ni kwamba Mahakama haikulazimisha malipo hayo yafanyike kwa mkupuo au kwa awamu ili mradi hela hizo zitimie. Kutokana na hayo SAMSUNG waliamua kuwachezea rafu ya aina yake APPLE kwa kupeleka Malori 30 ambayo ndani yake yalikuwa yamejaa Coins za senti 50 ili kulipa Faini hiyo.

Walipofika Mlangoni walizuiliwa na walinzi wa hapo lakini baadae kidogo CEO wa APPLE, Tim Cook alipigiwa simu na CEO wa SAMSUNG kumwambia kuwa huo ndio mzigo wao na deni litalipwa kwa namna hiyo.

Mchezo huo Mchafu na wa akili utawapa Gharama kampuni ya APPLE kwani watapoteza muda kuhesabu na kuhakikisha ukamilifu aw Kiasi hicho cha fedha na kujipanga kuzipeleka Bank.

Katika maelezo yake Mwenyekiti  wa SAMSUNG, Lee Kun-hee amesema kwamba kampuni yake haiwezi ikatetereshwa na na "Wajanja wenye Mbinu" ikiwa wanapenda michezo michafu, hata wao wanaiweza.

Ikiwa watataka kuziyeyusha Coin hizo na kutengenezea Computer basi ni juu yao hainihusu, nimeshatekeleza amri na kuwalipa Coins Bilioni 20 zenye thamani ya $ Bilioni Moja.


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger