KIKWETE ASHAURIWA KUFUKUZA KAZI PINDA

Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Khangi Lugola, akichangia mjadala wa Kamati za tatu za Bunge  zinazohusu fedha, bungeni Dodoma j

Rais Jakaya Kikwete, ameshauriwa kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikielezwa sababu kuwa ndiye kikwazo katika utendaji wa Serikali na kwamba akiachwa ataipeleka pabaya Serikali na CCM.
Kikwete pia ameshauriwa kumfukuza kazi Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, kwa kushindwa kukabiliana na matatizo ya ubadhirifu katika halmashauri nchini.
“Kama (Rais) unaitakia mema nchi na CCM kuchukua hatua za kuwafukuza kazi Pinda na Waziri Ghasia,” alisema Mbunge wa Mwibara, Khangi Lugola (CCM), juzi alipochangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka jana.
“Kwa nini Watanzania wafe kwa kunyimwa misaada na wafadhili kwa sababu ya mtu mmoja tu Pinda, kwa ajili ya Ghasia ameiendesha Tamisemi kama Saccos ama Vikoba?” alihoji.
 “Mchawi wetu ... ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekuwa mpole mno hawajibiki,” alisema Mh. Lugola na kuongeza, “Kuanzia jana (juzi) Waziri Mkuu anahudhuria mahafali.”
Wakati Lugola akizungumza mawaziri waliokuwepo bungeni ni wanne, manaibu mawaziri wawiliwawili, wakati  mawaziri wote 53.
Mwananchi

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger