Bangi, Pombe na Utovu wa Nidhamu vyamponza Dogo Janja


Dogo Janja atimuliwa Mtanashati Entertainment.....Makosa yake ni kuvuta bangi na kutoenda shule

Akizungumza na Mtandao huu, kiongozi wa Mtanashati Entertainment Ustaadh Juma Namusoma alisema kuwa sababu za kumtimua Dogo Janja ni utovu wa nidhamu, unywaji pombe, kutokwenda shule pamoja na uvutaji bangi.
 
 Aliongeza kuwa tayari amempatia nauli ya shilingi 90,000/=  kurudi nyumbani kwao jijini Arusha alipotokea. Dogo Janja alitua kwa mbwembwe jijini Dar es Salaam kwa ndege Juni 22 mwaka jana akitokea Arusha na kujiunga na kundi hilo.
 
 Awali alikuwa katika kundi la Tip Top Connection linaloongozwa na Madee lakini ilitokea kutoelewana kati yao na kurudishwa kwao Arusha.

 Alipopigiwa simu , Dongo Janja alidai kuwa bado ni memba hai wa Mtanashati Entertainment.

Read More »

Mbunge wa CCM (60) ndani ya kashfa ya kimapenzi na Mvulana wa Miaka 26


MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60), amejikuta kwenye kashfa nzito ya kufunga ndoa na kijana, kinda wa miaka 26, Michael Christian.

Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG), linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge wanaoifahamu pamoja na majirani wanaoishi na mbunge huyo.
 
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya wanandoa hao na majirani wanaowazunguka, vililiambia gazeti hili kuwa ndoa hiyo ilifungwa Septemba Mosi mwaka 2011, na imebaki kuwa siri kabla ya wawili hao kukorogana.
 
Kabla ya wawili hao kuamua kufunga ndoa, mbunge huyo kutoka mkoani Rukwa, mwenye makazi yake Bagamoyo mkoani Pwani, alikuwa akimtumia Michael kwenye shughuli mbalimbali na muda wote alikuwa akiishi nyumbani kwa mbunge huyo.
 
Inaelezwa kuwa mbunge huyo ambaye ana familia ya watoto wawili ambao kiumri wanalingana na Michael, alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo kwa siri kubwa na baadaye alifanikiwa kumshawishi wafunge ndoa huku akimuahidi kumpa huduma mbalimbali anazotaka.
 
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao waliamua kufunga ndoa katika Kanisa la TAG baada ya mbunge huyo kufanikiwa kumshawishi Mchungaji Rwakatare kwamba ndoa hiyo itakuwa siri, hasa kutokana na tofauti ya kiumri kati yao.
 
Hata hivyo ndoa hiyo kwa sasa imekumbwa na mgogoro mkubwa, huku mbunge huyo akidaiwa kuzuia kila kitu cha mumewe huyo, hasa vyeti vyake vya shule kama njia ya kumbana warudiane.
 
Siku ya harusi
Kwa mujibu wa mashuhuda wa harusi hiyo ya aina yake, mbunge na kijana huyo walikwenda kanisani wakiwa wawili bila mashahidi kama ilivyo kawaida, na ndoa hiyo ilifungwa katika ofisi ya kanisa na sio ndani ya kanisa.
 
Mashahidi wa ndoa hiyo waliitwa hapo hapo kanisani na walisimamia na kushuhudia utiaji saini wa cheti cha ndoa na kisha wanandoa hao kutawanyika kwenda kwenye fungate (Honey Moon). Hakukuwa na sherehe baada ya kufungwa ndoa.
 
Inadaiwa kuwa hakukuwa na ndugu yeyote wa maharusi hao aliyeshuhudia tukio hilo la kihistoria la wawili hao kuunganishwa na kuwa mwili mmoja.

Kauli ya Bwana harusi
Tanzania Daima Jumatano, lilifanikiwa kumpata Michael, ambaye katika mazungumzo yake alikiri kufunga ndoa na mbunge huyo Septemba Mosi mwaka 2011, lakini kwa sasa wametengana kutokana na sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.
 
“Mimi nadhani hili ni jambo binafsi, sio vizuri kulizungumza hadharani ila kweli nilifunga naye ndoa maana inaonekana mnajua mambo mengi kunihusu, na ni kweli kwa sasa tumeachana,” alisema kwa kifupi.
 
Alisema walikutana na mbunge huyo Bagamoyo wakati alipokuwa akifanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali ya wilaya hiyo kama muuguzi mkunga wakati mbunge huyo akiwa muuguzi mkuu wa wilaya katika hospitali hiyo.
 
Alipoulizwa sababu za kukubali kufunga ndoa na mama wa umri wa miaka 60 wakati ana miaka 26 na sababu za ndoa hiyo kuvunjika, Michael alisema ana historia ndefu katika maisha yake kwani alizaliwa yatima na amekua na kulelewa kwa ufadhili wa kituo  cha Safina Street Network.
 
“Katika mazingira niliyokulia, unaweza kujua kwanini nilikubali kuingia kwenye ndoa hiyo. Sina ndugu hata wa kunishauri. Hata hivyo, hayo tuyaache. Lakini ukweli ndio huo, lakini kwa sasa tumeachana, kila mtu ana maisha yake,” alisema Michael kwa masikitiko.
 
Michael ambaye kwa sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, pia alikiri kuwa mbunge huyo anashikilia vyeti vyote vya shule ambavyo anavihitaji sana kwa ajili ya kusaka ajira baada ya kumaliza masomo yake Muhimbili.

Alitaja sababu ya kuvunja ndoa hiyo kuwa ni manyanyaso kwa vile ni mdogo na masikini kwani hakuwa na sauti na alibanwa kwa kila kitu kiasi cha kukosa kabisa amani katika maisha yake.
 
“Kimsingi ndoa yangu na mama imevunjika na ilivunjikia mikononi mwa Rwakatare wakati akijaribu kutusuluhisha, alinitaka nirudi kwa mama, hapana, siko tayari na hapa nataka vyeti vyangu tu basi,” alisema Michael.

Mbunge ang’aka
Kwa upande wake, mbunge huyo alipoulizwa, kwanza alikuwa mbogo na kukataa katakata kuzungumza kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo zito kwenye simu.
 
Mbunge huyo alikiri kuwapo kwa ndoa hiyo, lakini alipinga kwamba haijavunjika na kumhoji mwandishi wa habari hizi kama anajua taratibu za kuvunja ndoa.
 
“Michael kakuambia hiyo ndoa imevunjika? Wewe si unajua taratibu za ndoa kuvunjika? Kwanza nimeshasema sitaki kuzungumzia suala hili kwenye simu ukitaka tuonane kesho kwani kuna haraka gani? Jambo la haraka ni la mjamzito kutaka kujifungua, lakini kama ni suala hilo hakuna sababu ya uharaka,” alisema mbunge huyo.
 
Hata hivyo baada ya kubanwa, mbunge huyo alimtaka mwandishi wa habari hizo kukutana naye katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ufafanuzi, lakini cha ajabu mwandishi alipofika katika ofisi hizo hizo, mama huyo alizima simu yake na  hakupatikana tena.

Mchungaji Rwakatare
Alipotakiwa kuzungumzia ndoa hiyo, Mchungaji Rwakatare kwanza aling’aka kwamba hajawahi kufungisha ndoa ya aina hiyo.
 
Lakini alipobanwa alikiri kuikumbuka ndoa hiyo na kwamba ilifungishwa na mchungaji wa kanisa lake, aliyemtaja kwa jina la  Mchungaji Mtetumo.
 
Alimtetea mchungaji wake kwamba alichokifanya ni kutimiza wajibu wake wa kichungaji wa kufungisha ndoa, hasa kama wanandoa wametimiza vigezo.
 
“Wajibu wa kanisa ni kufungisha ndoa, kama wanandoa wamekidhi vigezo vya kanisa. Sio kazi ya kanisa kuwachagulia wachumba kwa maana hakukuwa na sababu ya kuhoji umri wao, wala jambo lolote zaidi ya kufungisha ndoa hiyo,” alisema Mchungaji Rwakatare.

-Tanzania daima

Read More »

"Danny Mtoto wa Mama" anusurika kufanyiwa kitu mbaya baada ya kulewa pombe


Muigizaji wa filamu za kibongo anayejulikana kwa jina la Danny Cloud  maarufu  kama  Danny mtoto wa mama  ambaye  alipata  umaarufu  wa  jina  hilo  kupitia  filamu ya mtoto wa mama  amenusurika  kubakwa ( kuliwa kiboga )

Akizungumza  na  mwandishi  wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo  alidai kwamba  Danny  alikuwa maeneo ya Bilcanas  ambapo  alipewa  ofa  ya  pombe  na  jamaa  zake...

Rafiki huyo  alidai  kuwa, baada  ya  kupewa  ofa  hiyo  adimu, msanii  huyo  alianza  kuiparamia  pombe mfano  wa  mtu  mwenye  kiu  kali  ya  maji, hali  iliyomfanya  asijitambue  na  kuanza  kuvua  nguo...



"Kuna  wakati Danny  alinyanyuka  na  kuelea  chooni  huku  akipepesuka...Alipofika  huko  alidondoka  na kulala  huko huko chooni, hali  iliyowafanya   vibaka  watake  kumla  kiboga"...Alisema  huyo rafiki  yake  na  kuongeza:

"Baada  ya  kimya  kirefu, ilibidi  tukamwangalie  ambapo  tuliwakurupusha  vijana  watatu  wakiwa  wameshamvua  nguo"

Read More »

Kimemsibu Muuza chapati, Usitukane Wakunga.....!!!


Anachokifanya anti hapo pichani, si kigeni, anatengeneza chapati. Anti huyu huamka saa kumna1 asbuhi, akoke moto, akande unga, atengeneze chapati, akaange. Hii ni kazi yake ya kila siku. Anti huyu amekuwa akipika chapati miaka mi5 sasa, hivyo hivyo akiziuza kwa shida, maana kinachofuatia hapo ni kusubiri wateja, chapati moja TSH 200/=. Bahati, hapo jirani yake akahamia mdada mmoja, akawa mteja wake, anachukua chapati mbili kila siku anaenda nazo kazini. Mara yule mdada akaanza chukua nne, mara 8 mara 10, mara
akaweka oda ya chapati 100 kila siku. 

Mama akawa hana jasho la kuuza tena, yaani dada wa watu akifika tu analamba chapati 100 anasepa. Kwa vile anachukua 100, mdada akaomba awe anauziwa moja kwa 150/=, anti akaona inalipa, anti akakubali, mdada sasa akawa anachukua chapati 200 kila siku. Mama wa watu akaanza fuatilia kisirisiri, mdada anapeleka wapi? 

Kumbe yule dada anazichukua, anaenda nunua foil, anazifunga kwenye foil anauza Ofisini kwao na ofisi ya shosti yake jirani. Anauza moja Mia Tano. Mama kugundua, kaanza vimba, mara ananuna nuna, mara siku nyingine atengeneze 40 tu, mara aseme leo nnaumwa, mara leo nna oda kubwa dadaangu siwezi kukupa, basi akendelea hivyo ili mdada ashindwe. Mdada akamwambia anti naona mie niache tu. Anti akafurahi. Kesho yake anti akatengeneza 200 akamtuma mtoto wake wa kike akaziuze ktk zile ofisi mbili, unajua nini, aliuza 10 tu. Yule mdada alishaangaliaga plan B, anachukua kwa mama mwingine, tena anazipata kwa mia mia, sasa ana ofisi ya 3 anasaplai chapati 300 kila asbuhi. Kwa huyu mama mwingine jiko halikuwa zuri akampa jiko zuri na hotpots.

Tujifunze:

1. Ukiuza Samsung yako laki, aliyenunua akaenda uza milioni, piga kimya, haikuhusu!

2. Ukiona mwenzako anauza sana, usidhanie basi nawe unaweza anza chako ka kile ukauza sana, hujui siri ya biashara yake

3. Anti angetakiwa afurahie mafanikio ya mdada, fursa ya huyu anti ni kuomba masalahi, walau sasa aombe dada anunue kwa shs 170, ajenge hoja na sio kumfanyia visa.
4, HUYU MDADA ANANUNUA FOIL KUFUNGA CHAPATI
6. Endeleeni wenyewe....7.... 8..... 9.....


Source: mashughuli blog.

Read More »

Angalia "Swaga" za mtoto wa Wizkid


Dogo wa kiume huyo na ndo kwanza ana miaka 2 lakini ukimcheki unamwona ni matawi mengine kama alivyo baba yake. Picha hizo zimewekwa na mama yake Shola Ogudugu katika akaunt yake ya Instagram.



Read More »

Nick Minaj Awafagilia Wadada waliomshika Makalio.


Rapper Nick Minaj Ameandika kupitia Ukurasa wake wa Instagram kuwafagalia hawa madada wacheza uch* baada ya kumpapasa na kumshika makalio yake.

Read More »

Jamal Malinz, Mgombea Uraisi TFF, Azindua kampeni yake




Mgombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF 2013, Jamal Malinzi akizindua kampeni yake leo jijini Dar, mbele ya waandishi wa habari na wadau wa mpira wa miguu ambapo alielezea mikakati yake mbali mbali ya kuendeleza soka.
Mgombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF 2013, Jamal Malinzi akiongea na vyombo vya habari.
Wajumbe wa vyama vya soka nchini Tanzania wakifuatilia uzinduzi wa kampeni.
Waandishi wa habari wakiwa kwa wingi kufuatilia mgombea Jamal Malinzi wakati akimwaga sera zake mbele ya wajumbe.


Source:- GPL

Read More »

Diamond alivyowapagawisha mashabiki nchini China



Wakati ile movie ya Temptation  iliozua Gumzo Jijini iliyowakutanisha tena Msanii wa muziki Diamond na Mcheza Filamu Wa Tanzania Wema Sepetu ambao waliwahi kuwa wapenzi ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Diamond Na Wema Week End Hii diamond Amekua na Show Ya kukata na shoka huko Guangzhouhuku baadhi ya washabiki wakijiuliza mbona hawamuoni Maddam
Mkumbuke kuwa Maddam Na Diamond walikutana Hongkong na kwamba tayari Maddam amesharejea nchini, Labda show hiyo ni muendelezo wa Temptationambayo location yake kuwa inaonekana kuwa Nje ya Nchi.
Cheki picha za show hiyo:-
clip_image002[19]
clip_image002[4] 
 
clip_image002[25]
clip_image002[6]
clip_image002[8]
clip_image002[10]



Read More »

Ommy Dimpoz anunua gari la zaidi ya Mil 20, Angalia picha zaidi hapa.


Ni picha ambazo Ommy Dimpoz amezitoa Exlcusive kwa millardayo.com na AyoTV la hii Mark X aliyoiagiza kutoka Japan kwa gharama isiyopungua milioni 30 za Kitanzania, kuna video yake inakuja on AyoTV na itapatikana hapa millardayo.com pia
108
Ommy Dimpoz mara nyingi amekua mtu wa kutopenda kutangaza mali zake ila Camera za AyoTV na millardayo.com zilikutana nae Jaffarai Car wash Mikocheni Dar es salaam na kumuomba kupata pichaz, aliruhusu iwe hivyo kwa mtu wa nguvu ndio maana hizi picha zikafika hapa.
111
Anakwambia pesa yote iliyotumika kulinunua hili gani ni pesa iliyotokana na muziki peke yake, muziki wa bongofleva anaoufanya Ommy……. ili kupata pichaz nyingine za Exclusive pamoja na video, pia taarifa nyingine mbalimbali.
114
118
105
103
1
Credit: Millard Ayo.





Read More »

Auawa kwa wizi wa Kuku watatu, mmoja wa kuku ataga pembeni mwa mwili wa marehemu.


Ndugu wa marehemu Frank Shoka aliyetuhumiwa kwa wizi wa kuku mwili wake ukisubiriwa kuja kuchukuliwa napolisi
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula aliyesimama kushoto amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Polisi wakiuchukuwa mwili wa marehemu Frank









WAKATI jeshi la polisi Mkoani Mbeya likijitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, bado hali imezidi kushamiri baada  watu wawili kuuawa kwa tuhuma za wizi wa mifugo.

Matukio hayo ywmetokea katika Wilaya za Kyela na Mbeya vijiji yakiwemo ya wizi wa kuku na ng’ombe jambo lililopelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

Katika Tukio la kwanza lililotokea katika kitongoji cha Katusi kijiji cha Mjere wilaya ya Mbeya vijijini wananchi wamemuua Frank William Shoka(30) kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid(41)mkazi wa kijiji hicho.

Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao  alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20,mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manane na kuchukua kuku watatu wakati yeye akiwa amekwenda kumuuguza mwanae katika kituo cha Afya Mjere ambako aliandikiwa sindano za masaa.

Alisema Baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa na kuku hao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya,alipoulizwa juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.

Alisema mtuhumiwa huyo  baada ya kushindwa kutolea maelezo juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga kwa kutumia fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyomfanya kupoteza maisha papo hapo mita chache kabla ya kufikishwa katika ofisi ya kijiji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.

Aidha Baada  mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi na Daktari mwili ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa taratibu za maziko,hata hivyo wakati wa tukio hilo mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Mary Julius[30]alikuwa hayupo nyumbani akidai kuwa walikuwa wametengana.

Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.

Katika tukio la pili lililotokea kijiji cha Lupembe kata ya Katumba Songwe tarafa ya Unyakyusa wilaya ya Kyela Godfrey Mwakapalila mkazi wa kijiji cha Mpunguti aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.

Chanzo cha mauaji hayo ni wizi wa ng’ombe mali ya Moto Mwakiange(36) mkulima na mkazi wa kijiji cha Muungano tukio lililotokea majira ya saa mbili asubuhi octoba,19 mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la polisi linamshikilia Moto Mwakiange kwa mahojiano zaidi wakati upelelezi ukiendelea  wa kuwabaini watu waliohusika na mauaji,aidha mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkoani na atahakikisha wale wote waliohusika na mauaji wanakamatwa ili kujibu tuhuma za mauaji.

Picha na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu

Read More »

Top 5 ya mashabiki waliotokelezea baada ya kupiga picha katika Mapozi ya Diamond

 Kama unafatilia habari za mastaa wa Marekani utafahamu kuwa hii issue alishawahi kufanya rapper Nicki Minaj wa Young Money, Aliomba mashabiki watume picha wakiwa wamevalia mavazi kama yake na pozi zaki Nicki Minaj, Well Bongo Super Star Diamond amefanya yake kwenye instagram.
Picha zaidi ziko hapa.
 


 Kama unafatilia habari za mastaa wa Marekani utafahamu kuwa hii issue alishawahi kufanya rapper Nicki Minaj wa Young Money, Aliomba mashabiki watume picha wakiwa wamevalia mavazi kama yake na pozi zaki Nicki Minaj, Well Bongo Super Star Diamond amefanya yake kwenye instagram.
Picha zaidi ziko hapa.
 





Read More »

Msanii kutoka Uganda Afia katika Swimming Pool Tanzania


Mac Elvis alikuja Tanzania wiki mbili zilizopita kwa ajili ya concert Dar es salaam akiwa na wasanii wenzake kutoka Uganda ambao walirudi baada ya consert ila yeye akabaki ili kufanya kolabo na baadhi ya wasanii wa Tanzania.
Mtanzania Gee ambae ni rafiki yake, anasema ‘Alhamisi Elvis alikwenda kumtembelea rafiki yetu mmoja anaitwa Lulu (Sio mwigizaji) anaishi Mbezi Beach Africana ambapo Ijumaa jioni mida ya saa moja alijisikia kwenda kuogelea kwenye swimming pool, Lulu alimwambia asiogelee kwa sababu ilikua usiku umeshaingia lakini Elvis aliiamua kuogelea hivyohivyo’
‘Lulu alitoka nyumbani kidogo wakati huo Mac akienda kuogelea akiwa mwenyewe, ilikua ni kawaida kwake kuogelea mara nyingi huwa anapenda kuogelea hivyo hakikua kitu kigeni… Lulu aliporudi hakumuona Mac manake hakurudi hivyo akadhani mwimbaji huyu ameshaondoka, akawa anampigia simu rafiki anaeishi na Mac lakini haikupokelewa

‘Kesho yake mida ya saa nne mlinzi ndio akaona nguo pembeni na aliposogelea akaona mwili wa Mac ndani ya swimming pool chini ambapo baada ya kutolewa alionekana akiwa na jeraha kwenye paji la uso hivyo inaonekana alijigonga alipojirusha, tumbo lake halikujaa maji kama ambavyo ilidhaniwa, tayari mipango ya kumsafirisha imekamilika na anapelekwa kwao Uganda leo October 22 2013′

Read More »

Watu waliokufa wazidi "KUFUFUKA" mkoani Geita


HOFU imezidi kutanda kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kufuatia matukio ya watu waliofariki dunia na kuzikwa miaka iliyopita kuibuka wakiwa hai, Uwazi lina mkasa mwingine mpya.
Flora Onesmo (45) aliyefariki dunia Februari 28, 2008 baada ya kufufuka Aprili 12, 2013 katika Kijiji cha Kasamwa wilayani Geita.
Mgonda Thomas (22), aliyefariki dunia kwa kujinyonga Mei 28, mwaka jana na kuzikwa siku iliyofuata, Ijumaa iliyopita aliibukia karibu na mlango wa nyumbani kwao akiwa hai.
Tukio hilo ambalo bado la moto, lilijiri katika Kijiji cha Rumasa, Kata ya Buseresere, wilayani  Chato mkoani Geita.
Kwa mujibu wa chanzo, majirani ndiyo waliomshuhudia Mgonda akitembea barabarani saa tisa alasiri hatua chache kutoka kwenye mlango wa nyumba hiyo huku nguo zake zikiwa zimechakaa.
Shaban Maulid (16) aliyefariki dunia Januari 1, 2011 ambaye aliibukia Mtaa wa Mbugani jirani na nyumbani kwao, Kata ya 14, Kambarage mjini Geita.
Baba mzazi wa kijana huyo, mzee Thomas Msalaba (60) akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema majirani hao ndiyo waliomtaarifu kwamba mwanaye Mgonda alikuwa barabarani.
“Niliondoka kwenda kumshuhudia kama kweli ni mwanangu. Nilipofika, nilimchunguza kwa umakini sana na kubaini alikuwa yeye.
“Alama kubwa iliyokuwa kwenye mwili wa mwanangu ni kovu kwenye mkono wake wa kushoto lililotokana na kuungua moto, pia sura yake ilifanana sana na mama yake,” alisema mzee huyo.
Naye mama mzazi wa Mgonda, Martha Kitobelo alimthibitishia paparazi wetu kuwa kijana huyo ni mwanaye kweli.
Familia hiyo ilisema Mgonda alifariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia kamba aliyoifunga juu ya mti wa mwembe hatua chache kutoka nyumbani kwao. Haikujulikana chanzo cha kujinyonga.
Mzee Msalaba alisema kuwa, baada ya Mgonda kufariki dunia alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao na siku ya tatu ndugu walianua matanga.
Kufuatia hali ya Mgonda kuwa ya mawengemawenge na kushindwa kuzungumza, wazazi wake walimchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji wa eneo hilo aitwaye Juma Tabiho.
Mganga huyo alisema kijana huyo hakufa bali alichukuliwa msukule na maiti waliyoizika ilikuwa kiini macho.
Hata hivyo, katika tukio hilo Jeshi la Polisi Wilaya ya Chato likiongozwa na Mrakibu wa Polisi Wilaya, OCD Leonard Nyaoga lililazimika kufanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi waliopandwa na hasira waliotaka kufukua kaburi ili kuona kilichokuwa ndani.
Afande Nyaoga aliwaambia wananchi hao kwamba kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi na kuwaeleza kuwa chombo chenye uwezo wa kutoa kibali cha kufukua kaburi ni mahakama peke yake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Pudensiana Protas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi unaendelea ikiwa ni pamoja na kufanya utaratibu wa kumpima DNA kijana huyo ili kujiridhisha kama kweli ndiye Mgonda aliyefariki dunia mwaka jana.
Hili ni tukio la tatu kutokea mkoani Geita katika kipindi kisichozidi miaka mitano iliyopita.
Aprili 12, 2013 katika Kijiji cha Kasamwa wilayani Geita, Flora Onesmo (45) aliyefariki dunia Februari 28, 2008 aliibuka akiwa hai.
Septemba 28, mwaka huu aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mwatulole mjini Geita, Shaban Maulid (16) aliyefariki dunia  Januari 1, 2011 naye aliibukia Mtaa wa Mbugani jirani na nyumbani kwao, Kata ya 14, Kambarage mjini Geita.
Kufuatia matukio hayo yenye dalili za ushirikina, Askofu wa Kanisa la Zion Assemblies of God Geita, Edward Osako alisema katika maandiko hakuna binadamu aliyewahi kufa kisha akafufuka zaidi ya Lazaro aliyefufuliwa na Yesu akiwa kaburini.
“Haya matukio ya watu kufa na kuonekana wakiwa hai baada ya miaka kadhaa ni nguvu za giza ambapo hata kwenye Biblia yameandikwa,” alisema Askofu Osako.

chanzo: Global Publishers.

Read More »

Cheki Lulu alivyopozi na Bibi yake, wamefana au?


Hiyo ndo picha ya msanii Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa amepozi na Bibi Yake, Wamefanana sana, au macho yangu yanadanganya?

Read More »

Msanii wa Filamu alalamika kupewa kidogo na Mumewe


Huyo ni mwanadada Maheeda kutoka nchini Nigeria, amefunguka na kusema anachoshwa na Tabia ya Mumewe huyo kuwa busy zaidi na kazi na kumsahau yeye mkewe, akaongeza ya kwamba huyo mwanaume huwa na tabia hata ya kuchagua kunywa kahawa na kumsusa binti huyo ambaye binafsi anajikubali ana mvuto.

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger