Mwanamke ajifungua Mtoto anaye fanana na "Nyani"
Mwanamke mmoja amejifungua mtoto mwenye sura mfano wa Nyani huko Kaduna, Kagarko Nigeria vijijini. Imeelezwa kuwa mwanamke huyo alijifungua kiumbe hicho chenye miguu ya tofauti, maskio pamoja na uso kwa ujumla. Hata hivyo mtoto huyo alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa kutokana na kutokwa na damu sana wakati manesi na madaktari wakihangaika kumleta duniani.
Hali ilikuwa tofauti tangu ndani ya chumba cha uzazi kwani mtoto huyo alitanguliza miguu.