Aota maziwa baada ya kuiba Ng'ombe wa Watu
Wakati mwengine huwa nacheka na kushangazwa na kutokana na habari ambazo binafsi zinanifikia, ila ni kazi yangu ya kuzifikisha kwenu na kuwaachia ninyi kuweza kufanya maamuzi ya kuamini au kutoamini.
Jamaa huyu mwenye umri wa miaka 40 kutoka Nherera ndani ya Mhondoro, Zimbabwe gafla maziwa yake yalianza kukua kwa kile kinachoelezwa kuwa aliiba ng'ombe wa mtu mmoja na kisha kuwauza.
Wanakijiji wa sehemu hiyo wanasema kuwa jamaa huyu aliyefahamika kama Acry Chinhivi Shayamano amefanyiwa kitu hiyo mbaya na aliyeaminika kuwa ni mmiliki wa ng'ombe hao.