Kiganja cha Binadamu champeleka Mchina Mbaroni
Mkono wa mtu uliopatikana kandokando ya Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Viroba na Plastiki, Mabibo jijini Dar.
Dada wa kijana anayedaiwa kuwa mwenye mkono huo, Rehema Rashidi akihojiwa na mwandishi wa ITV, Sam Mahela.
Mmiliki wa kiwanda hicho, Lee Sliim, akiwa ndani ya gari la Polisi kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.
DUNIA inaimba sandakarawe! Mwenye kupata sasa anapata na mwenye kukosa hana chake tena! Mwekezaji mmoja wa kiwanda cha Urafiki Plastic Co. Ltd kinachokihusisha na utengenezaji wa mifuko ya viroba na palstiki ambaye ni raia wa China, Lee Slim amekamatwa kwa tuhuma za kuonekana kwa mkono wa mtu karibu na kiwanda chake, tukio hili limetokea mchana huu maeneo ya Mabibo, jijini Dar es salaam. Mkono huiop unadaiwa kuwa ni wa mfanyakazi wa kiwanda hicho, kijana Jumanne Rashid.
GPL.