Mrembo abaki Uch! baada ya kulewa na kuibiwa Mkoba wake Mchana Kweupe.
TIMBWILI! Mrembo wa haja ambaye jina halikupatikana mara moja, amenaswa akiwa matiti ‘nido’ nje baada ya kulewa tilalila mchana kweupe na kulizwa mkoba wake kisha kuzua varangati ‘hevi’, Ijumaa Wikenda lina mkanda kamili.
Varangati hilo lililonaswa na kachero wetu aliyekuwa kwenye ‘patroo’ ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM), lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza- Afrika Sana jijini Dar.
Katika sinema hiyo ya bure, mrembo huyo alishuhudiwa akipigana na kila mtu aliyekutana naye mbele yake huku akivua nguo kuashiria kuwa ‘pombe si chai’.
Kuna wakati mwanadada huyo alikatiza barabarani bila kujali magari na nusura agongwe jambo lililosababisha mtafaruku wa foleni huku mwenyewe akidondoka kama ‘embe dodo’ lililoiva.
Baada ya timbwili hilo kuchukua takriban dakika 35, ilibidi wasamaria wema kuingilia kati na kumshika huku akiwapiga baada ya kuona huenda angeumizwa.
Baadaye watu hao walifanikiwa kumtoa eneo la barabara huku wakimsitiri kwa kupandisha nguo kufunika nido kisha kumpeleka pembeni na kumtuliza.
“Kweli pombe siyo chai. Yaani msichana mzuri lakini ona alivyojidhalilisha,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Gazeti hili lilitaka kujua kulikoni kuwa katika hali hiyo ambapo mrembo huyo alijibu kwa kifupi kuwa kuna mtu alimuibia mkoba wake hivyo akawa hana namna nyingine zaidi ya kufanya fujo kutokana na hasira.