Showing posts with label Bongo Flavor. Show all posts

Kwa Staili Hii, Ali Kiba Atasubiri sana Mbele ya Diamond ikiwa hataki kubadilika.


Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.
Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.

Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.

Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!

Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa airtel hands across the world waliopiga wakina r.kelly,fall ipupa,2 face kama nafac ile angeipata diamond leo angekuwa wapi?
Diamond leo anatuletea remix ya number 1 f.t Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata kutuletea remix ya Dushelele f.t Fally ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anaejua biashara ya mziki ilivyo labda pengine ni management yake inayomsimamia.Diamond kaweza kuubadilia mziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa show.

Nampenda ali kiba,naipenda sauti yake,anajua mziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na kukubali soko la mziki linataka nini.

Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila usipokuwa makini utajikuta nyuma ya rich,barnaba,dimpoz na ben pol maana mziki sio kuimba peke yake mziki ni biashara pia


Read More »

Diamond na Davido ndani ya remix ya " My number one "


 Davido na Diamond wameamua  kuingia  studio na kufanya remix ya wimbo wa My number one  wa  msanii Diamond.

Wimbo huo wali-perform kwa mara ya kwanza kwenye show ya fiesta iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders club.Bado taarifa za uwezekano wa wawili hao kufanyia video ya wimbo  huo hazijatoka..
 
 Show ya pamoja kati ya Diamond na Davido ilikuja baada ya show kali aliyofanya Davido ambayo ilivutia wapenzi wengi wa muziki waliofika kwenye uwanja wa Leaders kwa ajili ya kuangalia performance za wasanii ambao hawakuweza kupanda usiku wa Jumamosi.




Read More »

Baadhi ya picha za FIESTA jana pale Leaders Club










 







 





 


 

Read More »

Sakata la Kuvaa Mlegezo (Kata K), BASATA wamvaa Ney wa Mitego.


Ney wa Mitego ambae ni staa wa single za ‘muziki gani’ na ‘salamu zao’ amethibitisha kupewa barua na baraza la sanaa Tanzania ikiwa ni onyo la kutoendelea kuvaa suruali mlegezo kwenye majukwaa mbalimbali anayoonekana.
 
 Kwenye interview yake na millardayo Ney amesema alipigiwa simu sana na namba moja lakini alikua amelala, alipoamka akakuta missedcalls nyingi so ikabidi apige ndio akaambiwa BASATA kuna barua yake ambapo baada ya kushindwa kwenda alipelekewa Manzese.
 
 Ney anasema: "Sielewe kama BASATA ndio wameamua kudili na milegezo, sijaelewa wao wanaangalia nini zaidi, nimejaribu kuuliza wakasema nikiendelea watanifungia kazi zangu....

"Ni kweli navaa mlegezo lakini kuna vitu vingi sana vya kufanyia kazi wao kama BASATA manake tunaibiwa kazi zetu kila siku mbona hawashughulikii hizo?’

"Mi tangu niko shule mlegezo ni tatizo langu kubwa ila nitajitahidi kupunguza japo nashangaa nimeandikiwa barua mimi mwenyewe wakati kuna wasanii wanavaa mlegezo hata kuliko mimi"





Read More »

Bangi, Pombe na Utovu wa Nidhamu vyamponza Dogo Janja


Dogo Janja atimuliwa Mtanashati Entertainment.....Makosa yake ni kuvuta bangi na kutoenda shule

Akizungumza na Mtandao huu, kiongozi wa Mtanashati Entertainment Ustaadh Juma Namusoma alisema kuwa sababu za kumtimua Dogo Janja ni utovu wa nidhamu, unywaji pombe, kutokwenda shule pamoja na uvutaji bangi.
 
 Aliongeza kuwa tayari amempatia nauli ya shilingi 90,000/=  kurudi nyumbani kwao jijini Arusha alipotokea. Dogo Janja alitua kwa mbwembwe jijini Dar es Salaam kwa ndege Juni 22 mwaka jana akitokea Arusha na kujiunga na kundi hilo.
 
 Awali alikuwa katika kundi la Tip Top Connection linaloongozwa na Madee lakini ilitokea kutoelewana kati yao na kurudishwa kwao Arusha.

 Alipopigiwa simu , Dongo Janja alidai kuwa bado ni memba hai wa Mtanashati Entertainment.

Read More »

Diamond alivyowapagawisha mashabiki nchini China



Wakati ile movie ya Temptation  iliozua Gumzo Jijini iliyowakutanisha tena Msanii wa muziki Diamond na Mcheza Filamu Wa Tanzania Wema Sepetu ambao waliwahi kuwa wapenzi ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Diamond Na Wema Week End Hii diamond Amekua na Show Ya kukata na shoka huko Guangzhouhuku baadhi ya washabiki wakijiuliza mbona hawamuoni Maddam
Mkumbuke kuwa Maddam Na Diamond walikutana Hongkong na kwamba tayari Maddam amesharejea nchini, Labda show hiyo ni muendelezo wa Temptationambayo location yake kuwa inaonekana kuwa Nje ya Nchi.
Cheki picha za show hiyo:-
clip_image002[19]
clip_image002[4] 
 
clip_image002[25]
clip_image002[6]
clip_image002[8]
clip_image002[10]



Read More »

Ommy Dimpoz anunua gari la zaidi ya Mil 20, Angalia picha zaidi hapa.


Ni picha ambazo Ommy Dimpoz amezitoa Exlcusive kwa millardayo.com na AyoTV la hii Mark X aliyoiagiza kutoka Japan kwa gharama isiyopungua milioni 30 za Kitanzania, kuna video yake inakuja on AyoTV na itapatikana hapa millardayo.com pia
108
Ommy Dimpoz mara nyingi amekua mtu wa kutopenda kutangaza mali zake ila Camera za AyoTV na millardayo.com zilikutana nae Jaffarai Car wash Mikocheni Dar es salaam na kumuomba kupata pichaz, aliruhusu iwe hivyo kwa mtu wa nguvu ndio maana hizi picha zikafika hapa.
111
Anakwambia pesa yote iliyotumika kulinunua hili gani ni pesa iliyotokana na muziki peke yake, muziki wa bongofleva anaoufanya Ommy……. ili kupata pichaz nyingine za Exclusive pamoja na video, pia taarifa nyingine mbalimbali.
114
118
105
103
1
Credit: Millard Ayo.





Read More »

Diamond Ala Shavu la Kutangaza Coca cola, Angalia Picha za Uandaaji wa Tangazo Hilo.





Hizo ni Baadhi ya Picha Ambazo Msanii Diamond Platnumz Aliziweka katika Instsgram yako akionesha jinsi hali ilivyokuwa katika utengenezaji wa Tangazo la Soda ya Cocacola Huko South Africa.



Diamond Alikuwa Miongoni mwa Abiria waliokwama jana kutokana na ajali ya moto katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, na aliendelea na Safari baada ya kukodiwa Ndege Binafsi na Coca Cola.


Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger