Showing posts with label Maisha. Show all posts

NANI KAMA MAMA?


Pichani ni mwanamke, mlemavu mzazi wa mtoto mchanga akimuhudumia kichanga wake kwa huruma na mapnz ya hali juu na hasa ukizngatia hali ya hali ya mikono yake. Nani kama mama?!!

Read More »

SHABIKI WA MAN U KENYA AJIUA BAADA YA KIPIGO CHA NEWCASTLE




Jamaa mmoja anayeaminika kuwa ni shabiki wa timu ya Manchester United mnamo siku ya Jumamosi usiku kwenye Jimbo la Pipeline jijini Nairobi, hii ni mara baada ya timu yake kufungwa goli 1-0 na Newcastle.

Polisi wamesema John Jimmy Macharia, mwenye miaka 23, alijirusha toka kwenye gorofa ya saba mara baada ya timu yake kupoteza mchezo mwengine kwenye mechi iliyochezwa Jumamosi jioni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake kuwa hawezi kuona timu yake ikifungwa mfululizo kabla ya kuamua kujirusha na kufa papo hapo.

“Wote walioshuhudia wanasema sababu ya jamaa kujiua ni kutokana na timu yake kufungwa ila maafisa wanaendelea kuongea na watu waliyekuwa nae kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.

Kibue aliwashauri vijana wa jiji hilo kutambua kwamba Ligi Kuu ya Uingereza ni kama aina nyingine ya michezo hivyo wanapaswa wasiwe wanaguswa sana kihisia na michuano hiyo.

“Sio mara ya kwanza kumpoteza kijana sababu ya Ligi ya Uingereza, ambayo ipo mbali na sisi, wanahitaji kujua kwamba hii ni michezo tu,” alisema Kibue.

Mwili wa marehemu ulitolewa na kupelekwa mochwari na polisi waliofika pale. Macharia inasemekana aliangukia kichwa pindi alipojirusha toka kwenye gorofa hilo.


Read More »

MWANGALIE MODEL HUYU AKIWA NDANI YA BIK1NI NA KAPTURA WAPI KAPENDEZA ZAIDI



Kwa jina anafahamika kama Risper Faith ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akipiga picha zake za Ki Model akiwa amevaa nguo zote, sasa ameanza kufuata nyayo za dada yake na kuanza kutuvalia vibikn bila kujali umbo lake kubwa alilobarikiwa na Mola.

Kazi imewapata wengi kwa ku koment na kushauri kuhusiana na step mpya ya mrembo huyo, je sawa kwake au aendelee ku modelika huku akiwa na nguo tu?!!!



Read More »

WAVULANA WA CALIFORNIA WAMEANZA KUONGEA KAMA WASICHANA- UTAFITI


Vijana wengi wa kiume kwenye jimbo la California wameanza kuongea kama wasichana, kwa mujibu wa uchunguzi mpya.

Wataalamu wa lugha wanaamini kumekuwa na ongezeko la  wanaume kuongea 'kwa sauti ya juu' mwishoni mwa sentensi kama vile wanauliza swali.

Wavulana wengi wanaanza kuongea kwa sauti ya juu kuelekea mbele, aina ya uongeaji ambao wanawake hutumia kuongea, hii ni kwa mujibu wa somo hilo.

Read More »

Waziri mkuu wa Latvia ajiuzulu kutokana na maafa yaliyoikumba Taifa hilo


Waziri mkuu wa Latvia, Valdis Dombrovskis, ametangaza kujiuzuru wadhifa wake mara baada ya kujiona kisiasa kuwa anahusika na kuanguka kwa paa la supermarket ambalo lilisababisha vifo vya watu 54 na kujeruhi wengine 40 wiki iliyopita, hivyo ana kila sababu ya kuwajibika kutokana na tukio hilo, Associated Press imetaarifu.

Paa la Supermarket ya Maxima iliyopo ndani ya Riga lilianguka siku ya Alhamisi Novemba 21 likiuwa watu kadhaa wakiwamo wakowaji watatu na wengine 39 wakiwa wameumia vibaya sana.

Kuanguka kwa paa la supermarket hiyo ni janga kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa nchi hiyo ya Latvia toka mwaka 1950.

Nasi tujifunze kuwajibika....

Dc.

Read More »

Kajala, Kupanda Kizimbani tena, Rufaa ya Mumewe yaweza kukwamisha Uraiani.



Kajala Masanja.
Msanii wa filamu Kajala Masanja atahukumiwa upya Novemba 25 mwaka huu, baada ya mumewe kukata rufaa. Hukumu ya rufaa ilibidi isomwe leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam lakini imeahirishwa baada ya Jaji aliyetakiwa kusoma hukumu hiyo kupata hudhuru!



Read More »

Taswira katika ajali iliyoua watu 7 huko Morogoro Leo


...Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.…

Toyota Noah yenye namba za usajili T502 AUP iliyokuwa ikitoka wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini baada ya kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB.
...Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.
...Muonekano wa Toyota Noah kwa nyuma baada ya ajali.
...Ndani ya Toyota Noah baada ya ajali.
Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora baada ya kugongana uso kwa uso na Toyota Noah yenye namba za usajili T502 AUP.
Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB baada ya ajali.
 
WATU saba wamekufa papo hapo kwenye ajali mbaya iliyotoka leo alfajiri katika kijiji cha Dakawa - Sokoine Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyohusisha gari ya abiria aina ya Noah yenye namba za usajili T 502 AUP iliyokuwa ikitoka Wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora.

Watu saba wamepoteza maisha katika ajali huyo akiwemo dereva wa Noah aliyejulikana kwa jina la Masoud Juma na wengine wanne hali zao ni mbaya.

 "Chanzo cha ajali hii ni dereva wa Noah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla akakutana na lori uso kwa uso" Alisema Bw. Sanjo Ole ambaye ni mfugaji jamii ya Kimasai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
 
CREDIT: globalpublishers.info



Read more: http://mambomseto88.blogspot.com/2013/11/updates-taswira-ya-mapicha-katika-ajali.html#ixzz2l1rPhS3i

Read More »

Kova Amtetea Kapuya Dhidi ya Tuhuma za Ubakaji na Kumwambukiza Mwanafunzi VVU


Akiongea na wanahabari leo mchana kamanda kova kasema hawawezi kumuita Mhe. Kapuya kasababu haya ni mambo yake binafsi na hakuna mtu yeyote ambaye amakuja hapa polisi kulalamika kutendewa vibaya na Mhe. Kapuya.

"hata hivyo kamanda kova kasema kama kuna ushahidi wowote wa kueleweka sio kusingizia mtu vituo vya polisi viko wazi masaa 24"


Read More »

Pastor Ajiua, alisema Mungu Hamskii Tena


Mchungaji Teddy Parker kutoka Georgia Marekani amejiua siku chache baada ya kuhubiri kanisani kwake kwamba Mungu hamsikii tena na wala ahisi muungane wake na Mungu tena.

" Najaribu kuomba, lakini nahisi Mungu anisikilizi tena, najitahidi kuhudumia lakini nahisi Mungu ahitaji kunitumia  tena, zipo zama katika maisha ya binadamu ambazo Mungu kwa makusudi maalum hukuondoa, hakutoi ili ubaki peke yako ila hukufanya ukue na kujitambua zaidi" Alisema Teddy.

Parker, baba wa watoto wawili alijiua Jumapili iliyopita kwa kujipiga risasi kichwani na bastola yake baada ya kumaliza misa ya kwanza, watu walikuwa wakimngojea arudi kwa ajili ya misa ya pili na hakutokea, haikuwa kawaida na ndipo walipoenda kumuangalia walikuta ameshafariki.


Read More »

Ushauri: Baada ya kugundua Mpenz anatembea na mtu mwingine!


Kutoka katika Mtandao wa Kijamii;

Wadau  naombeni ushauri wenu kijana mwezenu yamenikuta, mimi nina girlfriend tangu mwaka jana, nimekuwa nikimpa support ya shule kama ada na mahitaji mengine kadri ninavyoweza.

Mwaka jana aliombwa na dada yake akampe campani huko mbagala kwaani alikuwa amepata mtoto mchanga. Tangu aende kuishi kwa dada yake alianza kubadirika katika mawasiliano, aliniambia kuwa hakuwa free kama alipokuwa kwa wazazi wake temeke.

Kwaani kila nikimhitaji ilkuwa ni ngumu au kwa nadra sana mfano tuliweza kuonana mara moja kila baada ya miezi 1-2. Mawasiliano yetu makubwa yalikuwa ya simu. Kwa sababu ya mawasilano yetu kuwa finyu tuliweza kutofautiana mara kwa mara hivyo hata ile support yangu ikawa inapungua kwa sababu ilikuwa ni lazima niende kwenye tigopesa kumuwezesha nayopia ilitegemea nimepata muda gani kulingana na mazingira ya kazi yangu.

Bahati nzuri mp3nz! wangu amerudi nyumbani kwa wazazi sasa yapata mwezi mmoja na tunaweza kuonana mara kwa mara na mahusiano yetu yamestawi vizuri tena. Kwa bahati mbaya juzi siku ya Eid simu yangu nilimwazima mdogo wangu alikuwa amepoteza simu yake huku akiwa na issue ya pesa.

Hivyo mp3nz!wangu hakuweza kunipata alichukia sana mpaka akawa hapigi simu wala hajibu sms zangu kwa muda wa siku 3. Jumatatu wiki hii baada ya kazi nilienda kujua kulikoni, aliponiona tu aliniambia nimefuata nini? Nilimshangaa sana, akasema kuwa najifanya sijui kwa nini sikupokea simu yake siku ya Eid.

 Nilimwelewesha na kumwomba msamaha. Baadae nilimuuliza kuwa nilikuwa nimeona gari pale nyumbani kwao na nikajifanya kama nimepata taarifa kuwa ni ya mtu wake, alinijibu kuwa kwa hiyo nina amuaje..??

Niliamua kuchukua simu yake kwa nguvu nikaondoka nayo. Usiku iliingia sms iliyikuwa inamtaka wakafanye map3nz! kwaani ilikuwa yapata miezi 4 tangu wafanye mala ya mwisho. Sikuamini nilichokiona.

Jana jioni nilienda kukutana nae na kumuuliza kuhusu sms hiyo alilia na kuomba nimsamehe kwani alifanya mara moja kwa kuwa hatukuwa na mawasiliano mazuri kipindi hicho akiwa Mbagala eti alihisi tulikuwa tumeachana na alikuwa na shida ya shule hivyo ilimbidi kumkubali mtu bila kupenda. Zaidi aliniambia kuwa mbona yeye alinisamehe mwaka jana alipopata ujauzito tukautoa hata bila ya wazazi au dada yake kujua? Ni kweli tulitoa mimba ya mwezi 1.5. Lakini tulishauliana kuwa asome kwanza hayo mengine ndiyo yafuate. Akakubari.

Wadau naombeni ushauri wenu nifanyeje kijana mwenzenu yamenikuta na binti nampenda lakini kwa sababu ya hili la kutokuwa mwaminifu nimemwambia kuwa tangu jana tumeachana, kiukweli usiku kucha sijapata usingizi hata dk 1. Hapa nilipo nawaza sana. Na yeye ananiomba msamaha hatarudia ilitokea bahati mbaya.


Read More »

Dereva wa Bodaboda Akatika Mguu baada ya Kugongwa na Roli la Mizigo




Dereva wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka sasa (kwani hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu wake wa kulia mara baada ya kugongwa na roli la mchanga katika eneo la daraja la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwandishi wetu aliyeweza kuwahi kufika ktk eneo la tukio na kutoa msaada wa gari kumfikisha dereva wa pikipiki hiyo aliyopata ajali Hospitali ya Rufaa ya Bugando, annasema kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Mkolani kuelekea Buhongwa na Roli hilo lilikuwa likitokea Buhongwa kuelekea Mkolani, imetokea wakati dereva wa roli 'akiovateki' daladala iliyokuwa mbele yake ikibeba abilia, hivyo alipoipita tu daladala hiyo akakutana uso kwa uso na bodaboda.
Baadhi ya bodaboda na wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD Kanda ya Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.
Sambamba na kuvunjika mguu pia dereva huyo amevunjika vidole vitatu vya mkono wake wa kulia. 

TWAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI 


Read More »

Baada ya Miaka 80 ya kuishi pamoja, wafunga pingu za Maisha.


Kisa chao cha Map3nzi kilianza miaka 6 kabla ya kutokea vita ya pili ya dunia, mpaka sasa imepita miaka 80 (Themanini )tangu Wap3nzi hao wakutane na kupendana na hatimaye kuanza kuishi pamoja mnamo mwaka 1933.

Jose Manuel Riella, 103 alichukua kiapo cha ndoa kwa mkewe Bi Martina Lopez, 99 wote raia kutoka Paraguay katika sherehe iliyohudhuriwa na wanandugu. Mpaka sasa wanandoa hao wamejaaliwa kupata watoto 8, wajukuu 50, vitukuu 35 na vining'ina 20.

Mchungaji aliyewafungisha ndoa hiyo ya kanisani amekiri kuwa katika maisha yake yote hajawahi kufungisha ndoa mpya ya watu wenye umri mkubwa kama huo. Awali wawili hao walifunga ndoa ya Kiserikali miaka 31 iliyopita lakini wameona muda umefika wafanye ndoa ya ki imani zaidi,



Read More »

Akutwa na Maiti ya Mtoto ndani ya Begi Lake, Angalia Video.


Hii inaonyesha wazi dunia inakoelekea kijana huyu alikamatwa siku chache zilizopita huko nigeria akiwa na maiti ya mtoto mdogo kwenye begi. Jamaa huyu anasadikiwa kumteka nyara mtoto huyo na kumweka katika Begi hilo hadi Umauti ulipomfika.

Read More »

Zaidi ya Watu 10,000 Wahofiwa Kufa na Mamilioni Hawajulikani Walipo kutokana na Kimbunga Kikubwa Katika Historia Yakikumba Nchi ya Philippines.


Kimbunga kikubwa kimeikumba Philippines mnamo siku ya Ijumaa, kikiuwa zaidi ya watu 10,000 na kujeruhi watu wengi huku wengine kutofahamika walipo.

Kimbunga hicho ambacho kimepewa jina la Haiyan, kinaaminika kuwa ndio kimbunga kikubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia Duniani kinakadiliwa kuwa na ukubwa wa 235mph kwa 170mph.



Kimbunga hicho kimeharibu miundombinu mingi, huku kikisababisha huduma za umeme na mawasiliano kuvurugika kitu ambacho kimesababisha usumbufu na uhalibifu mkubwa sana.

Maelfu ya nyumba yameanguka na kubomoka huku miili ya binadamu ikiwa imetapakaa mitaani.


Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea Barani Asia ni kinategemea kufika Pwani ya nchi ya Vietnam siku ya Jumapili asubuhi huku ikielezwa kwamba kuna uwezekanao mkubwa wa idadi ya waathilika kuongezeaka.

Angalia picha za kuhuzunisha zaidi hapo chini:













Read More »

Mtoto Huyu anateseka, Mzazi aomba Msaada.


MTOTO Khalidi Juma mwenye umri wa miaka minne, mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, yuko katika mateso makali baada ya jicho lake moja kutolewa katika harakati za kumnusuru na ugonjwa wa Kansa, huku lingine nalo likilegea.
Mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo.
 Akizungumza  mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo, alisema alimzaa mtoto huyo akiwa na afya njema, lakini alipofikisha umri wa miezi tisa ndipo alipogundua kitu cheupe kwenye mboni ya jicho lake.
 Baada ya hali hiyo, alisema alimpeleka katika hospitali inayotibu watu wenye ulemavu mbalimbali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar, ambako baada ya kupimwa, aliambiwa mwanaye alikuwa na kansa.
Mtoto Khalidi Juma  jicho lake moja limetolewa katika harakati za kumnusuru na ugonjwa wa Kansa.
 “Baada ya kuambiwa mtoto wangu ana ugonjwa wa kansa sikuwa na jinsi, nilikubali afanyiwe upasuaji kwa ajili ya kuliondoa jicho hilo ili kuokoa maisha yake,” alisema.
 Mama huyo alisema ilipofika mwaka 2012, jicho lingine lilianza kumuuma huku likiwa linavimba, lakini alipompeleka katika Hospitali ya Muhimbili, aliambiwa kansa imeshaenea mpaka kwenye ubungo, hivyo arudi naye nyumbani kwani hawezi kuishi kwa muda mrefu.
 “Kwa kweli nilivyoambiwa hivyo nilinyong’onyea mwili mzima nikawa sina jinsi kabisa na nikapoteza matumaini kabisa ya mwanangu kuendelea kuishi tena,”alisema.
 Alisema alirudi nyumbani huku maumivu ya kijana wake yakiendelea na mwishoni, jicho lake likawa halioni tena. Kuhusu jicho lililotolewa, mama huyo alisema alikuwa akilitoa na kulirudisha kwa ajili ya kulisafisha, lakini hivi sasa hawezi kulitoa tena kwa vile kuna nyama zilizolishika na hivyo kumsababishia maumivu makali mno mwanaye hasa kichwani.
 “Unavyotuona hapa usiku hatulali kabisa, mtoto ni kulia kwa maumivu, amefikia wakati hawezi kula vizuri na anatumia muda mwingi kulia,” alisema.
 Mama huyo aliongeza kueleza kuwa kutokana na hali ya mwanaye, anakosa muda wa kufanya chochote cha kujiingizi kipato, hivyo kuwa katika wakati mgumu mno kimaisha, hasa kwa vile baba mzazi wa mtoto huyo alimkimbia tokea alivyoanza kuumwa.
“Mimi naamini kabisa labda nikipata msaada nikienda hata kwa wachina nitapata hata dawa ya kumpunguzia mtoto wangu maumivu anayoyapata kwa hivi sasa,” alisema.
Kwa ye yote ambaye ataguswa na habari hii na angepeta kutoa msaada wa aina yo yote, anaweza kuwasiliana na mama mzazi anayetumia simu nambari 0656 042017.


Read More »

Kiingereza cha Shilole chazua Gumzo Mtandaoni.



Shilole aliamua kutandika yai kwenye Instagram, ili kuzipa uzito shukrani zake za dhati kwa muongozaji wa video yake ya ‘Nakomaa na Jiji’ itakayotoka Jumamosi hii, Nisher.
Bahati mbaya, yai lake lilivunjika mapema wakati lilipokuwa likiufikisha ujumbe huo na kuwafanya watu waligeuzie mjadala.
Kama tumekuacha kwa lugha hiyo, ni kwamba Shilole aliandika Kiingereza kilichokosewa sarufi aka Broken English.

Shilole aliandika: I did ever think I would do a nice video like this thank you alot to my director @nisherbybee.

Baada ya hapo, haya ndio yaliyosemwa:
    [ @ ] nicrac1914 Lugha za majahazi!! Ongea Kiswahili tu utaeleweka vzr

    [ @ ] lisammbando Speaking English is not a joke Hahahahah 

    [ @ ] clararobinso Me cjaelewa hiyo lugha mpz, kwan ulitaka kuandika nn hapo?

    [ @ ] pinnadelicious Jmn mbona mnapenda kumcritisize hvo mwenzenu sa amekosea nn nyie mnaojua, duh dis is too much 

    [ @ ] teddybebe Jaman all in all si mmemuelewa.hata mbuyu ulianza kama mchicha kila kitu kinaitaji mazoezi na usione aibu hata wakikucheka mpenz jitahid tu utaelewa. @shilolekiuno 

    [ @ ] teddybebe Kumbukeni hata nyie mlitoka huko hata kama mlisoma za kishuaa. Vizur kumsahihisha na sio kumbeza  4h

[ @ ] m_bongo her message sent, delivered, read and understood hicks. By the way english isn't her first language.

    [ @ ] tutupahamidu Did or didnt?!!thank you or thanks to my director?!

    [ @ ] raqey_unique Yeah her English is not gud but a bet u all understood wat she meant so stop hating

      [ @ ] pinnadelicious Kiswahili every one anajua so mdada wawatu anajitahidi awe internationally so km tumeelewa wat she mean mbona hakuna tatizo, sema bongo tumemeza!!!!

    [ @ ] eshyleta bora washushuliwe tu, coz baadae wanaleta nyodo za kiswanglish, et kiswahili hawezi baadhi ya maneno, km huwezi kithungu tumia lugha yako ya taifa

    [ @ ] makavlive @shilolekiuno mwisho wa ujuaji ni aibu...ona sasa, ungeandika kiswahili isingekua shida, kutaka ung'eng'ee shule yenye hujaenda...acha kuiga paka la baa wee ongea kinyamwezi unachokijua!

    [ @ ] auma_bebe we al knw dat english iz not our mothertongue n tz nxma mnaijua histry yke shilole ss y mnamponda hvyo bdala hta ya kumrekebisha? sio fair bna...
 

Read More »

Mjue Mtangazi mwenye Ushawishi na Anayeskilizwa Sana Tz


Habari kutoka Bongo5.com

Jana tuliitisha kura za maoni Facebook na Twitter kutaka kufahamu kutoka kwa wasomaji wetu kuwa ni mtangazaji gani wa radio nchini mwenye ushawishi mkubwa na anayesikilizwa zaidi kuliko wengine.

Tanzania imeongea, na tunamtambulisha mtangazaji anayependwa zaidi, mwenye ushawishi kuliko wengine na ambaye kipindi chake husikilizwa zaidi, kuwa ni Millard Ayo aka ‘Mtu wa Nguvu’, wa Clouds FM.

Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.

Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM. Kipindi hicho pia ni miongoni mwa vipindi vinavyoiingizia fedha nyingi redio hiyo na kumfanya Millard kuwa miongoni mwa watangazaji wa kituo hicho wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi.

Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 67,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 145,530.

Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki na yenye matangazo mengi.

Kwa mshahara anaoupata, kazi ya uripota wa DSTV, ubalozi wa Fastjet, website yake, deal za voice-overs na mambo mengine, Millard anaingiza takriban ama zaidi ya shilingi milioni 10 kila mwezi.

Millard ni zaidi ya mtangazaji, bali ni mwandishi mwenye ‘pua ya habari’ (nose for news) huku akiongoza kwa kuja na angle za kipekee za habari zenye mvuto kwa watu (human interest stories) zinazokifanya kipindi chake cha Amplifaya kuteka matangazo ya jioni siku za wiki.

Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.

Hakuna shaka kuwa, Millard ana mustakabali wa nguvu kwenye fani hiyo. Ni mfano wa kuigwa kwa watangazaji wengine na hazina kubwa kwa wazazi wake, Clouds Media Group na hata taifa kwa ujumla.
-Bongo5


Read More »

Wastara Awaomba Watanzania wamuache aishi, na yeye ni Binadamu Pia


MSANII wa kike katika filamu za Kibongo, Wastara Juma amewashukia watu wanaotafsiri kila kitu anachokifanya katika maisha yake na kusema: “Yaani nisipige picha nikaweka kwenye mitandao ya kijamii, tayari watu wanasema yao...jamani nami pia ni binadamu.”

Wastara ambaye ni mjane wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ameliambia gazeti hili wikiendi iliyopita kuwa, baada ya kuachwa mpweke na mumewe Sajuki, watu wanafuatilia sana maisha yake kiasi kwamba anakosa uhuru.

Alisema, wengine hutafsiri vibaya hata wanaume anaokuwa nao karibu kikazi au marafiki, akafafanua: “Nashangaa kila nitakachofanya kinaanikwa na kuonekana ni kibaya wakati nami ni binadamu ninao uhuru wa kufurahi na kujiachia nitakavyo ili mradi sijavunja maadili.”


Read More »

Housegeli abakwa na kulawitiwa na bosi wake huko Arusha



VITENDO vya ukatili kwa watoto wenye umri mdogo vimeendelea kushamiri katika jamii, ambapo msichana wa kazi aliyetambulika kwa jina la Anna (13) mkazi wa ngaramtoni wilayani arumeru mkoaani arusha, ameharibika vibaya sehemu zake za siri kutokana na kitendo cha kunajisiwa na kulawitiwa na baba mwenye nyumba wake aliyejulikana kwa jina la Godifrey John(33).

Akizungumza na mwandishi wetu  baada ya kuokolewa na shirika la shaloom center for street children, linalojihusisha na utetezi wa haki za mtoto, mtoto huyo anaeleza kuwa, alianza kufanyiwa vitendo vya ukatili tangu April mwaka huu baada ya kutoka kijijini kwao masumbwe kilichopo wilayani kahama, mkoa wa shinyanga.

Alisema kitendo hicho kilikuwa kikimuumiza sana, lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga alilazimika kuzoea maumivu makali  aliyokuwa akiyapata kwani mwajiri wake alikuwa akishamaliza kumwingilia alikuwa akimtishia kumuua iwapo angethubutu kutoboa siri hiyo kwa mtu yeyote.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano, anaeleza kuwa, bosi wake huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa mazao, alikuwa akimnajisi na kumlawiti kwa kumziba mdomo ili asitoe sauti baada ya kumfungia mke wake chumbani majira ya usiku na mchana hasa kipindi ambacho mkewe alikuwa kwenye hali ya kujifungua.

Alisema bosi wake huyo alikuwa akimwacha mkewe kitandani na kumfuata sebuleni alikokuwa amelala na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile huku akiwa amemziba mdomo ili asitoe kelele wakati akifanyiwa ukatili huo.

''Alikuwa akiniingilia mara kwa mara, sikumbuki ni mara ngapi, na akianza kunifanyia mchezo mbaya alikuwa akiniziba mdomo na mkewe alikuwa akimfungia chumbani kwa komeo na kuna kipindi alikuwa mkali akinikaripia'' alisema.

Alisema kuwa, alifika mkoani arusha, mwezi februari mwaka huu, baada ya kuchukuliwa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la zawadi samuel ambaye ni rafiki yake na mtuhumiwa, ambaye alikuwa akihitaji msichana wa kazi kutokana na mkewe kuwa mjamzito.

"Huyo zawadi tulikutana nae kwenye basi nikitoka masumbwe kwenda kahama mjini, akaniambia kuwa anipeleke arusha akanitafutie kazi, nilikubali tukaondoka kesho yake, ila hadi sasa sina mawasiliano na wazazi wangu na sina ndugu yeyote hapa arusha,'' alisema anna.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi 8 alichofanya kazi kwa mtuhumiwa huyo, hakuwahi kulipwa mshahara ambao walikubaliana shilingi 20,000 kwa mwezi, ila aliwahi kumpa shilingi 10,000 na kumnunulia sketi mbili tu.

Alieleza kuwa mbali na kumfanyia unyama, alikuwa akimtesa kwa kumfanyisha kazi nyingi ikiwemo kumlazimisha kusomba maji umbali mrefu bila kupumzika, huku akishindwa kumsomesha kama alivyoahidi kufanya hivyo hapo awali.

 Kwa upande wa mwakilishi wa shirika la shaloom center, Enezael Joseph alisema kuwa wamefanikiwa kumwokoa mtoto huyo katika mazingira magumu baada ya kupata taarifa kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kinyume cha sheria.

Alisema kuwa shirika hilo lilipata taarifa kutoka kwa majirani wa mtuhumiwa ambao walichoshwa na vitendo vya manyanyaso anavyovipata mtoto huyo na kuamua kumfuata mtoto huyo na kuzungumza naye ndipo alieleza mambo mazito ya kulawitiwa na kunajisiwa naa mtuhumiwa kila kukicha.

 Joseph anasema kuwa baada ya taarifa hizo walitoa taarifa kituo cha polisi ngaramtoni na kupewa hati ya matibabu (PF3)  ambapo msichana huyo baada ya kupimwa katika hospitali ya seliani ya jijini arusha, aligundulika kuharibiwa vibaya sehemu zake zote za siri.

Alisema baada ya kupata majibu ya dakitari walirejea na kuwakabidhi polisi ambapo walifungua hati ya mashtaka ya kulawiti yenye kumbukumbu namba NGT/RB/1113/2013 ambapo mtuhumiwa alikamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaaendelea.

Hata hivyo mtuhumiwa wakati akitiwa mbaroni alisikika akidai kwamba anachofahamu kwa msichana huyo ni kwamba anamdai fedha zake za mshahara ila hayo madai mengine si kweli kwani amepandikizwa ili kumdhalilisha.





Read More »

Bibi kizee mchawi adondoka wakati akiwanga, aambulia Mkong'oto Mkali toka kwa Wananchi


Bibi mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika amesadikika kudondoka kichawi maeneo ya Tabata Kinyerezi Kisiwani baada ya wenzake aliodai  kuwa nao kumuacha.

Bibi huyo ambaye amechezea kipigo toka kwa raia  waliomtuhumu  kuwa  ni mchawi , amedondoka asubuhi ya leo  katika maeneo hayo huku akionekana kutokuwa na kumbukumbu nzuri


Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger