Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts

MCHEKI ETOO AKIWA NA MWANAE HAPA



Cheki picha zake alipokuwa mdogo uwanjani na akicheza kabumbu.


Samuel na David baada ya Fainali ya Copa De Rey
Baba na Mwana mnamo 2007

Read More »

RAGE ALIA NA WALIOMUUZA OKWI YANGA


MWENYEKITI aliyesimamishwa wa Simba, Ismail Rage, amefanya kikao na baadhi ya wanachama wa timu hiyo na kutoa siri kwamba waliomuuza mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa Yanga ni Waganda, SC Villa, lakini akasisitiza ni hujuma kutoka ndani ya klabu hiyo.
Emmanuel Okwi.
Championi Jumatano lilikuwa likipata ‘live’ kila kinachoendelea ndani ya kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya klabu ya Simba, barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam, jana.
Akionyesha mwenye masikitiko, Rage alisema kuna baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wanahusika katika usajili wa Okwi aliyetua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage.
Rage, amesema Okwi raia wa Uganda, mpaka sasa anakabiliwa na kesi tatu muhimu na kuzitaja ya kwanza ni ile ya nyota huyo kukakabiliwa na mashtaka ya kutoroka katika klabu yake ya zamani ya Etoile du Sahel ya Tunisia (ESS).
Shitaka la pili ni kuhusu SC Villa, ambao walipewa Okwi kwa mkopo lakini wakamuuza Yanga na tatu ni kesi yake aliyoifungua Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuhusu ESS, ambapo kabla ya shirikisho hilo kutoa majibu nyota huyo kukubali, Mganda huyo kauzwa Yanga.
“Nilipiga simu Fifa kutaka kujua kujua kuhusu Okwi, nikaambiwa kuna fedha dola 5,900 ambazo ni kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yetu, mwisho ilikuwa saa nne asubuhi leo (jana). Barua ilishatumwa tangu Desemba 6, lakini hakuna aliyeijibu na wakaificha,” alisema Rage akitaka kudondosha chozi ‘live’.
“Saa tatu asubuhi nikatuma fedha hizo ambazo zitatoa nafasi ya kusikilizwa kwa jambo hilo. Kama ningechelewa, basi Okwi angeweza kuwa mchezaji huru kwenda Yanga,” alisema Rage katika kikao hicho kilichofanyika kuanzia saa 10:15 hadi saa 11:45 jioni.
Aidha, Rage amesema anajua kuwa kamati ya utendaji ya timu hiyo inachangia kumhujumu ili aonekane hafai katika klabu hiyo, ambapo sasa ataitisha mkutano mkuu Januari mwakani.
“Simba imejaa wanafiki, wanafanya mpango wachezaji waende Yanga. Mfano, Okwi alishatangaza anaitaka Simba, vipi hawakumsajili na utaona mambo yanaharibika kila nikiwa nje ya nchi. Pia TFF kuna watu kama hao na wanachangia kutuhujumu na kuniharibia,” alisema.
Kuhusiana na suala la uchaguzi, Rage rasmi ametangaza kwamba hatagombea nafasi hiyo tena na badala yake kuna mtu amemuandaa.
“Tayari nimemuandaa mtu, siwezi kumtaja sasa ila nitawaacha wanachama waamue utakapofika uchaguzi,” alisema Rage.
Mzigo wa Okwi umekuwa ukimuangukia Rage kwa kuwa ndiye alifunga safari kwenda kumuuza Tunisia, lakini akarejea mikono mitupu na dola 300,000 za mauzo zikabaki Tunisia na hadi leo ni hadithi.

    Read More »

    BRUNO MARS NDIO MWANAMUZIKI BORA WA BILLBOARD 2013


    Huenda Miley Cyrus ameongoza zaidi kwa kuwa juu nabni ukweli usiopingika kwamba Justin Timberlake amerudi kwa kishindo kwenye muziki, ila habari sahihi ni kwamba Bruno Mars ndiye ambaye ametajwa kuwa msanii bora wa Billboard kwa mwaka 2013.
    "Ni maendeleo, ni heshima," Mars alisema kwenye mahojiano wiki hii. "Najisikia fahari kuwa sehemu ya timu hii yote niliyonayo."

    Nyimbo za mwaka huu za mwimbaji huyo zinahusisha pia wimbo namba moja When I Was Your Man na ngoma namba 5 akiwa na Treasure.

    Album yake kali, Unorthdox Juxebox, ilizinduliwa mwaka jana na imeuza zaidi ya nakala 1.8 million. Ikiwa ndiyo album ya pili bora kimauzo nyuma ya album ya Timberlake iitwayo The 20/20 Experience.

    Read More »

    CHRISTIAN BELLA KUSHIRIKI TAMASHA LA NGURUMO TCC CLUB JMOSI HII


    MWIMBAJI anayesadikika kuwa na sauti tamu zaidi kwa sasa, Christian Bella kutoka Malaika Music Band, amesema atashiriki tamasha la Gurumo litakalofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja wa TCC Club Chang’ombe.
    Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Christian Bella, ameomba awekwe kwenye ratiba ya waburudishaji ambapo atapanda kuimba japo wimbo mmoja kama ishara ya kuonyesha kuukubali mchango wa gwiji Muhidin Maalim Gurumo.
    Kama ilivyoelezwa hapo awali, tamasha la Gurumo, limeandaliwa mahsusi kwaajili ya kumuaga kwenye muziki wa jukwaani baada ya kutangaza rasmi kustaafu.
    Mbizo ameongeza kuwa Christian Bella amesema miongoni mwa kazi anazozikubali sana hapa nyumbani, ni kazi za Msondo Ngoma chini ya Gurumo.

    Read More »

    MANDELA AWAPONZA DROGBA NA NA EBOUE, WATOZWA FAINI NA CHAMA CHA MPIRA CHA UTURUKI



    Didier Drogba na Emmanuel Eboue watatozwa faini na chama cha mpira cha Uturuki baada ya kuonyesha vesti ambazo zilionyesha ujumbe wa kuguswa kwao na kifo cha Nelson Mandela.

    Add caption
    Wachezaji hao wawili wa kimataifa toka Ivory Coast waliziweka wazi hisia zao kwa ujumbe huo mara baada ya mechi ya Galatasaray dhidi ya Elazigspor mnamo siku ya Ijumaa, kwenye mechi ya kwanza toka kifo cha kiongozi huyo wa Afrika Kusini kilipotokea.

    Add caption

    Nguli huyo wa Chelsea, Drogba alivua jezi yake kwenye mechi iliyoisha kwa kushinda 2-0 na kisha kuonyesha kuguswa kwake na kifo hicho, ambapo maandishi kwenye vesti yake yalisoma: ‘Thank you Madiba’ huku yale ya nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue yalisema: ‘Rest in Peace Nelson Mandela’.





    Read More »

    BAADA YA MBURUNDI KUSHINDA TUSKER PROJECT FAME SHANGWE ZA KWAO ZIMEKUWA HIVI


    Pengine hii itakuwa ni mara ya kwanza na historia kwa nchi hiyo kutoa mshindi katika mashindano makubwa kama haya, huko pande za kwao kumekuwa na furaha na shangwe zisizo na kifani kutoka kwa raia wa nchi hiyo.

    Mshiriki Hope toka Burundi amejikuta akianguka chini kwa mshituko wa furaha ulimkuta baada ya kuibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi wa Tusker Project Fame na kujinyakulia kitita cha Shilingi 5,000,000/= za Kenya .

    Mashindano hayo yaliyomalizika hivi punde usiku wa jana yamemwacha Hope katika taharuki huku akiwabwaga wenziye; Hisia (Tanzania), Patrick (Rwanda),Wambura (Kenya), Daisy (Uganda),Amos & Josh wa Kenya


    Read More »

    HATARIIII!!" AJIFUNGA KAMBA KATIKA "DUSHELELE" KISHA KUTEMBEA JUU YA KAMBA MLIMANI





    Watu hawa wa ajabu walikutwa kwenye tamasha la highline wakiwa wanatembea juu ya kamba kwa umbali wa mita 61 huku wakiwa uc+hi wa mnyama - cha ajabu zaidi ni jamaa huyu aitwaye Andy Lewis ambaye tofauti na wenzake yeye aliamua kwenda mbali zaidi.

    Wakitembea juu ya kamba hizo ambazo zilipita juu toka kwenye ardhi iliyokuwa chini kwa urefu wa mita 30, hakika jamaa waliyaweka maisha yao kwenye hatari kama sio kifo huku wakiwa wako uc+hi wa mnyama.

    Majasiri hao waliacha nguo zao pembeni na kuvaa kamba moja ambayo waliifunga kwenye mguu na kiuno, ila kwa ishu ya Andy Lewis yeye ilikuwa ni ya kipekee zaidi kwani yeye aliifunga kamba hiyo kwenye "dudu" wake.

    Angalia picha hapo chini...




    DC Blog.

    Read More »

    ZAHA AKANUSHA KUWA NA MAHUSIANO NA MTOTO WA KOCHA WAKE, ASISITIZA HIYO SI SABABU YA KUKOSA NAMBA MAN U.





    Wilfried Zaha amechukua hatua ya aina yake kukanusha taarifa zilizozagaa kwamba ana uhusiano wa kmap3nzi na mtoto wa kike wa kocha mkuu wa Manchester United David Moyes.
    Winga huyo mwenye miaka 21 alinunuliwa na Sir Alex Ferguson kwa £15milllion lakini ameshindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza chini ya David Moyes.
    Kumekuwepo na taarifa kwamba amekuwa hapewi nafasi ya kucheza na Moyes kwasababu ya mahusiano yake na binti wa kocha huyo aitwaye Lauren.
    Lakini Zaha - ameonekana kukerwa sana na tetesi hizo - ametumia ukurasa wake wa Twittet kuwaambia mashabiki 490,000 kwamba taarifa hizo sio za kweli.
    Zaha: The 21-year-old has found himself playing for the Under 21s this year instead of with the first team
    'Sijawahi kuwa na mahusiano ya kmap3nzi wala kukutana na binti wa David Moyes, hivyo jambo hilo haliwezi kuwa sababu ya kukosa kwangu nafasi katika kikosi cha kwanza ...,' aliandika Zaha.
    'Ningependa hizi taarifa za uongo ziachwe kusambazwa….Nitaichezea Manchester United pindi kocha atakapoana nipo tayari kufanya hivyo...'

    Zaha aliichezea United katika mchezo wa kombe la hisani lakini tangu wakati huo ameichezea mechi moja tu ya mashindano dhidi ya Norwich City katika League Cup.


    Read More »

    PICHA YA KIPEKEE YA MZEE MANDELA NA MOHAMMED ALLY



    Dunia ikiwa katika maombolezo ya shujaa huyu wa Africa, tunakumbuka na kuyaenzi mengi mazuri ya kwake, pichani hapo juu Mzee Mandela akiwa na Mohamed Ally akimpa "JEB" Kuashiria kuuenzi mchezo wa ujanani mwake ambapo mzee Nelson Mandela alikuwa ni Bondia.

    Nelson Mandela, Madiba the great, ni mtu wa kipekee na mcheshi sana, na amekuwa hivi mpaka pumzi yake ya mwisho...! #RIPNelsonMandela

    Read More »

    CHAPA NYINGINE" YA KWAKE CHEGGE HII HAPA


    Hii ni ngoma mpya ya Chegge toka TMK, amemshirikisha mwanadada aitwaye Gift na Production ni ya Dunga.

    Isikilize na Ishushe hapa....
     

    Read More »

    FIFA Yazindua Aina Mpira Utakaotumika Kwenye Kombe la Dunia 2014 Uitwao ‘Brazuca’


    Mpira rasmi utakaotumika kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia nchini Brazil hapo mwakani umetangazwa rasmi.

    Mpira huo utaitwa ‘Brazuca’ baada ya kufanyika kwa droo la mashabiki nchini Brazil ambalo lilihusisha kura karibu na milioni.

    Read More »

    CECAFA Challenge:MBWANA SAMATA NA THOMAS ULIMWENGU WAIPELEKA STARZ ROBO FAINALI


    TIMU ya Taifa ya Tanzania bara, The Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA baada ya kuitafuna Burundi bao 1-0 alasiri ya leo.

    Shukurani kubwa zimwendee nyota wa Tanzania anayekipiga klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 7 akiunganisha kwa ufundi mkubwa krosi iliyochongwa na Mtanzania mwenzake anayekipiga klabu ya Tp Mazembe, Thomas Ulimwengu.

    Stars imecheza soka zuri na kupata nafasi nyingi za kufunga, lakini umahiri wa kipa wa Burundi, Arakaze Arthur amewaokoa Warundi kwani aliokoa bunduki nyingi langoni mwake.
    Kwa Matokeo ya mchezo wa leo, Kili Stars imemaliza mechi za makundi ikijikusanyia pointi 7 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia, kisha kuifunga Somalia 1-0 mechi za awali, na leo hii kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burundi.

    Nani atakuwa kinara wa kundi B, matokeo ya mchezo unaoendelea sasa baina ya Zambia na Somalia utaamua ambapo mpaka sasa ni mapumziko na Zambia wako mbele kwa mabao 2-0.
    Kama Zambia itaibuka na ushindi mkubwa leo hii basi itaongoza kundi B, na tafsiri yake ni kuwa Kilimanjaro Stars itakumbana na Uganda katika mchezo wa robo fainali.

    Iwapo Kili stars itakutana na Uganda, itakuwa na hamu ya kulipa kisasi kwani walilala 3-0 katika mchezo wa nusu fainali wa michuano iliyopita mjini Kampala, Khamis Kiiza na Emmanuel Okwi wakiwemo ndani kwani mwaka huu pia wamejumuishwa kwenye kikosi cha Uganda The Cranes.
    kama Stars itaongoza Kundi B, itakutana na Timu ya Taifa ya Rwanda, `Amavubi` .
    Tanzania Bara;

    Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Amri Kiemba/Haroun Chanongo dk77, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk81.

    Burundi;
    Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan/Abdulrazack Fiston dk81, Hererimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsabiyumva Frederic, Nduwimana Jean, Ndikumana Yussuf, Duhayinavyi Gael/Mussa Mosi, Nduwarugira Christophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaaban/Ndarusanze Claude.

    Read More »

    Iskilize Hapa Single Mpya ya Abdu na Ally Kiba



    Huu ni wimbo mpya wa Abdul Kiba aliomshirikisha Ally Kiba unakwenda kwa jina la Kajiinamia...

    Usikilize hapa chini..


    Read More »

    Ryan Gigs atimiza Miaka 40 leo, bado yupo yupo kwanza na Man U.


    Kiungo wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs hana mpango wa kustaafu japokuwa leo Ijumaa akiwa anatimiza miaka 40.

    Mchezaji huyo toka Wales ametumia muda wake wote wa mpira akiwa anachezea timu hiyo toka Old Trafford, akiicheza klabu hiyo jumla ya mechi 953 tok alipoanza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Everton mnamo mwaka 1991.

    "Nina bahati kwamba nimekuwa kwenye klabu moja. ambapo nimezungukwa na wachzaji wazuri na meneja mzuri," alisema.

    "Inaweza kuwa ngumu wakati mwengine ila bado nafurahia, vyovyote itakavyokuwa nitaendelea."

    Akaongeza: "Nahitaji kufanya vyema kwenye kila mchezo, nataka kushinda mataji na lengo langu nikuwa kwenye hilo."


    Read More »

    Kiwanja cha Kombe la Dunia 2014 Brazil chaua watatu


    Sao Paulo, Brazil - Vifo vya watu watatu vimeripotiwa kutokana na kuanguka kwa sehemu ya kiwanja kitakachotumika kwa ajili ya ufunguzi wa michuano hiyo mnamo siku ya Jumatano, November 27, huku ikielezwa kwamba ajali hiyo pia imesababisha uharibifu mkubwa.

    Hii inamaanisha kwamba kutakuwa na ucheleweshwaji wa makabidhiano ya viwanja vyote 12 kwa FIFA itakapofika mwezi Desemba kama ambavyo imepangwa, hii ni kutokana na Uwanja huo wa Itaquerao kuanguka, mpaka inaanguka sehemu ya uwanja huo ulikuwa tayari umekamilika kwa asilimia 94.



      

    Read More »

    Angalia hapa Mambo yalivyokuwa katika Tuzo za "American Music Awards"


    Tuzo za American Music 2013 zilifanyika jana Nov. 24, kwenye ukumbi wa Nokia Theatre uliopo ndani ya Los Angeles. Picha juu na chini zinamuonyesha Rihanna (ambaye alishinda tuzo ya icon) pia wapo Lady Gaga na Jennifer Lopez. 

    Rihanna
    J Lo
    Lady Gaga
    Angalia picha zaidi picha kwenye red carpet wakihusishwa wasanii na nyota kibao walioshinda tuzo tofauti...
    Miley Cyrus

    Jeniffer Hudson
    Christina Aguilera

    Jordan Sparks
    Lil Mama
    Chilli & T-Boz wa TLC

    Ciara
    2 Chainz
    Lady Gaga

    R. Kelly

    Read More »

    Angalia picha zaidi ya 20 za matukio katika Show ya P square Dar

     
     
    Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square wakilivamia jukwaa la Leaders

    WEUSI WAKIFANYA YAO STEJINI

    Joh Makini akilitawala jukwaa.
    Nikki wa Pili (kushoto) na G Nako wakifanya yao…

    PROFESA JAY AWADATISHA MASHABIKI NDANI YA LEADERS CLUB

    LADY JAYDEE AKIFANYA YAKE STEJINI

    Mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee' au 'Anaconda' akiwapagawisha mashabiki wake waliohudhuria katika Viwanja vya Leaders Club usiku wa janakatika shoo wa wakali P-Square.…

    MA MC KAZINI...

    MC Dullah akiwa kazini.
    Ma MC wakiwajibikia stejini.

    BEN POL AKILISHAMBULIA JUKWAA KATIKA YA SHOO YA P-SQUARE

      Mwanamuziki Ben Pol akiwasha moto katika steji ndani ya Viwanja vya Leaders usiku huu katika shoo ya P-Square Live in Dar.…

    Steji.…


    Read More »

    Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
    Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
    Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
    Designed by: Creative Blogger