Showing posts with label Mpira. Show all posts

Yanga Yampa Matumaini Barthez



Licha ya kufanikisha usajili wa kipa mkongwe, Juma Kaseja, uongozi wa Yanga umesema hauna mpango wa kumtoa kwa mkopo kipa wake aliyetetereka, Ali Mustafa ‘Barthez’.
Wiki iliyopita Yanga ilitangaza kumsajili Kaseja kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 40 milioni na kuifanya timu hiyo iwe na jumla ya makipa watatu, kwani tayari ilikuwa na Barthez na Deogratius Munishi ‘Dida’.
Hata hivyo, usajili wa Kaseja ndani ya kikosi cha Yanga ulitafsiriwa na baadhi ya mashabiki wa soka kuwa ndiyo mwanzo wa kuondolewa kwa Barthez ambaye alipoteza nafasi ya kuwa kipa namba moja tangu alipotunguliwa mabao matatu katika pambano la Ligi Kuu dhidi ya Simba lililomalizika kwa sare ya mabao 3-3.
 Hata hivyo, jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdalah Bin Kleb alisema, Barthez ataendelea kuwamo kwenye kikosi cha timu yake sambamba na Kaseja na Dida.
“Mwalimu wetu (Ernest Brandts) aliacha mapendekezo ya wachezaji anaowataka wasajiliwe na usajili wa Kaseja ni sehemu ya kutekeleza mapendekezo hayo.
“Tunataka tuwe na makipa watatu wa uhakika ndiyo maana tumemwongeza Kaseja, lakini hatuna mpango wa kumtoa kwa mkopo kipa yeyote si Barthez wala Dida,” alisema Binkleb na kuongeza:
“Makipa watatu si wengi na hata kama mwalimu atasema anataka mwingine tena sisi tutatekeleza. Kama unavyojua michuano ya Ligi ya Mabingwa si lelemama unatakiwa ujiimarishe sawasawa.”
Katika hatua nyingine makipa Dida na Barthez wamesema wanamkaribisha kwa mikono miwili Kaseja na kuahidi kushirikiana naye kwa roho safi.
Wakizungumza kwa wakati tofauti, Dida na Barthez wameliambia gazeti hili kuwa kwa upande wao hawana kinyongo na Kaseja isipokuwa wamefurahishwa na ujio wake Yanga.
“Hilo ni jambo la furaha kwetu kwa kukutana tena pamoja na hivyo ndivyo maisha ya soka yanavyokuwa. Hakika hatuna budi kwa pamoja kushukuru Mungu kwa kutukutanisha tena.
“Kazi yangu ni kujituma uwanjani kila ninapopata nafasi naamini na wenzangu pia watakuwa wakifanya hivyo,” alisema Dida ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Azam.
Hata hivyo kwa upande wake Barthez alisema kuwa, ”Mimi na Kaseja ni marafiki na siyo maadui kama watu wanavyozusha na hilo litajulikana pindi tutakaporudi kutoka mapumziko.
“Nimeishi naye Simba kwa amani bila ya tatizo lolote akiwa kama nahodha wangu, kama tulipishana ni hali ya kawaida kwa binadamu. Namkaribisha Yanga na nitafanya naye kazi kwa roho safi bila ya tatizo lolote kama ilivyokuwa hapo awali.
“Kuhusu nafasi ya kucheza, kocha ndiye mwenye uamuzi nani acheze na nani asicheze, lakini nitaendelea kujituma mazoezini kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Barthez.

Read More »

Simba Wakwaa Kisiki, Mashabiki wafanya fujo kubwa.




MBIO za Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara zinazidi kuwa ngumu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar jana, lakini habari mbaya zaidi ni kuwa mashabiki wa timu hiyo walijeruhiwa kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mechi hiyo.
Vurugu hizo zilitokea katika mechi hiyo ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya Kagera kusawazisha bao katika dakika ya 95 kutokana na mkwaju wa penalti uliopigwa na Salum Kanoni, mara baada ya beki wa Simba, Joseph Owino kumchezea vibaya Daudi Jumanne.

Mara baada ya bao hilo la kusawazisha, mashabiki wa Simba walianza kuvunja viti, kitendo kilichosababisha askari wa kutuliza ghasia kurusha mabomu mawili ya machozi kwenye jukwaa la mashabiki hao, ndipo mtifuano ukawa mkubwa.
Tukio hilo lilitokea sekunde chache kabla ya mwamuzi wa kati, Mohamed Theofile wa Morogoro kumaliza mchezo huo, ambapo askari waliendelea kurusha mabomu kadhaa.

Gazeti hili lilishuhudia viti zaidi ya 50 vikiwa vimevunjwa na kuzagaa, huku baadhi ya mashabiki wakiumia na wawili kupoteza fahamu, huku wachezaji wakitoka mbio kuelekea vyumbani mara baada ya kipenga cha mwisho.
Mmoja wa mashabiki aliyepoteza fahamu ni wa Simba aliyetambulika kwa jina la Fii Kambi, ambaye hali yake ilikuwa mbaya lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa Msalaba Mwekundu, alirejewa na fahamu, lakini mpaka gazeti hili linaondoka uwanjani hapo, alikuwa bado hajarejea katika hali yake ya kawaida.

Akizungumzia juu ya kilichotokea uwanjani hapo, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, alisema:

“Tumeingiwa na hofu na yawezekana tunatengenezewa mazingira magumu ya kutwaa ubingwa kutokana na kuonewa.”
Upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope, alisema: “Asilimia kubwa ni matatizo ya waamuzi wetu wa Tanzania, aliongeza muda mwingi wakati dakika zilikuwa zimemalizika.”

Naye nahodha wa Simba, Said Nassoro ‘Chollo’ naye alisema: “Kitendo cha mabomu kulipuliwa wakati tukiwa uwanjani mechi ikiendelea ni jambo baya na wanatakiwa kulichukulia hatua kali.”

Katika mechi hiyo Simba ndiyo ilianza kupata bao katika dakika ya 45 kupitia kwa Amissi Tambwe ambaye ameendelea kuwa kinara wa mabao kwa kufikisha mabao tisa na kumzidi Hamis Kiiza wa Yanga mwenye mabao nane.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni, akisema: “Naishauri TFF mpya iangalie juu ya suala la waamuzi kwa kuwa wao ndiyo tatizo.”

Upande wa Kocha wa Kagera, Jackson Mayanja, alisema: “Mwamuzi alifanya kazi inavyotakiwa kwa kuwa aliona mchezaji alifanyiwa faulo, ndiyo maana akatoa penalti halali.”

Kituko katika mchezo huo, ni mashabiki wa Simba kushangilia uamuzi wa Abel Dhaira kuwekwa benchi katika mechi, badala yake langoni akasimama Abuu Hashim ambaye alidaka dakika zote 90.

gpl


Read More »

Jamal Malinzi ashinda urais wa TFF


Habari tulizozipata  ni kwamba Jamal  emil Malinzi amefanikiwa kushinda uchaguzi wa TFF kwa nafasi ya urais aliyokuwa anagombea dhidi ya Makamu wa zamani wa Rais wa TFF Athumani Nyamlani.

Uchaguzi huo, uliotawaliwa na kashkashi za hapa na pale, ulifanyika katika ukumbi wa NSSF WATER FRONT, Dar es salaam
 
Jamal Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Kagera ameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada ya kushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka 2008.




Read More »

David Beckham Aingia Katika Filamu Baada ya Kustaafu Mpira



Aliyekuwa Mchezaji wa PSV Kabla ya Kustaafu, David Beckham ameonesha nia ya kuingia katika Uigizaji wa Filamu. Ingawa Mwenyewe hajatoa maamuzi ya mwisho rasmi,Becks anatarajiwa kuleta msisimuko na hasa pale atakapokuwa akiigiza Tamthiliya za Kipelezi na Kijasusi kama za James Bond.

New career path: David, who proved his one screen presence in the short film, could be set to star in his first proper acting role
Miongoni mwa spicha katika filamu ambayo Becks amewahi kuigiza kwa kipande kifupi mno.

Kuna Testesi za nyota huyo kuigiza kama Starring katika Filamu inayokwenda kwa jina la "Kick-Ass" ambapo mkali Samuel L. Jackson anatarajia kumpa Kampani akiigiza kama Adui Mkuu.
Moving on: David played his last game for PSG back in May as he retired form the sport
Mechi ya Mwisho ya Beckham Kucheza kabala ya Kustaafu May 2013.


Read More »

Yanga yawakaba koo URA

Dar es Salaam. Mabingwa wa Tanzania, Yanga wamelazimisha sare 2-2 na URA ya Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga walisubiri hadi dakika ya 90, wakati mshambuliaji Jerryson Tegete alipofunga bao la kusawazisha baada ya mabeki wa URA kushindwa kuelewana na kipa wao.
Mshambuliaji wa URA , Lutimba Yayo aliifungia timu yake mabao mawili ya kuongoza katika dakika 42 na 51, kabla ya Didier Kavumbagu kuipatia Yanga bao katika dakika ya 66 na Tegete kuisawazishia Yanga.
URA walitawala vizuri kipindi cha kwanza ikiwa ni saa 24, tangu walipoichapa Simba kwa mabao 2-1 kwenye uwanja huo. Katika dakika ya 4, Derrick Walulya nusura aifungie timu yake bao baada ya shuti lake kupaa juu kidogo ya goli la Yanga.
Kipa mpya wa Yanga, Deogratias Munish ‘Dida’ alithibitisha ubora wake baada ya kuokoa shuti la Ngama Emmanuel akiwa ndani ya eneo la 18 katika dakika ya 27.
Yanga walimtoa Hamis Thabit na kumwingiza Bakari Masoud katika dakika 40, wakati URA waliwapumzisha, Joseph Owino, Ngama Emmanuel na kuwaingiza Munaaba Allan na Ike Obina.
Dakika tatu kabla ya mapumziko URA walipata bao la kuongoza lililofungwa na Yayo kwa shuti kali baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Yanga.
Waganda walirudi kipindi cha pili kwa nguvu zaidi na kufanikiwa kupata bao la pili lilililofungwa na Yayo kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya beki wa Yanga, Ibrahimu Job kumchezea vibaya Ngama Emmanuel katika dakika 51.
Mshambuliaji Kavumbagu alifungia Yanga bao la kwanza katika dakika 66, akiuganisha kwa kichwa krosi ya Juma Abdallah. Kocha wa Yanga, Ernest Brandts alimtoa Bahanuzi na kumwingiza Haruna Niyonzima katika dakika 77, ambapo mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa  Yanga kwani iliwasaidia kurudi mchezoni.
CHANZO: MWANANCHI

Read More »

Loh!! Macho hayana pazia, Mwangalie Mikel Obi akimkododolea mdada mwenye Bikini huku akiwa anarekodiwa.


Angali Picha Ikimwonesha Mchezaji wa kulipwa Mwenye Asili ya Nigeria, ambaye pia ni Midfielder Mikel Obi akimtupia jicho mrembo wa Ki Brasil aliyekuw anakatiza mbele yake kiasi cha kumfanya ajisahau kama yupo katika Interview na Camera inamuangalia yeye.

Unaionaje hii?

Read More »

Ronaldo amsaliti Mpenzi wake sababu ya Miss Bum Bum 2013













No wonder Cristiano Ronaldo didn’t play well during Real Madrid vs Borussia Dortmund match on Wednesday April 24th (Real lost 4-1 to Dortmund)…he had sex two days before…lol.
Andressa Urach (pictured above right) is claiming the star footballer, who is in a serious relationship with Russian super model, Irina Shayk, slept with her in a £12,500-a-night Villa Magna hotel on Monday April 22nd. Andressa is 2013 Miss Bum Bum Brazil queen. She told The Sun UK that Cristiano got in touch with her after seeing her photos online, and had sex with her just a day after Ronaldo was pictured leaving a restaurant with Irina (pictured left).
Andressa said she took a taxi to the hotel that Monday and waited for Ronaldo at the Lobby. Ronaldo eventually arrived in a grey Audi R3 and parked in an underground car park before taking a private lift to his room, from where he texted her his room number. The beauty queen said the sex was great.

“It was incredible, his body’s perfect, like a Greek god. He went on for hours and would not stop talking about my butt.’
Cristiano’s girlfriend, Irina, is known as one of the world’s top swimwear and lingerie models. Meaning her body is bad! Still he cheated on her. How much more us mere mortals! Lol. Men! Choi!!


Read More »

Mchezaji wa Ligi Kuu ampiga Refa Ngumi na Kumtoa damu Puani

-->


Indonesian footballer Pieter Rumaropen, who punched a referee in the face, has been banned for life by the country’s football authority.
The striker for Papua province club Persiwa Wamena, punched referee Muhaimin after he awarded a penalty to Pelita Bandung Raya during a Super League match on Sunday in West Java’s capital Bandung.
Muhaimin was taken to hospital where he received four stitches.
The match was held up for 15 minutes before a replacement official took over and gave Rumaropen a red card.
Hinca Panjaitan, a member of the disciplinary commission of Indonesia’s Football Association, PSSI, said Rumaropen’s behavior damaged the image of the country’s football.
In 2008, PSSI imposed life bans on four players for beating up a referee and his assistants.
Rumaropen’s Persiwa Wamena were tied 1-1 with Pelita Bandung Raya on Sunday when referee Muhaimin awarded a penalty to Pelita with eight minutes left on the clock.
Video replays of the incident showed Rumaropen running up behind Muhaimin and landing a swinging left hook on the referee, who had to be admitted to a hospital due to excessive bleeding from his nose.
Persiwa, currently seventh in the 18-team league, lost 2-1 after their opponents converted the penalty.
Persiwa defender Richardo Roberto was also sent off in the first half of the match


Angalia Video


Read More »

Beckham atolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu mbaya

Huko katika Legue 1 nchini Ufaransa na kuisababishia timu yake kumaliza mchezo ikiwa na wachezaji 8 wa ndani baada ya kutolewa yeye na mwenzie .Beckham ambaye aliingia uwanjani kipindi cha pili alimchezea vibaya

-->

Youssef Adnane  na kumfanya refa kumpa kadi nyekundu moja kwa moja. Angalia video chini

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger