Showing posts with label Ujana. Show all posts

Sintah Ampiga Dongo Penny, Amwambia Asing'ang'anie Asipotakiwa


"This goes out to my ladies ambao ni glues heee kama superglue yaani wanajifanya wenyewe tutabanana hapa hapa, jamani kama mwanamme hakupendi muache maana kuna other potentials out there  unakazana na asie wako ili iweje??

jamani penny hausiki ktk hili maana anaishi na dimondo so naombeni kwa heshima mumuache apumzike tuendelee na yetu" Sintah

Read More »

Mjue Mtangazi mwenye Ushawishi na Anayeskilizwa Sana Tz


Habari kutoka Bongo5.com

Jana tuliitisha kura za maoni Facebook na Twitter kutaka kufahamu kutoka kwa wasomaji wetu kuwa ni mtangazaji gani wa radio nchini mwenye ushawishi mkubwa na anayesikilizwa zaidi kuliko wengine.

Tanzania imeongea, na tunamtambulisha mtangazaji anayependwa zaidi, mwenye ushawishi kuliko wengine na ambaye kipindi chake husikilizwa zaidi, kuwa ni Millard Ayo aka ‘Mtu wa Nguvu’, wa Clouds FM.

Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.

Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM. Kipindi hicho pia ni miongoni mwa vipindi vinavyoiingizia fedha nyingi redio hiyo na kumfanya Millard kuwa miongoni mwa watangazaji wa kituo hicho wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi.

Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 67,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 145,530.

Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki na yenye matangazo mengi.

Kwa mshahara anaoupata, kazi ya uripota wa DSTV, ubalozi wa Fastjet, website yake, deal za voice-overs na mambo mengine, Millard anaingiza takriban ama zaidi ya shilingi milioni 10 kila mwezi.

Millard ni zaidi ya mtangazaji, bali ni mwandishi mwenye ‘pua ya habari’ (nose for news) huku akiongoza kwa kuja na angle za kipekee za habari zenye mvuto kwa watu (human interest stories) zinazokifanya kipindi chake cha Amplifaya kuteka matangazo ya jioni siku za wiki.

Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.

Hakuna shaka kuwa, Millard ana mustakabali wa nguvu kwenye fani hiyo. Ni mfano wa kuigwa kwa watangazaji wengine na hazina kubwa kwa wazazi wake, Clouds Media Group na hata taifa kwa ujumla.
-Bongo5


Read More »

Huyu ndiye Producer wa " Number One" ya Diamond


Ukiingia ndani ya studio ya Burn Records iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam, huwezi kuamini kama ndiyo sehemu ‘zinakopikwa’ kazi za baadhi ya wasanii zinazowafanya kuwa maarufu na kuwaingizia kipato, kupitia shoo na mialiko ya ndani na nje ya nchi.
Studio hii iliyopo maeneo ya ‘uswahili’ imezingirwa na nyumba nyingi kiasi cha kushindwa kuijua njia kwa uharaka zaidi pale mtu anapotaka kufika kwa prodyuza huyo. Studio hii ni ndogo yenye vifaa vichache tu vya kimuziki lakini yenye prodyuza makini na mwenye kipaji.
Shadrack Willced Mongi maarufu ‘Sheddy Clever’ ndiye prodyuza wa studio hii iliyotengeneza wimbo wa ‘My Number One’ unaomilikiwa na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’, wimbo uliofanya vizuri katika levo za kimataifa.
Hata hivyo sehemu ya mahojiano na mwandishi wa Starehe ni kama ifuatavyo;
Swali: Mbona Studio yako ipo uchochoroni hivi?
Jibu: Unasema uchochoroni!  Wasanii wengi wamekuja hapa na wanatumia muda mwingi kuwepo ndani ya studio hii huku wakitumia vyakula vya hukuhuku kwetu uswahili, si jambo la ajabu. Lakini ni mazoea tu kwetu tunaona sawa na kwa upande wangu inanipa hamasa kwani najisikia huru kufanya kazi nikiwa maeneo haya.
Swali: Ndiyo kusema Diamond alikuja kurekodi kwenye studio hii?
Jibu: Ndiyo alikuja kurekodi katika studio hii na alikuwa akikaa hapa kutwa nzima. Yule jamaa anafanya kazi sijawahi ona kutoka kwa wasanii wengine akija hapa anatumia muda mwingi kujenga mashairi, hata hivyo anatumia akili kubwa sana katika kufanya kazi si sawa na vile watu wanamwona. Korasi ya wimbo wa My Number One tulitumia zaidi ya saa 12 kuitengeneza na saa nyingine 12 kuirekebisha, yupo makini sana. Ilichukua miezi sita kukamilika.
Swali: Ilikuwaje akapajua hapa?
Jibu: Diamond alinitafuta yeye mwenyewe, ilikuwa saa mbili asubuhi akanipigia na kunifahamisha jina lake akasema anakuja, kwa kuwa namba niliyokuwa nayo alishaacha kuitumia nilidhani si yeye lakini baada ya muda nikashangaa amefika. Alinitaka nimsikilizishe midundo nami nilifanya hivyo hatimaye akapenda mmoja wapo, basi tulipeana mikakati kazi ikafanyika.
Swali: Kazi uliyoifanya imeweza kumwingizia kitita kikubwa cha pesa mwanamuziki huyo vipi kwa upande wako inakuneemesha vipi?
Jibu: Hapana nilimfanyia kazi akanilipa ujira wangu mzuri tu, hivyo huko mbele ni kazi yake. Lakini katika upande wa hatimiliki hivi sasa tupo mbioni kuhakikisha chama chetu cha maprodyuza  cha Tanzania TSPA kinasajiliwa ili kuweza kutetea kazi zetu na hatimiliki.
Inaendelea katika Mwananchi

Read More »

Auawa kwa wizi wa Kuku watatu, mmoja wa kuku ataga pembeni mwa mwili wa marehemu.


Ndugu wa marehemu Frank Shoka aliyetuhumiwa kwa wizi wa kuku mwili wake ukisubiriwa kuja kuchukuliwa napolisi
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula aliyesimama kushoto amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Polisi wakiuchukuwa mwili wa marehemu Frank









WAKATI jeshi la polisi Mkoani Mbeya likijitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, bado hali imezidi kushamiri baada  watu wawili kuuawa kwa tuhuma za wizi wa mifugo.

Matukio hayo ywmetokea katika Wilaya za Kyela na Mbeya vijiji yakiwemo ya wizi wa kuku na ng’ombe jambo lililopelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

Katika Tukio la kwanza lililotokea katika kitongoji cha Katusi kijiji cha Mjere wilaya ya Mbeya vijijini wananchi wamemuua Frank William Shoka(30) kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid(41)mkazi wa kijiji hicho.

Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao  alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20,mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manane na kuchukua kuku watatu wakati yeye akiwa amekwenda kumuuguza mwanae katika kituo cha Afya Mjere ambako aliandikiwa sindano za masaa.

Alisema Baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa na kuku hao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya,alipoulizwa juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.

Alisema mtuhumiwa huyo  baada ya kushindwa kutolea maelezo juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga kwa kutumia fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyomfanya kupoteza maisha papo hapo mita chache kabla ya kufikishwa katika ofisi ya kijiji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.

Aidha Baada  mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi na Daktari mwili ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa taratibu za maziko,hata hivyo wakati wa tukio hilo mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Mary Julius[30]alikuwa hayupo nyumbani akidai kuwa walikuwa wametengana.

Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.

Katika tukio la pili lililotokea kijiji cha Lupembe kata ya Katumba Songwe tarafa ya Unyakyusa wilaya ya Kyela Godfrey Mwakapalila mkazi wa kijiji cha Mpunguti aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.

Chanzo cha mauaji hayo ni wizi wa ng’ombe mali ya Moto Mwakiange(36) mkulima na mkazi wa kijiji cha Muungano tukio lililotokea majira ya saa mbili asubuhi octoba,19 mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la polisi linamshikilia Moto Mwakiange kwa mahojiano zaidi wakati upelelezi ukiendelea  wa kuwabaini watu waliohusika na mauaji,aidha mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkoani na atahakikisha wale wote waliohusika na mauaji wanakamatwa ili kujibu tuhuma za mauaji.

Picha na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu

Read More »

"Cheka Unenepe" Unaionaje Shule Hii?


Cheka kidogo upunguze stress, imagine mwanao au wewe mwenyewe ndo ingekuwa shule yako au
unatakiwa ukaifundishe kama ticha? Majina ya Hizi shule nyingine kaazi kweli kweli!!!




Read More »

Ambaka Rafiki Yake Kisha kumpiga Picha za Uchi na Kuziweka katika Mitandao ya Kijamii.


Awali ya yote Tunampa pole Thelma Lawrance, Msichana wa miaka 23, mwanafunzi kutoka Chuo cha Masuala ya Kiteknolojia kwa mkasa uliompata baada ya Kubakwa na Rafiki wake wa kawaida alipokwenda kuchukua " Memory Card" yake.

Thelma, Alifanyiwa unyama huo na Henry Aiyenero, 27, ambaye siku zote alikuwa akimchukulia kama rafiki yake wa kawaida ingawa kwa mara kadhaa alikuwa akimtongoza na kumshawishi kuhusu kufanya mapenzi lakini akawa anakataliwa.

Siku ya Tukio Thelma alikwenda kuchukua Memory card hiyo kwa Henry, alipofika Henry aliwahi kuufunga mlango, kisha akamtolea kisu na kumwambia aidha kubali Kupigwa Picha za Uchi kupitia simu ya mwanaume huyo au ampe "Penzi"

Thelma alikubali kuvua nguo na kumwambia atampa Penzi lakini asimpige Picha, Henry akapewa alichokihitaji huku akiwa ameshikilia kisu chake mkononi na baadae akampiga picha na Video msichana huyo kisha akizirusha mtandaoni na ku share na rafiki zake.

Polisi Wameshamkamata mwanaume huyo, ingawa amekana mashtaka hayo  yupo mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yake itasikilizwa tena tarehe 4 mwezi wa 9, 2013.


Read More »

Msichana Mwingine Auliwa, Face Book yamponza

;">

Wito umetolewa kwa watoto wa kike kupunguza kwenda sehemu kukutana na watu wasiowafahamu au kwa kuwajua kwa uchache kupitia mitandao ya kijamii, hususan Face book ili kuepuka madhara ambayo siku za hivi karibuni yamekuwa yakiwakuta wengi.

Mwanafunzi huyo wa Shahada ya Sheria kutoka Abuja amefikwa na Umauti baada ya kula kinachosadikiwa kuwa sumu. Imeelezwa kuwa binti huyo alitoka chuoni na akamuaga room mate wake kwamba anakwenda kukutana na jamaa ambaye walikuwa wana chat kupitia face book, ingawa alikatazwa lakini aliamua kwenda tu.

Asubuhi yake ndo mwili ukagundulika ukiwa umetelekezwa barabarani.


Read More »

Mrembo Jack, Ajutia Ndoa yake, Asema Alikurupuka.


Super Model wa Bongo, Jacky Patrick amefunguka na kusema ya kwamba kilichopelekea ndoa yake kudumu kwa kipindi kifupi ni kukosa tathmini ya kina na kutofanya maamuzi ya busara juu ya suala la ndoa.

Jack ameongea na gazeti moja hapa nchini na kusema ya kwamba, laiti wangekaa angalau miaka miwili katika uchumba basi angeweza kumsoma vizuri mumewe huyo kitabia na anaimani asingedumbukia katika shimo hilo.

Jack aliolewa na mfanayabiashara maarufu hapa Bongo ambaye kuna kipindi aliwahi kukamatwa kutokana na skendo za madawa ya kulevya Abdulatif Fundikira Maaruf kama "Tiff"


Read More »

Wanawake wenye jinsia Mbili, Huoa na Kuolewa.



Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa michezo ya ajabu kufanywa na Wasichana, pia wavulana hususan katika suala zima la kujibadilisha jinsia kutoka aliyokupa Mola wako na kujipachika Unayoihusudu wewe kwa matamanio yako.

Pia hiyo ni hali halisi ya mambo yalivyo hivi sasa kwani kuna wasichana wamegeuka wanaume na wengine wanabakisha zote mbili, huu ni mwisho wa dunia.

Read More »

Mwalimu wa Miaka 22 ajihusisha kimapenzi na Mvulana wa miaka 15.

Kalee Warnick


Mwalimu wa Somo la Kiingeeza katika Shule ya Wall huko New Jersey anakabiliwa na shitaka la matumizi mabaya ya madaraka na kumlazimisha mapenzi mwanafunzi wake wa miaka 15.

Kalee Warnick,22, alikamatwa Jumanne iliyopita kwa kosa hilo la kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mtoto, kesi yake imepangwa kusikilizwa Alhamisi Ijayo hata hivyo wakili wa mwalimu huyo Amesema ya kwamba mteja wake amepanga kukana mashtaka yanayomkabili.

Shule hiyo ambayo mwalimu huyo pia alisoma na kumaliza mwaka 2008

Read More »

Eniola Auliza Mashabiki kuhusu kuwa Dada yake Rick Ross!!


Yule mwanamke mnene na anayekula kushinda wanawake wa Nigeria, Eniola Badmus ameandika katika page yake ya Instagram ikiwauliza wadau ya kwamba vipi kila mtu anamfananisha na Mwanamuziki kutoka Marekani, Rapper Rick Ross, yawezekana akawa dadake? Angalia picha mwenyewe kisha toa tathmini yako.

Read More »

Majanga ONA Majanga!!!! Mpaka Kieleweke Leo!!


Kama kawaida, Cheka Upate Afya, leo nakuletea Picha niliyoipata katika mtandao wa kijamii huku ikiwa Commented ya Kwamba Mpare Utamjua Tu!!!! Walionaje hili?

Read More »

Ex-Lover wa Pokello, Mshiriki wa BBA Amjibu kwa Nyimbo.


Mwanamuziki, Rapper Stunner ameachia Single yake mpya inayokwenda kwa jina la "Bye Bye" ambayo kiundani inamjibu Aliyekuwa Mpenzi wake, Mwakilishi katika jumba la BBA The Chase, Pokello ambaye uhusiano wao ulivunjika baada ya mwanamke huyo kuanzisha mahusiano na Mshiriki Mwenzie Elikem wa Mjengoni hapo

Pokello alimkacha Stunner live katika mahojiano na kiyuo kimoja cha Television cha nchi hiyo, wengi wamesema mbinu ya mwanadada huyo kujiweka karibu na Stunner ilikuwa ni kujijengea Umaarufu tu.

Read More »

Justin Bieber Awatemea Mate Mashabiki walikuwa wamejazana kumshangaa!!!


Kweli majuu hapaishiwi vituko, Mkali wa Pop Kijana mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amefanya Kufuru ya aina yake baada ya kuwatemea mate mamia ya mashabiki waliokuwa wamejazana chini katika ghoroma moja alipokuwa amekwenda kwa rafiki zake Alhamis ya Tarehe 25 July. Angalia Picha zaidi Chini..


Read More »

Angalia Alichokiandika Selly katika Ukurasa wa Twitter Baada ya Nando Kutimuliwa BBA The Chase.

-->   Mshiriki kutoka Ghana aliyewahi kukashifiwa ya kwamba amemwambukiza magonjwa ya zinaa mshiriki wa Tanzania, Selly ameandika Kauli ya Kufurahia kutolewa kwa Nando katika Jumba hilo la BBA.

Angalia Mwenyewe:-


@therealsellygh
My God has fought my battle! All the stigmatization..hmm!! Fanx 2 all my friends and fans! Fanks to Africa!!

 

Read More »

Justin Bieber Awatemea Mate Mashabiki walikuwa wamejazana kumshangaa!!!


Kweli majuu hapaishiwi vituko, Mkali wa Pop Kijana mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amefanya Kufuru ya aina yake baada ya kuwatemea mate mamia ya mashabiki waliokuwa wamejazana chini katika ghoroma moja alipokuwa amekwenda kwa rafiki zake Alhamis ya Tarehe 25 July. Angalia Picha zaidi Chini..


Read More »

Maskini, Msichana wa Chuo Akutwa Amefariki katika Nyumba ya Kulala Wageni.





Msichana Aliyetambuliwa kwa jina la Florence Ngwu, Mwanafunzi katika chuo kikuu cha Nigeria Amepatwa na Umauti Katika Hotel Moja Mjini Lagos, Nigeria. Mwili wa Msichana Huyo Ulikutwa sakafuni.

Mpaka Sasa hakuna taarifa za ziada zilizotolewa, pia haijajulikana ni kitu gani kilimtoa Chuoni na Kwenda Lagos.



Read More »

Lulu Ajipanga Kurudi Darasani Tena


STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekazia nia yake ya kutaka kurudi shule siku chache zijazo.
Lulu aliandika hayo juzikati alipokuwa akichati na mashabiki wake kupitia ukurasa wa facebook ambapo alikuwa akiulizwa maswali na kuyajibu live kupitia Runinga ya East Africa.
Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza Lulu kuhusu mipango yake ya kurudi shuleni ambapo alimjibu kuwa yupo katika mipango  hiyo hivyo hivi karibuni atarudi darasani.
“Am on process..soon mpenzi nitarudi darasani,” aliandika Lulu ambaye awali alidaiwa kukatisha masomo yake ya sekondari.
Source: GPL

Read More »

Mlemavu wa Miguu amvua Papa Mwenye Kilo zaidi ya 250.


Kijana Mlemavu wa miguu, Matt Sechrist, 19 juzi aliandika kumbukumbu ya maisha yake baada ya kumkamata Papa mwenye uzito wa zaidi ya kilo 250 katika Fukwe za Vilano huko Florida.

Matt alifanikiwa kumkamata Papa huyo akisaidiwa na Baba yake pamoja na Rafiki wa Babab yake, Iliwachukua takribani saa moja kuhangaika na kiumbe huyo mpaka kumtoa nchi kavu, hata hivyo baada ya kupiga nae(Papa) picha za ukumbusho pamoja na watu wengine walimrudisha katika maji.

Read More »

Huyu ndiye Msichana Mrembo kuliko wote, kwa mwaka 2013, Ashinda zaidi ya Million 4 Naira, Kuiwakilisha Nigeria Indonesia

-->

Anna Ebiere Banner, 18 ndio mshindi wa lile shindano la Mrembo Mzuri kuliko wote kwa Nigeria 2013. Msichana huyo aliweza kuibuka kidedea na kuwabwaga washindani wengine 31 na kujizolea kiasi cha shilingi za Kinageria 4 Million(Naira) 

Mshindi huyo anatarajia kuiwakilisha Nigeria katika kinyang'anyiro cha kumsaka Mrembo Mzuri wa Dunia mnamo Septer 28 huko Jakarta Indonesia.


Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger