Showing posts with label Habari za Kimataifa. Show all posts

Kutana na Mtoto wa Miujiza Aliyezaliwa Tarehe 11.12.13 Mida ya Saa 14:15


Mara nyingi mtoto wa kwanza wa mama yeyote huwa ni wa matukio na mambo mengi sana anapozaliwa - ila siku ambayo mtoto wa Chelsea Johnson alizaliwa ilifanya kuwa na kitu kikubwa cha ziada kukikumbuka na kwa sababu maalum kabisa.

Sio tu kwamba alikuwa kama Landon-Jonah Johnson ambaye alizaliwa mnamo December 11, 2013, ila pia alifanya timing ya ajabu kwa kuingia Duniani, hii ni baada ya mtoto huyo kuziliwa mnamo majira ya saa 14:15 hivyo kufanya siku na muda aliozaliwa kusomeka hivi 11/12/13 14:15.

Chelsea, mwenye miaka 21, kutoka Rawmarsh, Rotherham, alisema kwamba mtoto wake ni wa ‘miujiza’.

“Ni mtoto maalumu,” alisema. “Nasubiri kwa hamu kuja kumueleza kipindi atakapokuwa mkubwa, na kwamba anatambua ni aina gani ya tukio lilikuwa
.” 


Read More »

MCHAGA AICHOMA NYUMBA YAKE MOTO BAADA YA KUBAINI MKEWE ANAISALITI NDOA YAO HUKU SEGEREA DAR.



Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.

Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea Jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.

Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali

Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo.

Mpaka Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.

Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.


Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa



Read More »

RAIS KIKWETE ATOA HOTOBA KATIKA MAZISHI YA MANDELA HUKO QUNU AFRICA YA KUSINI




Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika mazishi ya Nelson Mandela kijijini Qunu, Afrika Kusini.
Jeneza lenye mwili wa Hayati Nelson Mandela likiwa mbele ya waombolezaji katika kijiji cha Qunu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehutubia kwenye shughuli ya mwisho ya mazishi ya Nelson Mandela katika Kijiji Cha Qunu ambapo ndipo maziko yanapofanyika hapo baadaye.
Rais Kikwete amesimulia uhusiano wa karibu uliokuwepo enzi za utawala wa Mandela na Mwalimu Nyerere.
Mwili wa hayati Mandela utazikwa kwa tamaduni za Xhosa, ambapo ng’ombe dume atachinjwa na jeneza la Mandela kufungwa kwa ngozi ya Chui.

GPL

Read More »

SAFARI YA KUUGA MWILI WA MANDELA, ANGALIA PICS HAPA.



December 13.
A cheering man climbs up a fence after the casket of Mandela passed on its way to the Union Buildings on December 13.A cheering man climbs up a fence after the casket of Mandela passed on its way to the Union Buildings on December 13.
A rainbow forms over the Union Buildings in Pretoria on Thursday, December 12, after the public viewing of Mandela's casket. A rainbow forms over the Union Buildings in Pretoria on Thursday, December 12, after the public viewing of Mandela's casket.
Mandela's funeral procession drives toward the Union Buildings on December 12. Each morning his remains were transported from the mortuary to the government buildings. Mandela's funeral procession drives toward the Union Buildings on December 12. Each morning his remains were transported from the mortuary to the government…



The hearse carrying former South African President Nelson Mandela leaves the Union Buildings after the final day of his lying in state in Pretoria, South Africa, on Friday, December 13.The national flag-draped coffin of the former South African President is carried down steps of the Union Buildings at the end of the third and final day of lying in state on December 13.South African Naval personnel stand guard around Mandela's casket as he is carried to the Union Buildings on the final day of his lying in state on December 13.South African Naval personnel stand guard around Mandela's casket as he is carried to the Union Buildings on the final day of his lying in state on 

Read More »

BAADA YA MIAKA 112, BARAFU YAANGUKA NA KUJAA CAIRO


Watu wengi wanapolifikiri jiji la Cairo hakika watakuwa wanafikiria juu ya mazingira ya joto na vumbi.

Ila kitu kimoja kisichokuwa cha kawaidia kimetokea kwenye eneo hilo usiku - barafu imemwagika.


Kwa mujibu wa waandishi wa ndani wamesema hii ni mara ya kwanza kwa barafu kushuka kwenye mji huo mkuu wa Misri ndani ya miaka 112.

Picha za kushangaza zimeonyesha mji huo ambao mara nyingi huwa ni wenye joto ukiwa umefunikwa na weupe wa barafu.

Wananchi wa Misri walitumia mtandao wa Twitter kuposti baadhi ya picha za hali hiyo ya kushangaza.




DC Blog.


Read More »

MBUZI AZAA MTOTO MWENYE SURA YA BINADAMU HUKO KENYA


Wakazi wa eneo la Likoni, Mombasa nchini Kenya walipatwa na mshangao mkubwa mara baada ya mbuzi mmoja kujifungua mtoto mwenye sura inayofanana na binadamu.

Tukio hilo lilifanya shughuli mbalimbali kwenye kijiji hicho kusimama huku wakazi wa eneo hilo wakiwa wanastaajabu juu ya tukio hilo la ajabu.


Read More »

KIM K AJITAMBA BAADA Y KURUDISHA FIGURE YAKE NA KUWA KAMA HAJAJIFUNGUA



Kim Kardashian ameliweka wazi umbele lake matata miezi sita baada ya kujifungua, huku akiwa amevaa b!kini na brazia nyeupe kwenye kava la wiki hii la jarida la Us Weekly.

Ameonekana poa sio...!

Read More »

MWANAMITINDO NAOMI CAMPBELL AMWAGA MACHOZI MBELE YA JENEZA LA MANDELA


Mwanamitindo nyota Duniani Naomi Campbell alijikuta akimwaga machozi alipokuwa anapita kuliangalia jeneza la Hayati Nelson Mandela, wakati mwili wa nembo ya mpigania ubaguzi wa rangi huyo na aliyekuwa Rais mweusi wa kwanza wa Afrika Kusini ulipowekwa kwenye majengo ya Union ndani jiji la Pretoria.
Maelfu ya watu walifika kumuaga Mandela, watu mashuhuri Duniani walitoa heshima zao za mwisho kwa nembo hiyo ya Ulimwengu.

Nelson Mandela alifariki mnamo Alhamisi ya December 5, 2013  akiwa na umri wa miaka 95 na atazikwa siku ya Jumapili December 15, 2013 ndani ya Qunu, nyumbani kwao Mashariki ya Jimbo la Cape.

Read More »

OPRAH AFUNGUKA KWANINI HANA WATOTO


Kwenye taarifa za hivi karibuni za Waandishi wa Hollywood, Oprah amefunguka juu ya kwa nini hana watoto na ukweli wa juu ya hali hiyo kutohusani na wanachohisi wengi kwamba hana uwezo wa kushika ujauzito huku akielezea kwa sababu kuu ni yeye kutaka kuwa mwanamke mwenye nguvu.

"Kama ningekuwa na watoto, watoto wangu wangenichukia. "Wangeishia kwenye hali ya kuniongelea kama ilivyo kwenye Oprah show; sababu kuna kitu katika maisha yangu kingeishia kuteseka na inawezekana kabisa wangekuwa wao. Gayle [King, rafiki wa karibu Winfrey ambaye ni mama wa watoto wawili] alikuwa ni aina ya mtoto ambaye, kwenye daraja la saba la darasa, alikuwa anaandika jina lake chini na majina ya watoto wake. Wakati alipokuwa na ndoto hizo za mchana, nilikuwa na ndoto za mchana juu vipi naweza kuwa Martin Luther King."

DC Blog


Read More »

NYUMBA YA ASKOFU TUTU YAVAMIWA NA WEZI


Wezi wamevunja na kuingia nyumbani kwa Askofu mstaafu Desmond Tutu.
Polisi wamesema wizi huo ulifanyika wakati bwana Tutu akiwa katika ibada ya Nelson Mandela Mjini Johannesburg.

Inaarifiwa Tutu aliibiwa vitu vyake wakati akiwa anahudhuria ibada maalum ya kumuaga Hayati Nelson Mandela siku ya Jumanne.

Aidha wameelezea kuwa uvamizi ulifanyika nyumbani kwake mjini Cape Town Ahamisi jioni baada ya kutoa hotuba katika ibada ya Mandela siku hiyo.Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa FNB mtaani Soweto.
Wizi na uvamizi wa nyumba za watu ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini ambako visa vya uhalifu viko juu sana.

CHANZO NI BBC SWAHILI




Read More »

THE GAME AJICHORA TATOO YA MANDELA MWILINI MWAKE



Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, rapa mashuhuri toka nchini Marekani, The Game amechora tattoo ya sura ya Nelson Mandela kwenye mwili wake.
Rapa huyo ameposti na ku-share picha hizo na mashabiki wake, akiandika;
“The finished “Nelson Mandela” lookin out of the prison bars by @NikkoHurtado done on my side. 7 hour sitting…. Few more hours to tie in the tats around it & we solid. #NelsonMandela #RIP #Legend #Leader #Freedom #Peace #Equality #Tattoos #SouthAfrica”.

Angalia picha hapo chini.




Read More »

MAKOMANDO WA KIMAREKANI WALIVYOSHIKILIA ULINZI KATIKA IBADA YA MZEE MANDELA


Saa chache kabla ya kuanza kwa tukio maalumu la kihistoria la Ibada ya Kitaifa ya kumuaga Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, makomandoo wa Marekani wameshika jukumu la ulinzi katika maeneo nyeti nchini hapa. Ulinzi huo unatokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barrack Obama, mkewe Michelle pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali, ambao watahudhuria tukio linalotarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu; ndani na nje ya Afrika Kusini.
Rais Jacob Zuma atahutubia katika ibada hiyo, ambayo itafanyika katika Uwanja wa FNB (Soccer City), wenye uwezo wa kuchukua watu 95,000 kwa wakati mmoja.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Afrika Kusini inasema milango ya uwanja huo ambao ulitumika wakati wa sherehe za ufunguzi na fainali za Kombe la Dunia 2010, itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 na Ibada ya kwaheri inatarajiwa kuanza saa 5:00 asubuhi.
Karibu barabara zote za kuingia uwanjani hapo zimetangazwa kufungwa kwa ajili ya magari yote, badala yake Serikali imeandaa usafiri wa bure kwa wananchi watakaokwenda katika tukio hilo.
Jana, kutwa nzima, helikopta zilikuwa zikiruka katika anga la Jiji la Johannesburg lakini zilitumia muda mwingi zaidi kuzunguka juu ya Uwanja wa FNB ulioko Soweto, huku kukiwa na taarifa kwamba makomandoo wa Marekani walikuwa kazini, kuhakikisha usalama wa kiongozi wao.
Pamoja nao, mamia ya polisi wa Afrika Kusini walionekana katika maeneo yanayozunguka uwanja huo, huku baadhi ya vyombo vya habari vikiwanukuu maofisa wa Serikali kwamba askari 11,000 watashiriki katika ulinzi wakati wa maombolezo na mazishi.
Ulinzi pia umeimarishwa katika sehemu mbalimbali za Jiji la Johannesburg pamoja na kule atakakozikwa katika Kijiji cha Qunu, Mthatha ambako wanajeshi wenye silaha wamelizunguka eneo la makazi ya kiongozi huyo.
Maeneo mengine yaliyowekewa ulinzi mkali ni katika viwanja vya ndege na katika Majengo ya Umoja (Union Buildings) jijini Pretoria ambako mwili wa Mandela utawekwa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima za mwisho kati ya keshokutwa na Ijumaa.
Vituo vya televisheni vya Afrika Kusini vilionyesha magari ya kijeshi zaidi ya 10 yakiwa yameegeshwa katika eneo linalozunguka makazi ya Mandela, Qunu.
Waandishi waliokuwa wamepiga kambi karibu na makazi ya Mandela, Qunu walihamishwa na kuwekwa mbali zaidi kutokana na sababu walizoelezwa kuwa ni za kiusalama.


Read More »

TOILET PAPER ZENYE SURA YA OBAMA ZATENGENEZWA HUKO MAJUU, MOJA YAUZWA SAWA NA TSH 8,000/= ZA BONGO


Maduka kwenye majimbo ya Kusini nchini Marekani yamejiingiza kwenye kimbembe kutokana na kuuza toilet paper zimechapwa picha ya Rais wa nchi hiyo Barack Obama.

Mtandao wa Houmatoday.com, ambao unajihusisha na habari za mji wa Louisiana, hivi karibuni ulitoa habari juu ya tukio hilo ambapo wakazi wa eneo hilo waliziona tishu hizo zikiuzwa kwenye duka jirani na kwao.


Mwanamke aliyeitwa Linda Williams, alighafirika alipoyaona mabunda ya tishu hizo alipokuwa akiingia kwenye duka hilo. Aliueleza mtandao wa wa Houmatoday.com, “Kwa muda wa miaka 52 nilioishi, sijawahi kuona picha ya Rais kwenye mabunda ya toilet paper.”

Meneja wa duka linalouza toilet paper hizo alisema makaratasi hayo ni moja kati ya bidhaa inayonunuliwa sana. Alieleza Houmatoday.com, “Hatujaribu kuikataza kwa mtu yeyote, ila ni swala tu la kibiashara.”

DC Blog.

Read More »

MANDELA AWAPONZA DROGBA NA NA EBOUE, WATOZWA FAINI NA CHAMA CHA MPIRA CHA UTURUKI



Didier Drogba na Emmanuel Eboue watatozwa faini na chama cha mpira cha Uturuki baada ya kuonyesha vesti ambazo zilionyesha ujumbe wa kuguswa kwao na kifo cha Nelson Mandela.

Add caption
Wachezaji hao wawili wa kimataifa toka Ivory Coast waliziweka wazi hisia zao kwa ujumbe huo mara baada ya mechi ya Galatasaray dhidi ya Elazigspor mnamo siku ya Ijumaa, kwenye mechi ya kwanza toka kifo cha kiongozi huyo wa Afrika Kusini kilipotokea.

Add caption

Nguli huyo wa Chelsea, Drogba alivua jezi yake kwenye mechi iliyoisha kwa kushinda 2-0 na kisha kuonyesha kuguswa kwake na kifo hicho, ambapo maandishi kwenye vesti yake yalisoma: ‘Thank you Madiba’ huku yale ya nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue yalisema: ‘Rest in Peace Nelson Mandela’.





Read More »

MIMI NI ZAIDI YA MANDELA, NA NTAFANYA MAKUBWA ZAIDI YAKE "KANYE WEST"




Kanye West kwa mara nyingine tena anashambuliwa, hii ni mara baada ya hivi karibuni kusema kwamba muda si mrefu atakuwa ni mtu mkubwa kama nembo ya mtetea haki za binadamu zaidi ya Nelson Mandela.

Kwenye mahojiano aliyoyoyafanya na WGCI radio ndani ya Chicago, rapa huyo wa Kimarekani alisema kwamba kifo cha kiongozi huyo aliyefariki akiwa na miaka 95 hatimaye kitawafanya watu wamuangalie zaidi yeye Kanye West kwa mafaniko yake.


Kanye alipoulizwa, kwa mtazamo wake, kwamba anaweza kumrithi Mandela kama kiongozi, alijibu,

“Mimi ndiyo Mandela ninayefata. Nina miaka 36, na nikiangalia kwenye kila kitu ambacho nimefanikiwa, ni swala tu la kulinganisha ndilo litakaloleta maana. Mpaka nakuja fika miaka 95, nitakuja kuwa ni shujaa mkubwa kuliko alivyowahi kuwa."

DC

Read More »

SHABIKI WA MAN U KENYA AJIUA BAADA YA KIPIGO CHA NEWCASTLE




Jamaa mmoja anayeaminika kuwa ni shabiki wa timu ya Manchester United mnamo siku ya Jumamosi usiku kwenye Jimbo la Pipeline jijini Nairobi, hii ni mara baada ya timu yake kufungwa goli 1-0 na Newcastle.

Polisi wamesema John Jimmy Macharia, mwenye miaka 23, alijirusha toka kwenye gorofa ya saba mara baada ya timu yake kupoteza mchezo mwengine kwenye mechi iliyochezwa Jumamosi jioni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake kuwa hawezi kuona timu yake ikifungwa mfululizo kabla ya kuamua kujirusha na kufa papo hapo.

“Wote walioshuhudia wanasema sababu ya jamaa kujiua ni kutokana na timu yake kufungwa ila maafisa wanaendelea kuongea na watu waliyekuwa nae kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.

Kibue aliwashauri vijana wa jiji hilo kutambua kwamba Ligi Kuu ya Uingereza ni kama aina nyingine ya michezo hivyo wanapaswa wasiwe wanaguswa sana kihisia na michuano hiyo.

“Sio mara ya kwanza kumpoteza kijana sababu ya Ligi ya Uingereza, ambayo ipo mbali na sisi, wanahitaji kujua kwamba hii ni michezo tu,” alisema Kibue.

Mwili wa marehemu ulitolewa na kupelekwa mochwari na polisi waliofika pale. Macharia inasemekana aliangukia kichwa pindi alipojirusha toka kwenye gorofa hilo.


Read More »

GRACA MACHEL, MJANE WA MANDELA NA SAMORA MACHEL



ANAITWA Graca Simbine Machel ni Mmozambique (Msumbiji). Kufuatia kifo cha rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru, Nelson Mandela (95) kilichotokea usiku wa kuamkia jana, Graca anakuwa mwanamke pekee duniani kuwa mjane wa marais wawili kwenye nchi mbili tofauti.
Marehemu Nelson Mandela (kushoto) na Graca Machel.
Mwaka 1975 hadi 1986, Graca alikuwa mke wa Rais wa Msumbiji, marehemu Samora Moses  Machel.  Wakati huo, Graca alikuwa waziri wa elimu na utamaduni wa nchi hiyo.
Baada ya kifo cha mumewe kilichotokea kwa ajali ya ndege mwaka 1986, Graca aliishi mjane hadi mwaka 1998 ambapo alifunga ndoa na Nelson Mandela akiwa rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru.  Ni baada ya Mandela kumtaliki mkewe wa pili, Winnie Madikizele Mandela kwa madai ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa.



Kuanzia hapo mwanamama huyo alianza kutambulika kwa jina la Graca Machel Mandela.
Hata hivyo, Graca alishika nafasi ya u-first lady wa ‘Sauz’ kwa mwaka mmoja tu, 1999 mumewe hakugombea tena urais.
Kifo cha mumewe kimempa ujane mwingine unaodaiwa kutotokea duniani, kuolewa na rais, rais kufa, kuolewa na rais mwingine naye kufa.

HISTORIA YA GRACA KWA UFUPI
Graca alizaliwa Oktoba 17, 1945 katika Jimbo la  Gaza nchini Msumbiji.
Alipata elimu ya msingi jimboni humo, elimu yake ya chuo kikuu aliipatia Lisbon, Ureno.
Ana watoto wawili, Malengani na Josina  aliowapata kwa marehemu Machel. Hakupata mtoto kwa Mandela.

Read More »

MAZISHI YA MANDELA NI DESEMBA 15 KIJIJINI KWAKE


Rais Jacob Zuma ametangaza kuwa mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 mwaka huu kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini.

Rais Zuma pia ametangaza siku 5 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.

Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinton na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha kushiriki.

Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.

Mwili wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi.

Read More »

PICHA YA KIPEKEE YA MZEE MANDELA NA MOHAMMED ALLY



Dunia ikiwa katika maombolezo ya shujaa huyu wa Africa, tunakumbuka na kuyaenzi mengi mazuri ya kwake, pichani hapo juu Mzee Mandela akiwa na Mohamed Ally akimpa "JEB" Kuashiria kuuenzi mchezo wa ujanani mwake ambapo mzee Nelson Mandela alikuwa ni Bondia.

Nelson Mandela, Madiba the great, ni mtu wa kipekee na mcheshi sana, na amekuwa hivi mpaka pumzi yake ya mwisho...! #RIPNelsonMandela

Read More »

Tanzania Ndani ya siku 3 za Maombolezo ya kifo cha Mandela


Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.

"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".

Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.

Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.

Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.

CHANZO: BBCSWAHILI


Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger