Showing posts with label Udaku Magazetini. Show all posts

Watu waliokufa wazidi "KUFUFUKA" mkoani Geita


HOFU imezidi kutanda kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kufuatia matukio ya watu waliofariki dunia na kuzikwa miaka iliyopita kuibuka wakiwa hai, Uwazi lina mkasa mwingine mpya.
Flora Onesmo (45) aliyefariki dunia Februari 28, 2008 baada ya kufufuka Aprili 12, 2013 katika Kijiji cha Kasamwa wilayani Geita.
Mgonda Thomas (22), aliyefariki dunia kwa kujinyonga Mei 28, mwaka jana na kuzikwa siku iliyofuata, Ijumaa iliyopita aliibukia karibu na mlango wa nyumbani kwao akiwa hai.
Tukio hilo ambalo bado la moto, lilijiri katika Kijiji cha Rumasa, Kata ya Buseresere, wilayani  Chato mkoani Geita.
Kwa mujibu wa chanzo, majirani ndiyo waliomshuhudia Mgonda akitembea barabarani saa tisa alasiri hatua chache kutoka kwenye mlango wa nyumba hiyo huku nguo zake zikiwa zimechakaa.
Shaban Maulid (16) aliyefariki dunia Januari 1, 2011 ambaye aliibukia Mtaa wa Mbugani jirani na nyumbani kwao, Kata ya 14, Kambarage mjini Geita.
Baba mzazi wa kijana huyo, mzee Thomas Msalaba (60) akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema majirani hao ndiyo waliomtaarifu kwamba mwanaye Mgonda alikuwa barabarani.
“Niliondoka kwenda kumshuhudia kama kweli ni mwanangu. Nilipofika, nilimchunguza kwa umakini sana na kubaini alikuwa yeye.
“Alama kubwa iliyokuwa kwenye mwili wa mwanangu ni kovu kwenye mkono wake wa kushoto lililotokana na kuungua moto, pia sura yake ilifanana sana na mama yake,” alisema mzee huyo.
Naye mama mzazi wa Mgonda, Martha Kitobelo alimthibitishia paparazi wetu kuwa kijana huyo ni mwanaye kweli.
Familia hiyo ilisema Mgonda alifariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia kamba aliyoifunga juu ya mti wa mwembe hatua chache kutoka nyumbani kwao. Haikujulikana chanzo cha kujinyonga.
Mzee Msalaba alisema kuwa, baada ya Mgonda kufariki dunia alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao na siku ya tatu ndugu walianua matanga.
Kufuatia hali ya Mgonda kuwa ya mawengemawenge na kushindwa kuzungumza, wazazi wake walimchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji wa eneo hilo aitwaye Juma Tabiho.
Mganga huyo alisema kijana huyo hakufa bali alichukuliwa msukule na maiti waliyoizika ilikuwa kiini macho.
Hata hivyo, katika tukio hilo Jeshi la Polisi Wilaya ya Chato likiongozwa na Mrakibu wa Polisi Wilaya, OCD Leonard Nyaoga lililazimika kufanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi waliopandwa na hasira waliotaka kufukua kaburi ili kuona kilichokuwa ndani.
Afande Nyaoga aliwaambia wananchi hao kwamba kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi na kuwaeleza kuwa chombo chenye uwezo wa kutoa kibali cha kufukua kaburi ni mahakama peke yake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Pudensiana Protas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi unaendelea ikiwa ni pamoja na kufanya utaratibu wa kumpima DNA kijana huyo ili kujiridhisha kama kweli ndiye Mgonda aliyefariki dunia mwaka jana.
Hili ni tukio la tatu kutokea mkoani Geita katika kipindi kisichozidi miaka mitano iliyopita.
Aprili 12, 2013 katika Kijiji cha Kasamwa wilayani Geita, Flora Onesmo (45) aliyefariki dunia Februari 28, 2008 aliibuka akiwa hai.
Septemba 28, mwaka huu aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mwatulole mjini Geita, Shaban Maulid (16) aliyefariki dunia  Januari 1, 2011 naye aliibukia Mtaa wa Mbugani jirani na nyumbani kwao, Kata ya 14, Kambarage mjini Geita.
Kufuatia matukio hayo yenye dalili za ushirikina, Askofu wa Kanisa la Zion Assemblies of God Geita, Edward Osako alisema katika maandiko hakuna binadamu aliyewahi kufa kisha akafufuka zaidi ya Lazaro aliyefufuliwa na Yesu akiwa kaburini.
“Haya matukio ya watu kufa na kuonekana wakiwa hai baada ya miaka kadhaa ni nguvu za giza ambapo hata kwenye Biblia yameandikwa,” alisema Askofu Osako.

chanzo: Global Publishers.

Read More »

Mume wa Pili wa Wastara Aibuka na Kuzua Mapya


Na Issa Mnally
MIEZI nane baada ya kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, hatimaye mume wa pili wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anataka ampatie mwanaye aliyezaa naye.
Ahmed Kushi na Wastara siku ya ndoa yao.
Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni mkewe kumezua mshangao mkubwa.
MADAI YA KUSHI
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Fares.
Alisema: “Kisheria bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.
Jamaa huyo alidai kuwa zaidi ya mara tatu amekuwa akimtaka Wastara ampatie mwanaye huyo ambaye kwa sasa ametimiza miaka minane bila ya mafanikio.
KWA NINI WAKATI HUU?
Gazeti hili liliamua kumbana kwa kumuuliza kwa nini ameibuka wakati huu baada ya Sajuki kufa na mbona hakujitokeza kwa zaidi ya kipindi cha miaka kumi iliyopita? Pia akaulizwa kwa nini ameamua kutafuta umaarufu kwa kumdhalilisha? Akaishia kukaa kimya.

WASTARA AFUNGUKA
Baada ya Kushi kuibuka na ishu hiyo yenye utata, gazeti hili lilizungumza na Wastara ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kuhusu mtoto, kama kweli alikuwa na lengo la kumchukua mwanaye na ananijua, basi atakuwa anawajua wazazi wangu hivyo angefuata utaratibu.
“Hakuna utaratibu kama huo kama kweli anamhitaji mwanaye angeenda kwa wazazi wangu, huko ni kunidhalilisha kwa kuwa ananiona mnyonge baada ya kufiwa na mume wangu Sajuki.
“Kama siyo kunidhalilisha ni nini? Naomba asitumie jina langu kutafuta umaarufu kwa kunichafua. Naomba aache kwa sababu ananiongezea maumivu juu ya maumivu.”
Kuhusu madai kwamba bado ni mkewe, Wastara alilia: “Hivi huyo mtu alikuwa wapi muda wote nikiwa na Sajuki? Mbona hakuibuka wakati mume wangu akiwa hai? Najua anatumia kigezo cha kuondoka Sajuki kunionea lakini Mungu anajua.”
NI KWELI ALIFUNGA  NDOA NA KUSHI?
Pamoja na kumbembeleza aeleze kama kweli aliwahi kufunga ndoa na Kushi, Wastara alisema: “Sitaki kumzungumzia mtu, naomba watu wawe na huruma kwangu, wasitumie kigezo cha kumpoteza Sajuki kunidhalilisha.”

SHEHE AMPINGA KUSHI
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimtafuta shehe wa Msikiti wa Nuur wa Magomeni-Mapipa jijini Dar, Juma  Simba ili kupata ufafanuzi juu ya talaka moja ambapo alimpinga Kushi kwa kusema kuwa kisheria Wastara si mkewe tena.
“Kumpa talaka moja si sababu ya kuendelea kuwa mke wake mpaka leo hii, sheria inasema kuwa Kushi alitakiwa kumrejea Wastara kabla ya miezi mitatu kupita tangu alipompa talaka moja,” alisema na kusisitiza kuwa ndoa hiyo ilishakufa.

YATOKANAYO
Awali ilidaiwa kuwa Wastara aliwahi kuolewa mara mbili kabla ya kufunga ndoa na staa mwenzake wa filamu, Sajuki.
Ndoa ya kwanza ya Wastara aliifunga mwaka 1998 na Juma Mpemba ambaye alibahatika kupata naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Samir.
Sajuki alikuwa mume wa tatu kwa Wastara ambaye naye alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Farheen.

source: GPL

Read More »

Mke Mtarajiwa Anaswa Akijiuza, Atupwa Gerezani hadi Agosti 20


ZA mwizi arobaini! Kauli hiyo ya wahenga ilitimia Jumatatu iliyopita kufuatia msichana Pili Baraka (21) aliyevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake hivi karibuni (jina tunalihifadhi) kujikuta akitupwa Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kunaswa kwa tuhuma za ukahaba, Amani linakupasha.
Mrembo huyo alifikishwa kwenye Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) na kusomewa shitaka na mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timothy Lyon.
Akisoma shitaka hilo, Magodi alisema: Agosti 5, mwaka huu, saa nane usiku, Pili alinaswa kwenye maeneo ya Manzese jijini Dar akifanya biashara ya ukahaba.
Aliposomewa shitaka lake hilo, Pili aliinamisha kichwa na kujibu kwa kifupi: Si kweli.
Licha ya kukana shitaka hilo, Hakimu Lyon alimtaka mchumba huyo wa mtu kutafuta wadhamini wawili lakini aligonga mwamba na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Agosti 20, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Akijitetea kabla ya kupandishwa kwenye karandinga kwenda Segerea, Pili aliiomba mahakama hiyo imuonee huruma asiende kuilia Sikukuu ya Idd, Segerea kwa kuwa mchumba’ake yuko safarini kikazi na hakuwa na mtu mwingine wa kumwekea dhamana, ombi ambalo lilikataliwa.
Source: GPL

Read More »

Mfanya Biashara wa Madini Apigwa Risasi na Kuuliwa baada ya Kutokea "Mtobozano"


Na Mwandishi Wetu, Arusha
JIJI la Arusha na Mkoa wa Manyara, hali ya hewa ilishachafuka, wingu zito limefunika kufuatia kuuawa kwa kupigwa risasi, mfanyakazi wa Kampuni ya Tanzanite One, Onesmo William Mushi.
Marehemu Onesmo William Mushi enzi za uhai wake.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ni bilionea wa madini, mkazi wa Arusha, Joseph Mwakipesile ‘Chusa’ ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki migodi, Mererani wilayani Simanjiro, Manyara.
Mtuhumiwa wa mauaji, Joseph Mwakipesile ‘Chusa’.
ONESMO ALIVYOUAWA
Habari zimedai kwamba Onesmo akiwa eneo lake la kazi, mgodini chini, alipigwa risasi mbili kifuani ambazo ziliondoa uhai wake.
Tukio hilo lilitokea saa 8 usiku, Julai 20, mwaka huu, chanzo kikitajwa kwamba ni mgogoro wa kugombea madini.
Imedaiwa kuwa Onesmo, akiwa na wafanyakazi wenzake wa Tanzanite One ambao wamefahamika kwa jina mojamoja, Kennedy na Leonard, walikutana na wachimbaji wadogowadogo hivyo kutokea mvutano wa kimaslahi.
Habari zimedai kwamba miongoni mwa wachimbaji hao wadogo, alikuwepo Chusa ambaye ndiye anadaiwa kufanya mashambulizi dhidi ya Onesmo.
Wafanyakazi wa Tanzanite One wakiwa na mabango.
FAMILIA YALIA KUMPOTEZA ONESMO
Julai 25, mwaka huu, Onesmo alizikwa kijijini kwao, Uswaa, Machame, Hai, Kilimanjaro hivyo kuhitimisha safari yake hapa duniani.
Vilio na huzuni vilitanda kipindi chote cha mazishi ya Onesmo, huku sikitiko kubwa likielekea kwa mjane wa marehemu ambaye ameachiwa watoto wawili ambao atawalea bila baba.
Mke wa marehemu, watoto wake na ndugu wengine walikuwa wanyonge muda wote wa mazishi, kuonesha namna walivyoguswa na kifo hicho.
MERERANI YATIKISIKA
Wiki moja baada ya Onesmo kuuawa, wafanyakazi wa Tanzanite One wapatao 200, walilitikisa eneo la Mererani na kusimamisha shughuli zote za uchimbaji madini mpaka wapate tamko la serikali.
Kishindo cha wafanyakazi hao kilisababisha shughuli kusimama hata katika migodi ya wachimbaji wadogo, kwani hasira zilikuwa kali mno.
Awali, wafanyakazi wa Tanzanite One waligoma kufanya kazi wakiitaka menejimenti ya kampuni hiyo kufuatilia haki zote, ikiwemo mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa na kufikishwa kortini.
Baadaye, wafanyakazi hao walikusanyika na mabango kisha kushinikiza sheria kuchukua mkondo wake, vilevile wakaituhumu serikali kufumbia macho suala hilo.
Aidha, wafanyakazi hao walibeba mabango yenye ujumbe ambao uliwatuhumu moja kwa moja baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi pamoja na wale wa madini Kanda ya Kaskazini kwamba hawaaminiki katika kutenda haki.
MIGODI YAFUNGWA
Kutokana na kifo cha Onesmo, Wizara ya Nishati na Madini, imeifunga kwa muda migodi minne inayozunguka eneo la mgodi wa Kampuni ya Tanzanite One ili kusafisha hali ya hewa iliyochafuka.
Wizara imefanya hivyo kufuatia malalamiko ya wafanyakazi wa Tanzanite One kwamba kifo cha Onesmo kimesababishwa na serikali kulea mgogoro wa mipaka kwa muda mrefu.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Benjamini Mchwampaka, alisema kuwa migodi iliyofungwa ni ile inayomilikiwa na wafanyabiashara Joseph Mwakipesile ‘Chusa’, Jackson Simon, Abdulhakim Mula pamoja na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Maning’oo.
SERIKALI YACHUKUA HATUA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Akili Mpwapwa, aliliambia gazeti hili kuwa Chusa alikamatwa yapata wiki mbili zilizopita, baada ya jeshi lake kujiridhisha na tuhuma dhidi yake.
“Tuliona tuhuma dhidi yake zina nguvu ndiyo maana tukamkamata,” alisema Mpwapwa na kuongeza: “Siku tatu zilizopita (kutoka Jumapili iliyopita), alifikishwa mahakamani, akasomewa mashtaka kwa mara ya kwanza na sasa hivi yupo gerezani.
“Sijajua atarudishwa lini mahakamani lakini hii ninayokupa ni taarifa ya uhakika kwamba huyo bwana yupo gerezani. Tulimkamata na kumfikisha mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji, siyo kwa ajili ya kuisaidia polisi.”
TATIZO LA MGOGORO
Kwa mujibu wa taarifa za Mererani, mgogoro wa mipaka kati ya wachimbaji wadogo na Kampuni ya Tanzanite One ni wa muda mrefu.
Imeelezwa kwamba mara kwa mara, wafanyakazi wa kampuni hiyo wamekuwa wakikutana na wachimbaji wadogo mgodini chini, hivyo kuibua mvutano.
Kitendo cha wachimbaji wadogo kukutana mgodini chini na wafanyakazi wa Tanzanite One, kinajulikana kama Mtobozano.
Kwa upande mwingine, imekuwa ikidaiwa kuwa Mtobozano ni lugha ya kulainisha mambo, kwani ukweli ni kwamba ni kitendo cha wachimbaji wadogo kuvamia mgodi wa Tanzanite One na kupora madini.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki migodi Mererani, hujipatia fedha haramu, kwa kuiba madini ya tanzanite katika migodi ya Tanzanite One.
Kufuatia hali hiyo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Uswaa Machame, Robinson Manga, alisema wakati wa ibada ya mazishi ya Onesmo kwamba lazima serikali itafute ufumbuzi wa kudumu kuhusiana na mipaka Mererani.
Mchungaji Manga alisema: “Tatizo la migogoro kati ya wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite na wawekezaji wakubwa limekuwa la miaka mingi, serikali inatakiwa kuangalia upya mipaka na kupata ufumbuzi wa kudumu.”

Source GAZETI LA UWAZI (GPL)

Read More »

Gumzo kuhusu Sakata la Mzee Majuto Kuoa kwa Siri Dar!!!!

-->


Chande Abdallah na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, kuna taarifa kwamba gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ almaarufu mzee Majuto amefunga ndoa ya siri ndani ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Tukio hilo limetokea Julai 8, mwaka huu pande za Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo mzee Majuto alifunga ndoa na msichana mbichi aitwaye Rehema Omary.
Mzee Majuto aliambatana na wasanii wenzake Suleiman Barafu aliyekuwa mpambe wake na mwingine aliyefahamika kwa jina la utani kama mama Sharon.
Baada ya waandishi wetu kupata taarifa kuhusu tukio hilo, waliwahi kutia timu Mbagala, nyumbani kwa binti huyo.
Baada ya kufika, waandishi wetu walibaini kuwa ni kweli kulikuwa na shamrashamra za ndoa ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri huku watu wakizuiliwa kupiga picha.
Muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Noah (namba za usajili tunazo) lililowabeba mzee Majuto na wapambe wake liliwasili.
Muoaji akaongozana na wakwe na mashehe kwenda Msikiti wa Aqswa uliopo jirani ambapo ndoa hiyo ilifungwa kisha wakarudi nyumbani ambako cherekochereko ziliendelea.
Paparazi wetu alifanikiwa kujipenyeza na kuonekana kama mmoja wa ndugu na kushuhudia mzee Majuto akikabidhiwa mkewe.
Baada ya robo saa, mzee Majuto na mkewe walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuingia kwenye gari hilo aina ya Noah.
Paparazi wetu alipojaribu ‘kufotoa’ picha kadhaa, alisababisha kuzuka kwa  kizaazaa kwa wanandugu waliomlazimisha kuzifuta picha hizo ambapo alitii.
Baada ya tukio hilo, waandishi wetu walijaribu kuzungumza na mzee Majuto kwa simu lakini kazi haikuwa nyepesi kwani simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Alilipopigiwa simu mpambe wa bwana harusi, Barafu, alisema hana la kusema na kusisitiza atafutwe mzee Majuto.
Mwandishi wetu alirudi Mbagala kwa mama wa biharusi ambaye alikuwa mkali na kusema kuwa atafutwe mzee Majuto.
Siku hiyohiyo mzee Majuto alipokea simu na kuulizwa kama ni kweli amefunga ndoa na msichana aitwaye Rehema.
Katika hali ya kushangaza, mzee Majuto alicheka sana na kudai kwamba utafiti wake umekakilika. Alipohojiwa ni utafiti gani alisema:
“Nilikuwa nafanya utafiti wa kutaka kuigiza filamu ya ndoa ya siri ndiyo maana nikaenda kule Mbagala lakini sasa nimeamini kwamba hakuna ndoa ya siri,” alisema mzee huyo huku akikwepa kukubali.
Habari zinasema kwamba mzee Majuto anakwepa kukubali kwamba amefunga ndoa kwa kumhofia mkewe wa kwanza ambaye amemuacha jijini Tanga.

Source: GPL

Read More »

Kajala Atimkia South Africa, Wadau Wamohofia na Madawa, Mwenyewe Asema ni kupunguza Stress Tu!!!


Imelda Mtema
MWIGIZAJI Bongo, Kajala Masanja ambaye miezi michache iliyopita alichomoka nyuma ya nondo za Segerea kwa dhamana, ametimkia nchini Afrika Kusini kupunguza mawazo.
Kajala Masanja.
Mapema wiki hii, Kajala alitupia picha zake mbalimbali katika mtandao wa Instagram zikimuonyesha akiwa nchini humo na kusindikiza na ujumbe wa maandishi uliosomeka kuwa amekwenda kwa ajili ya kubadilisha hali ya hewa kwani toka akumbwe na matatizo, hajapata mtoko wa kupumzisha akili.
“Nimekuja kubadilisha hali ya hewa  maana nimetoka kwenye matatizo, sijapata kabisa muda mzuri wa kuipumzisha akili yangu hivyo nimeona bora nije huku kupumzika kidogo kisha nitarejea nyumbani,” alisema Kajala.

Source: GPL

Read More »

Za mwizi, 40.!!! Kibaka achezea kipigo huko Kawe, ni baada ya kuruka geti.


Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.…
Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.
Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi waliochoshwa na wizi.
...Akiendelea kusulubiwa kabla ya kupelekwa polisi.
Baada ya kulainika akawa anapelekwa polisi.
Kutokana na kipigo jamaa huyo alianguka hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa.

MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Source:GPL


Read More »

Rafiki Wa Sharo Milionea Adaiwa Kudhulumu Mali za Marehemu

-->


MALI zilizoachwa na aliyekuwa staa wa vichekesho Bongo, marehemu Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Milionea’ zinadaiwa kudhulumiwa na rafiki yake wa karibu aliyejulikana kwa jina moja la Suma, Risasi Jumamosi lina  mkanda wote.


MADAI
Chanzo chetu kilichoongea na gazeti hili Julai 25, mwaka huu kilisema Suma anadaiwa kudhulumu mali za Sharo kufuatia kupewa madaraka ya kufuatilia na kuuza baadhi ya vitu bila fedha kumfikia mama wa marehemu, Zainabu Mkieti.

MAMA WA SHARO AFUNGUKA
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Alhamisi iliyopita, mama huyo alikiri kuonekana kwa njama za Suma kudhulumu mali hizo likiwemo gari aina ya Opa lenye namba za usajili T 879 CAR na shilingi milioni 1. 2 za seti ya sofa alizonunua marehemu siku chache kabla ya kifo.

AZUNGUMZIA GARI
“Kweli nahitaji msaada ili nifanikishe kupata mali za mwanangu kwani kuna mambo hayaeleweki, kikubwa ni gari ambalo baada ya arobaini tulimpa Suma akaliuze kwa shilingi milioni kumi na moja na anipe fedha hizo lakini hadi sasa sijaona hata shilingi mia. Arobaini ya Sharo ilikuwa Januari 2013.

FEDHA ZA MASOFA
“Ukiachilia mbali gari, kuna fedha za masofa shilingi milioni moja na laki mbili sijazipata hadi leo, Suma aliahidi kunipa baada ya kuuza masofa hayo kwa dada yake na nimeshajaribu kuzungumza naye lakini hakuna majibu ya ukweli.
“Kabla ya Tuzo za Kili Music, Juni, mwaka huu, mimi nilikuja Dar na nikaongea na Suma na mama yake kuhusu fedha hizo, nilipomuuliza kuhusu gari, Suma akasema hataliuza na badala yake baada ya siku mbili angenitumia fedha lakini hadi leo hii simpati kwenye simu.

FEDHA ZILIKUWA ZITUMIKE KWA UJENZI
“Nakosa njia rahisi ya kuzipata fedha hizo maana huyu Suma naona kama mjanja, nilikuwa nataka kuanza ujenzi  wa nyumba kwenye kiwanja alichokiacha marehemu lakini naona kama muda unakwenda,” alisema mama mzazi wa Sharo.

MAJIBU YA SUMA
Suma baada ya kupatikana kwenye simu yake ya kiganjani na kusomewa mashitaka hayo, alidai ameshaongea na mama Sharo lakini alisafiri na ni kweli alikuwa hapatikani kwenye simu.
“Mbona nimeshaongea na mama na mambo tumeyaweka safi, ujue nilikuwa South Africa (Afrika Kusini) nina kama wiki tatu tangu nirudi na kusema kweli sijawasiliana na mama Sharo ila tutamalizana tu mambo yakiwa vizuri,” alisema Suma.

KUMBUKUMBU
Sharo Milionea alifariki dunia kwa ajali ya barabarani Novemba 19, 2012 iliyotokea kwenye Kijiji cha Songa Maguzoni, Muheza Tanga akiwa ndani ya gari aina ya Harrier lenye namba za usajili T 378 BVR likitokea Dar es Salaam kwenda Tanga.
Alizikwa Novemba 23 kijijini kwao, Lusanga, Muheza, Tanga.

Source: GPL


Read More »

Mwanafunzi Ashikiwa Uchawi, Akutwa na zana kibao za uchawi huku akiwa na Nguo ya Ndani Tu!!!


Stori:Gladness Mallya na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, duniani kuna uchawi! Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Pasco (21) ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Samaritan iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara amekutwa getini kwa kaka’ke, Edward Raphael akiwa amefungwa kamba na matunguri.
Denti akiwa amaefungwa kamba
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni huko Yombo-Buza jijini Dar na kuibua sekeseke la aina yake kutokana na mazagazaga ya kichawi aliyokutwa nayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Pasco alikuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni huku akiwa na nguo ya ndani pekee.
Habari zilieleza kuwa pia kijana huyo alikuwa amepakwa unga na kuandikwa maandishi ya Kiarabu mwilini huku kiunoni akiwa na shanga, hali iliyowashangaza wengi.
Polisi akiwa eneo la tukio
Akizungumza na wanahabari wetu juu ya tukio hilo, kaka wa kijana huyo alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili, wiki mbili zilizopita ambapo aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake lakini alipofungua geti alishangaa kumuona mtu akiwa amelala akiwa hajitambui.
Alisema baada ya tukio hilo, alirudi ndani haraka na kumwita mpangaji wake ili akashuhudie alichokiona.

Mazagazaga aliyo kutwa nayo
Alisimulia kuwa baada ya mpangaji huyo kuamka, waliamua kwenda polisi lakini wakiwa huko, mkewe aliamua kwenda kumchunguza mtu huyo kwa makini usoni ambapo aligundua kuwa ni shemeji yake, jambo ambalo lilizidi kuwachanganya watu.
Alisema aliporudi alikuta umati mkubwa wa watu umemzunguka Pasco.
Wakazi wa eneo hilo wakishangaa

Kaka mtu alisema kuwa alitimba na askari ambao walimfungua kamba na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza lakini wakiwa njiani, kijana huyo alikuwa akiongea maneno ya ajabu kama vile mtu mwenye majini.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina la Mube, Joseph Paja alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema naye alikuwa miongoni mwa mashuhuda.
Alisema kuwa alipofika, alikuta kijana huyo aliyewahi kuishi mtaani hapo kwa kipindi kirefu akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hali ambayo ilimshangaza kila mtu.
Mchungaji wa Kanisa la Church of World, Steven Paul ambaye naye alishuhudia tukio hilo, alisema kuwa baada ya ndugu kuamua kumpeleka polisi aliambatana nao hadi kituoni lakini walipofika, askari walimtema kwa kigezo kuwa hakuwa na kesi ya kufunguliwa, wakashauri apelekwe hospitali.
Ilielezwa kuwa zoezi la kumpeleka hospitali lilifanyika lakini walipofika huko, madaktari walimkataa kwa kigezo kuwa hawakuona ugonjwa wowote, jambo lililosababisha hofu kutanda.
Akizungumza na waandishi wetu, mchungaji huyo alisema kutokana na kote huko kushindikana, aliamua kumchukua kijana huyo na kuishi naye nyumbani kwake kwa lengo la kumfanyia maombi.
Baada ya kumchukua, alianza dozi ya maombezi ya nguvu ambapo hivi sasa anaendelea vizuri.
Katika mahojiano na waandishi wetu, Pasco alisema hajui kilichotokea hadi akajikuta amefika Dar, tena getini kwa kaka yake akiwa uchi.
Alisimulia kuwa siku hiyo, alienda benki kutuma ada ya shule na baada ya hapo, alirudi nyumbani kwa bibi yake na kumkuta akiandaa ugali ambapo alikula kidogo kwani alikuwa akihisi maumivu makali ya kichwa.
Baada ya kushindwa kula vizuri, bibi yake alimtaka ale chungwa ambapo alichukua moja na kwenda nalo chumbani, akachukua panga kisha kulikata vipande viwili lakini alipoanza kula, kabla ya kumaliza kipande kimoja alihisi usingizi mzito ambapo alikuja kushtukia akiwa sehemu tofauti yaani getini kwa kaka yake akiwa amezingirwa na watu kibao.
Alieleza kuwa kutokana na kusumbuliwa na mauzauza ya kichawi ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kaka yake amhamishie Rorya mkoani Mara ambako alienda kuanza kidato cha pili wakati huku Dar alikuwa ameshafika kidato cha nne.

Chanzo: GPL

Read More »

Mwanaume Akatwa Miguu baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu



Na Mwandishi Wetu, Kilosa
ALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said  Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali, mkanda mzima upo mikononi mwa Amani.


Mke wa mtu sumu: Said  Iddi akiwa chini baada ya kukatwa miguu na Ali Omar.
Tukio hilo la kikatili lilijiri Julai 15, mwaka huu wakati Said na mama Ali walipokuwa ndani ya nyumba ya Ali iliyopo kijijini hapo.
MANENO YA SHUHUDA
Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema Said alifumaniwa ndani ya nyumba asubuhi akiwa na mke wa Ali baada ya kuwekewa mtego ambao ulimnasa vizuri.
“Ali alipewa habari na kijana mmoja aitwaye God kwamba mkewe si mwaminifu katika ndoa, akamwongezea kuwa anatoka kimapenzi na Said. Ndipo Ali na mnyetishaji wake huyo walipopanga kumfumania jamaa,” alisema shuhuda.
Chini ya ulinzi: Mwenye mali, Ali Omar (kati) akiwa chini ya ulinzi baada ya kumkata Said.
Aliongeza kudai kuwa, Said ni msimamizi wa mashamba ya Ali kijijini hapo na kwamba God ni mtoto wa mwenye nyumba ambayo Ali amepanga kijijini hapo.
MPANGO WA FUMANIZI
Habari zinapasha kuwa mara baada ya mnyetishaji kutoa taarifa za usaliti huo, Ali alimtafuta  ‘baunsa’ ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja na wakaweka mtego kwa kujificha karibu na nyumba hiyo ambayo Said angeingia ili kuivunja amri ya sita ya Mungu.
Umbea kazi: Kijana aitwaye God (kulia) aliyetoa taarifa kwa Ali naye akiwa chini ya ulinzi.
Katika kufanikisha mtego huo, mmbeya huyo alipewa jukumu la kuhakikisha nyendo za Said na mama Ali siku hiyo zinarekodiwa mpaka kuingia ndani ya nyumba hiyo na kumtaarifu Ali ambaye siku hiyo alimuaga mkewe kwamba amesafiri.

SAID ATINGA NYUMBANI KWA ALI
Habari zinasema mtoboa siri huyo alimwambia Said kuwa Ali amesafiri na ndipo jamaa akafunga safari kwenda kwa mama Ali kwa nia ya kujivinjari licha ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukifikia katikati.
Mwanamke hutulii?: Mke wa Ali Omar naye akipelekwa polisi baada ya tukio hilo.
Habari zinadai mara baada ya kufika kwa Ali, Said aliingia ndani ya nyumba bila kujua kwamba mwenye mke alikuwa amejificha jirani akisubiri mtego unase.
Inasemekana Said akiwa ndani, Ali na baunsa wake waliibuka kwa kutaarifiwa na God na kumnasa jamaa huyo huku akidai ni mgoni wake. Alimuuliza maswali kadhaa, yakiwemo haya:
“Umekuja kufanya nini ndani ya nyumba yangu? Kwa nini umekaa na mke wangu?”
Habari zinasema Said alijibu hakuona ubaya kwa kuwa yeye ni mwangalizi wa mashamba ya mwanaume huyo hivyo anaweza kuingia ndani kwake wakati wowote.
Said  Iddi akiwa amezungukwa na wananchi baada ya kukatwa miguu.
MWENYE MKE ATIBUKA NA MAJIBU, AMWAGA DAMU
Jibu hilo lilidaiwa kumtibua Ali na ndipo yeye na baunsa wake wapomfunga kamba miguuni Said na kuanza kumkata kwa panga mguu mmoja kisha kuugeukia wa pili.
Said alipiga mayowe yaliyowafanya wanakijiji kukimbilia eneo la tukio kwa lengo la kujua kulikoni ambapo walimkuta Said akiwa anavuja damu na sehemu ya nyuma ya miguu ikiwa nyanga’nyang’a.
Said akipelekwa kwenye difenda.
MWENYE MKE AKIMBIA, ANASWA
Ali, God na baunsa walikimbia eneo hilo. Baadhi ya wanawake walitumia khanga zao kuifunga miguu ya Said kwa lengo la kujaribu kuzuia damu isiendelee kumwagika. Said alikuwa akilia sana.
“Wanakijiji walichukizwa sana na ukatili uliofanywa na Ali, hivyo wakaanza kumsaka na kumkamata kichakani akiwa amejificha pamoja na God. Alipewa mkong’oto kwa lengo la kutaka kumuua, lakini viongozi wa kijiji walisihi asiuawe bali afikishwe kwenye kituo cha polisi,” alisema shuhuda.
...Akiingizwa ndani ya difenda.
MKE, MUME, MMBEYA WAFIKISHWA POLISI
Polisi wa Kituo cha Dumila waliitwa na kumchukua Said, Ali na God kwa kutumia gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T 750 AAJ. Mke wa Ali yeye alipelekwa polisi kwa pikipiki.
Walipofika kituoni, Said alipewa fomu ya matibabu ya polisi (PF 3) na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa matibabu.
“Pale hospitali Said alishonwa miguu yote lakini madaktari wakaamua ahamishiwe katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi,” alisema shuhuda huyo.
Bwana Said akiwa ndani ya difenda.
ANAWEZA ASITEMBEE TENA
Akaongeza: Daktari mmoja alisema haamini kama jamaa (Said) atatembea tena kwa sababu zana iliyotumika kumkata ilifika hadi kwenye mishipa ya nyuma ambayo ndiyo humfanya binadamu aweze kusimama na kutembea.
Said akishonwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
BAUNSA ASAKWA
Afisa mmoja wa polisi kituoni hapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema wanaendelea kumsaka baunsa aliyeshirikiana na Ali kumkata miguu Said.
...Said akizidi kupatiwa huduma.




 SOURCE: GPL

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger