Showing posts with label Udaku wa Ulaya. Show all posts

MCHEKI ETOO AKIWA NA MWANAE HAPA



Cheki picha zake alipokuwa mdogo uwanjani na akicheza kabumbu.


Samuel na David baada ya Fainali ya Copa De Rey
Baba na Mwana mnamo 2007

Read More »

Kutana na Mtoto wa Miujiza Aliyezaliwa Tarehe 11.12.13 Mida ya Saa 14:15


Mara nyingi mtoto wa kwanza wa mama yeyote huwa ni wa matukio na mambo mengi sana anapozaliwa - ila siku ambayo mtoto wa Chelsea Johnson alizaliwa ilifanya kuwa na kitu kikubwa cha ziada kukikumbuka na kwa sababu maalum kabisa.

Sio tu kwamba alikuwa kama Landon-Jonah Johnson ambaye alizaliwa mnamo December 11, 2013, ila pia alifanya timing ya ajabu kwa kuingia Duniani, hii ni baada ya mtoto huyo kuziliwa mnamo majira ya saa 14:15 hivyo kufanya siku na muda aliozaliwa kusomeka hivi 11/12/13 14:15.

Chelsea, mwenye miaka 21, kutoka Rawmarsh, Rotherham, alisema kwamba mtoto wake ni wa ‘miujiza’.

“Ni mtoto maalumu,” alisema. “Nasubiri kwa hamu kuja kumueleza kipindi atakapokuwa mkubwa, na kwamba anatambua ni aina gani ya tukio lilikuwa
.” 


Read More »

PICHA YA MTOTO WA KIM NA KANYE BAADA YA MIEZI 6


Nyota wa vipindi vya uhalisia, Kim Kardashian hivi karibuni aliamua kushea na jamii picha ya mtoto wake mzuri wa kike, North West.

Picha hiyo ya karibu ya mtoto wake wa kwanza aliyezaa na rapa Kanye West, inamuonyesha mtoto huyo akiwa mwenye furaha huku akiwa anacheka.

Read More »

KAMA JAMES BOND ANGEKUWA KIUKWELI BASI KWA WANAWAKE NA POMBE YANGEMKUTA HAYA:


KUNDI la madaktari wa Kingereza limefunguka na kusema kwamba kama James Bond angekuwa mtu wa ukweli, basi kimaisha zaidi angekuwa ni mtu wa kuwachezea wanawake na kwa wastani asingekuwa hai zaidi ya kuwa ameshakufa.

Kwa upande mwengine jamaa huyo anayetambulika kwa namba ya 007 inaelezwa kuwa pia jamaa angekuwa ni mlevi kupindukia, na hii ni kwa mujibu wa somo lililochapishwa na British Medical Journal (BMJ).

Kama tathmini zina muongozo, Bond angekuwa amekufa kwa pombe na tumbaku sambamba na magonjwa yanayohusika nayo, imesema taarifa hiyo.

DC Blog

Read More »

KHLOE KARDASHIAN AFUNGUA KESI YA MADAI YA TALAKA KWA LAMAR, NI BAADA YA MUMEWE HUYU KUZIDISHA USALITI


Inaonekana matatizo ya ndoa ya Khloe Kardashian kwa Lamar Odom yameshafika ukingoni, hii ni kutokana na kuwepo kwa taarifa kwamba nyota huyo wa vipindi halisia amefungua kesi ya madai ya talaka hapo jana.

Kardashian anategemea kutengana kimoja na mume wake ambaye ni nyota wa mpira wa kikapu, huku chanzo ikielezwa kuwa ni tofauti zao, TMZ imeripoti.
 
Wawili hao wametengana kwa kipindi cha miezi sasa, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Odom anahangaika juu ya ishu zake za madawa ya kulevya.

Nyota huyo wa vipindi halisia vya TV aliamua kumpiga chini Odom kimoja mara baada ya jamaa kuposti kwenye mitandao, video ya muziki wa rap iliyohusu usaliti, akisema: “Wakati Khloe akiwa nje ya mji, mimi naendelea kuwepo kwenye DL”.
 
Akiwa kwenye ndege kuelekea Australia Kardashian aliiona hiyo video ikiwa imeenea kwenye mitandao, na toka kipindi hicho Khloe hajawahi onekana akiwa amevaa pete yake ya ndoa.

DC Blog

Read More »

ANGALIA WABONGO WALIVYOFUNIKA NDANI YA CALIFORNIA KATIKA KWETU FASHION


Nuthing Makes a Woman more beautiful than the Belief that She is Beautiful..Trust Kwetu Fashion Design to Compliment your Beauty

Juu na chini Kwetu fashion ilivyo pepea…



Nuthing Makes a Woman more beautiful than the Belief that She is Beautiful..Trust Kwetu Fashion Design to Compliment your Beauty
Juu na chini Kwetu fashion ilivyo pepea California.


Read More »

BRUNO MARS NDIO MWANAMUZIKI BORA WA BILLBOARD 2013


Huenda Miley Cyrus ameongoza zaidi kwa kuwa juu nabni ukweli usiopingika kwamba Justin Timberlake amerudi kwa kishindo kwenye muziki, ila habari sahihi ni kwamba Bruno Mars ndiye ambaye ametajwa kuwa msanii bora wa Billboard kwa mwaka 2013.
"Ni maendeleo, ni heshima," Mars alisema kwenye mahojiano wiki hii. "Najisikia fahari kuwa sehemu ya timu hii yote niliyonayo."

Nyimbo za mwaka huu za mwimbaji huyo zinahusisha pia wimbo namba moja When I Was Your Man na ngoma namba 5 akiwa na Treasure.

Album yake kali, Unorthdox Juxebox, ilizinduliwa mwaka jana na imeuza zaidi ya nakala 1.8 million. Ikiwa ndiyo album ya pili bora kimauzo nyuma ya album ya Timberlake iitwayo The 20/20 Experience.

Read More »

KIM K AJITAMBA BAADA Y KURUDISHA FIGURE YAKE NA KUWA KAMA HAJAJIFUNGUA



Kim Kardashian ameliweka wazi umbele lake matata miezi sita baada ya kujifungua, huku akiwa amevaa b!kini na brazia nyeupe kwenye kava la wiki hii la jarida la Us Weekly.

Ameonekana poa sio...!

Read More »

MUIGIZAJI NYOTA WA TAMTHILIYA YA SHAMELESS, EMMY ROSSUM AJIACHIA MTUPU KATIKA JARIDA LA ESQUIRE





Huyu ni nyota wa tamthilia inayotamba kwa sasa iitwayo Shameless, anaitwa Emmy Rossum, hakika hakuwa akijali chochote zaidi ya kuondoa aibu wakati wa kupiga picha hizi ambazo ni maalum kwa ajili ya jarida la Marekani liitwalo Esquire.
Add caption

Bila wasi wala shaka, muigizaji huyu wa kike mwenye umri wa miaka 27 alipiga picha hizi za toleo la mwezi January 2014 la jarida hilo lenye kuhusu mitindo ya maisha.
 

Angalia picha zaidi hapo chini..




Read More »

OPRAH AFUNGUKA KWANINI HANA WATOTO


Kwenye taarifa za hivi karibuni za Waandishi wa Hollywood, Oprah amefunguka juu ya kwa nini hana watoto na ukweli wa juu ya hali hiyo kutohusani na wanachohisi wengi kwamba hana uwezo wa kushika ujauzito huku akielezea kwa sababu kuu ni yeye kutaka kuwa mwanamke mwenye nguvu.

"Kama ningekuwa na watoto, watoto wangu wangenichukia. "Wangeishia kwenye hali ya kuniongelea kama ilivyo kwenye Oprah show; sababu kuna kitu katika maisha yangu kingeishia kuteseka na inawezekana kabisa wangekuwa wao. Gayle [King, rafiki wa karibu Winfrey ambaye ni mama wa watoto wawili] alikuwa ni aina ya mtoto ambaye, kwenye daraja la saba la darasa, alikuwa anaandika jina lake chini na majina ya watoto wake. Wakati alipokuwa na ndoto hizo za mchana, nilikuwa na ndoto za mchana juu vipi naweza kuwa Martin Luther King."

DC Blog


Read More »

Mke wa Obama Aleta Wivu kwa Waziri Mkuu wa Denmark Mpaka Ikabidi Wabadili Siti na Mumewe Kwenye Ibada ya Kumbukumbu ya Nelson Mandela



Wakati viongozi mbalimbali Duniani walipokuwa kwenye maadhimisho ya kufurahia maisha ya kiongozi wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela, mitandao ya kijamii nayo ilikuwa ilikuwa na yake zaidi ya kufatilia na hasa juu ya watu binafsi na maisha yao yanavyokwenda.

Rais wa Marekani, Barack Obama, alifanikiwa kupanda kwenye jukwaa la uwanja wa FNB na kumuelezea Mandela kwa namna ya kipekee kwenye hotuba aliyoitoa, ila si mara moja ni zaidi ya mara mbili kuna matukio yaliyochukuliwa kwa picha ambayo kidogo yalileta hisia tofauti kwa wadaku mbalimbali.



Kwanza kulikuwa na picha ya Obama akionekana kusalimiana kwa kushikana mkono na Rais wa Cuba Raul Castro. Kisha kulikuwa na ile ambayo ilipigwa ikimuonyesha Obama akiwa Waziri Mkuu wa Denmark Bi. Helle Thorning-Schmidt picha mabayo walionekana wakiwa kwenye tabasamu sambamba na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron.


Baadhi ya mitandao ya kijamii imesema kwamba hakikuwa ni kitu sahihi kupiga picha za namna ile kwenye Ibada ya kumbukumbu hiyo, kwenye picha hizo watu wengi wameonekana kumuangalia zaidi First Lady wa Marekani Michelle Obama, ambaye alikuwa amekaa pembeni ya Obama, huku akionekana kuwa na muonekano wa hasira kwenye uso wake.

Wakati Michelle akionekana kuangalia katikati ya kiwanja, vichwa vya habari na twees mbalimbali zilikuwa vikimfatilia yeye zaidi kwa muonekano wake wa kutokuwa na furaha tofauti na viongozi wengine waliokuwa wanacheka pembeni yake.



Picha nyingine baadae iliwaonyesha Obama hao wakiwa wamebadilishana siti, Michelle alionekana akiwa amekaa na Waziri Mkuu huyo wa Denmark na Obama akionekana kuangalia mbele huku sura yake ikionekana kuwa ameboreka. Baadae Obama aliposimama wakiwa wanataka kuondoka, Michelle Obama alionekana anaongea na Thorning-Schmidt.
Add caption

Read More »

TOILET PAPER ZENYE SURA YA OBAMA ZATENGENEZWA HUKO MAJUU, MOJA YAUZWA SAWA NA TSH 8,000/= ZA BONGO


Maduka kwenye majimbo ya Kusini nchini Marekani yamejiingiza kwenye kimbembe kutokana na kuuza toilet paper zimechapwa picha ya Rais wa nchi hiyo Barack Obama.

Mtandao wa Houmatoday.com, ambao unajihusisha na habari za mji wa Louisiana, hivi karibuni ulitoa habari juu ya tukio hilo ambapo wakazi wa eneo hilo waliziona tishu hizo zikiuzwa kwenye duka jirani na kwao.


Mwanamke aliyeitwa Linda Williams, alighafirika alipoyaona mabunda ya tishu hizo alipokuwa akiingia kwenye duka hilo. Aliueleza mtandao wa wa Houmatoday.com, “Kwa muda wa miaka 52 nilioishi, sijawahi kuona picha ya Rais kwenye mabunda ya toilet paper.”

Meneja wa duka linalouza toilet paper hizo alisema makaratasi hayo ni moja kati ya bidhaa inayonunuliwa sana. Alieleza Houmatoday.com, “Hatujaribu kuikataza kwa mtu yeyote, ila ni swala tu la kibiashara.”

DC Blog.

Read More »

BAADA YA WANAIJERIA KUTUMIA "NYETI" KAMA KEKI YA BIRTHDAY, NICK MINAJ AFANYA BALAA ZAIDI, IANGALIA KEKI YAKE HAPA


Rapa wa kike toka US, ambaye pia ni muimbaji, muandishi, muigizaji na mtangazaji wa vipindi vya televisheni Onika Tanya Maraj, maarufu kama Nicki Minaj, mnamo siku ya Jumapili December 8, 2013, alitimiza miaka kadhaa.

Nicki Minaj alifikisha miaka 31, na hakika alisherehekea siku yake hiyo kwa mtindo wa kipekee. Keki iliyotumika kwenye birthday hiyo imevuja kwenye mitandao.

Icheki hapo chini:




Read More »

MCHEKI LADY GAGA HAPA AKIWA NA GAUNI LENYE IPAD MOJA KWA MOJA


Mkali huyu mwenye umri wa miaka 27 ambaye kwa sasa anayeshika nafasi za juu kwenye chati mbalimbali Duniani, kwenye kipindi cha friday night chat ndani ya jiji London aliamua kuvaa nguo hii isiyo na vishikizi kwa ajili ya kipindi hicho.

Gaga alivaa nguo hiyo yenye kava maalum la plastiki ambalo lina sehemu ya kuweka iPad ambayo imejengewa ndani yake.

DC Blog.

Read More »

UMEPATA KUIONA CHENI MPYA YA ALMASI YA 50 CENTS, CHENI AMBAYO THAMANI YAKE KWA BONGO WAWEZA JENGA MIJENGO KADHAA.


Rapa toka Marekani, ambaye pia ni mjasiriamali, muwekezaji na muigizaji 50 Cent sio tu kwamba ni tajiri, ila ni tajiri kupindukia.

Nyota huyo hivi karibuni alidhihirisha hilo kwa kuonyesha cheni yake kubwa ya thamani kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Cheni hiyo ina vidani 172 vya almasi ambavyo uzito wake unakaribia kilo mbili. ‘Fifty’ aliiposti picha hiyo, huku akiweka maneno haya chini yake:

“Mimi ni mtamu kwa sasa. Jaribu kilo mbili zenye vidani vya almasi 172 orijino”.



Sina hakika kwa sana ila kibongobongo kwa cheni hii huwezi kujenga shule kadhaa za kata...?

Kupitia Ukurasa wake, 50 aliandika " I am chunky right now. Try 2 kilos 172 carrots natural diamond"



Read More »

MIMI NI ZAIDI YA MANDELA, NA NTAFANYA MAKUBWA ZAIDI YAKE "KANYE WEST"




Kanye West kwa mara nyingine tena anashambuliwa, hii ni mara baada ya hivi karibuni kusema kwamba muda si mrefu atakuwa ni mtu mkubwa kama nembo ya mtetea haki za binadamu zaidi ya Nelson Mandela.

Kwenye mahojiano aliyoyoyafanya na WGCI radio ndani ya Chicago, rapa huyo wa Kimarekani alisema kwamba kifo cha kiongozi huyo aliyefariki akiwa na miaka 95 hatimaye kitawafanya watu wamuangalie zaidi yeye Kanye West kwa mafaniko yake.


Kanye alipoulizwa, kwa mtazamo wake, kwamba anaweza kumrithi Mandela kama kiongozi, alijibu,

“Mimi ndiyo Mandela ninayefata. Nina miaka 36, na nikiangalia kwenye kila kitu ambacho nimefanikiwa, ni swala tu la kulinganisha ndilo litakaloleta maana. Mpaka nakuja fika miaka 95, nitakuja kuwa ni shujaa mkubwa kuliko alivyowahi kuwa."

DC

Read More »

TIMU YA RUGBY YA WANAWAKE YAAMUA KUKAA "UTUPU" ILI KUKUSANYA FEDHA ZA HISANI




Timu ya wanawake ya Chuo cha Oxford inaonekana imeamua kushika vichwa vya watu na habari kwa ujumla mara baada ya kuamua kuja na kalenda yao ya kujitolea ya mwaka 2014.


Picha hizo za rangi nyeusi na nyeupe (black-and-white) zilipigwa kwenye jiji la Idyllic na zimetumika kwenye kalenda ambazo zimekuwa zikiuzwa kwa £10, pesaambazo zitatumika katika kuchangia kampeni ya Oxford juu ya tahadhali dhidi ya ufahamu wa afya.

Wachezaji wa timu hiyo waliamua kuja na mpango huo mara baada ya timu ya wanaume kutoka na toleo lao mwaka jana, kisha wao wakaelezwa: “Kama ingekuwa ni ninyi kwenye picha basi tungenunua moja.”

DC BLOG

Read More »

HATARIIII!!" AJIFUNGA KAMBA KATIKA "DUSHELELE" KISHA KUTEMBEA JUU YA KAMBA MLIMANI





Watu hawa wa ajabu walikutwa kwenye tamasha la highline wakiwa wanatembea juu ya kamba kwa umbali wa mita 61 huku wakiwa uc+hi wa mnyama - cha ajabu zaidi ni jamaa huyu aitwaye Andy Lewis ambaye tofauti na wenzake yeye aliamua kwenda mbali zaidi.

Wakitembea juu ya kamba hizo ambazo zilipita juu toka kwenye ardhi iliyokuwa chini kwa urefu wa mita 30, hakika jamaa waliyaweka maisha yao kwenye hatari kama sio kifo huku wakiwa wako uc+hi wa mnyama.

Majasiri hao waliacha nguo zao pembeni na kuvaa kamba moja ambayo waliifunga kwenye mguu na kiuno, ila kwa ishu ya Andy Lewis yeye ilikuwa ni ya kipekee zaidi kwani yeye aliifunga kamba hiyo kwenye "dudu" wake.

Angalia picha hapo chini...




DC Blog.

Read More »

ZAHA AKANUSHA KUWA NA MAHUSIANO NA MTOTO WA KOCHA WAKE, ASISITIZA HIYO SI SABABU YA KUKOSA NAMBA MAN U.





Wilfried Zaha amechukua hatua ya aina yake kukanusha taarifa zilizozagaa kwamba ana uhusiano wa kmap3nzi na mtoto wa kike wa kocha mkuu wa Manchester United David Moyes.
Winga huyo mwenye miaka 21 alinunuliwa na Sir Alex Ferguson kwa £15milllion lakini ameshindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza chini ya David Moyes.
Kumekuwepo na taarifa kwamba amekuwa hapewi nafasi ya kucheza na Moyes kwasababu ya mahusiano yake na binti wa kocha huyo aitwaye Lauren.
Lakini Zaha - ameonekana kukerwa sana na tetesi hizo - ametumia ukurasa wake wa Twittet kuwaambia mashabiki 490,000 kwamba taarifa hizo sio za kweli.
Zaha: The 21-year-old has found himself playing for the Under 21s this year instead of with the first team
'Sijawahi kuwa na mahusiano ya kmap3nzi wala kukutana na binti wa David Moyes, hivyo jambo hilo haliwezi kuwa sababu ya kukosa kwangu nafasi katika kikosi cha kwanza ...,' aliandika Zaha.
'Ningependa hizi taarifa za uongo ziachwe kusambazwa….Nitaichezea Manchester United pindi kocha atakapoana nipo tayari kufanya hivyo...'

Zaha aliichezea United katika mchezo wa kombe la hisani lakini tangu wakati huo ameichezea mechi moja tu ya mashindano dhidi ya Norwich City katika League Cup.


Read More »

WAVULANA WA CALIFORNIA WAMEANZA KUONGEA KAMA WASICHANA- UTAFITI


Vijana wengi wa kiume kwenye jimbo la California wameanza kuongea kama wasichana, kwa mujibu wa uchunguzi mpya.

Wataalamu wa lugha wanaamini kumekuwa na ongezeko la  wanaume kuongea 'kwa sauti ya juu' mwishoni mwa sentensi kama vile wanauliza swali.

Wavulana wengi wanaanza kuongea kwa sauti ya juu kuelekea mbele, aina ya uongeaji ambao wanawake hutumia kuongea, hii ni kwa mujibu wa somo hilo.

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger