Baadhi ya picha za FIESTA jana pale Leaders Club










 







 





 


 

Read More »

Sakata la Kuvaa Mlegezo (Kata K), BASATA wamvaa Ney wa Mitego.


Ney wa Mitego ambae ni staa wa single za ‘muziki gani’ na ‘salamu zao’ amethibitisha kupewa barua na baraza la sanaa Tanzania ikiwa ni onyo la kutoendelea kuvaa suruali mlegezo kwenye majukwaa mbalimbali anayoonekana.
 
 Kwenye interview yake na millardayo Ney amesema alipigiwa simu sana na namba moja lakini alikua amelala, alipoamka akakuta missedcalls nyingi so ikabidi apige ndio akaambiwa BASATA kuna barua yake ambapo baada ya kushindwa kwenda alipelekewa Manzese.
 
 Ney anasema: "Sielewe kama BASATA ndio wameamua kudili na milegezo, sijaelewa wao wanaangalia nini zaidi, nimejaribu kuuliza wakasema nikiendelea watanifungia kazi zangu....

"Ni kweli navaa mlegezo lakini kuna vitu vingi sana vya kufanyia kazi wao kama BASATA manake tunaibiwa kazi zetu kila siku mbona hawashughulikii hizo?’

"Mi tangu niko shule mlegezo ni tatizo langu kubwa ila nitajitahidi kupunguza japo nashangaa nimeandikiwa barua mimi mwenyewe wakati kuna wasanii wanavaa mlegezo hata kuliko mimi"





Read More »

Raisi wa Uswisi awazindua Watanzania na Fedha za Mafisadi


Katika mahojiano maalumu na timu ya waandishi wa Mwananchi na The Citizen jana, Graf alisema kuwa Serikali ya Tanzania inapaswa kusaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa za masuala ya usimamizi wa fedha na kodi ili kuweza kujua ni kina nani wameweka fedha nchini kwake na kunufaika na kodi.
Graf, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini, alisema kuwa hivi karibuni Serikali ya Uswisi ilisaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa kuhusu masuala ya fedha, ambao unajulikana kwa lugha ya Kiingereza kama `Convention on Mutual Administrative Assistance in Tax Matters’.
Alisema ikisaini mkataba huo ina maana itasaidiwa na Serikali ya Uswisi kupata fedha zilizofichwa na Watanzania.
“Serikali ya Tanzania inatakiwa kuweka mkakati wa kisheria utakaotengeneza mazingira ya kubadilishana taarifa za fedha na mataifa mengine. Kwa jambo hilo hata Serikali ya Uswisi inaweza kusaidia katika kupatikana kwa fedha zilizofichwa,” alisema Graf, ambaye anaongoza Serikali ya Uswisi kwani kwa kawaida Rais wa Bunge ndiye pia kiongozi wa taifa hilo.
Graf alisema kwa sasa itakuwa ngumu kwa Tanzania kupata fedha hizo kwani haijasaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa za fedha na mataifa mengine.
Alieleza pia katika miaka ya karibuni Serikali ya Uswisi imeandaa muswada wa sheria wa kubana fedha zilizopatikana kwa njia za kifisadi na kufichwa katika benki za Uswisi. Graf alisema sheria hiyo ikipita itaruhusu Serikali ya nchi hiyo kutaifisha fedha ambazo zimepatikana kwa njia haramu na kufichwa katika benki za huko.
Muswada huo unaoitwa kwa lugha ya Kiingereza `Freezing and Restitution of Assets of Politically Exposed Persons obtained by Unlawful Means Bill’ ulisomwa kwa mara ya kwanza kwenye Bunge la nchi hiyo mwezi Mei, mwaka huu.
Graf alisema faida nyingine ya Tanzania kusaini mkataba huo ni kuwa, itaweza kuwatoza kodi Watanzania hao walioweka fedha huko.
Alifafanua kuwa siyo fedha zote zinazowekwa kwenye benki za Uswisi kuwa ni haramu kwani kuna nyingine zimepatikana kihalali, lakini zinaweza kutozwa kodi.
“Tanzania inakosa kodi kutokana na fedha zilizohifadhiwa na Watanzania wenye akaunti kwenye benki za Uswisi,” aliongeza Graf, ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo Novemba 26, 2012 na kutakiwa kukaa madarakani kwa mwaka mmoja.
Graf alisema pia fedha za kodi zingeisaidia Tanzania kugharimia sekta mbalimbali za maendeleo.
Zito aitupia lawama Serikali
Naye Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, ambaye yuko nchini Uswisi akifuatilia masuala ya utoroshaji fedha na kufichwa kwenye benki za huko, alisema kuwa wakati shinikizo la dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na utoroshaji wa fedha kutoka nchi za Afrika, lakini Serikali ya Tanzania inasuasua juu ya kupambana na jambo hilo.
Zitto alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa moja ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata taarifa za kampuni kubwa za kimataifa yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana taarifa unaoitwa kwa lugha ya Kiingereza `automatic exchange of tax information’.
“Kutokana na shinikizo la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa `tax havens’ (nchi zinazohifadhi fedha kwa siri) fedha zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa taarifa,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).
Alisema kuwa Tanzania mpaka sasa haijaweka saini na Serikali haijatoa taarifa yoyote kwa umma juu ya sababu ya kutokufanya hivyo. “Ghana, Afrika Kusini na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama Tanzania zimeweka saini mkataba huu tayari,” aliongeza Zitto.Alisema asilimia 44 ya fedha za kigeni inazopata Serikali ya Tanzania zinatokana na mauzo ya madini nje. Kampuni za madini ndizo zinazoongoza kukwepa kodi.
Alisema Tanzania inapoteza jumla ya Dola 500 milioni (Sh783 milioni) na Dola 1.25 bilioni (Sh2 trilioni) kwa mwaka kutokana na kampuni kubwa za kimataifa kukwepa kodi.
“Hii ni sawa na kusema Tanzania inapoteza Dola2 milioni (Sh3.1 bilioni) kila siku kwa uporaji huu,” alisema Zitto.
Zitto alisema Serikali lazima ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi.
Jaji Werema agoma kujibu
Alipoulizwa juu ya Tanzania kutokusaini mikataba ya kimataifa ya kubadilishana taarifa za utoroshaji fedha na mambo au kodi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema hawezi kujibu suala hilo.
“Muulize huyo aliyekwambia kuwa Tanzania haijasaini mikataba ya kubadilishana taarifa za utoroshaji fedha na masuala ya kodi. Naomba uniache nifanye kazi zangu,” alijibu Jaji Werema kwa mkato na kukata simu.
Mahojiano kamili na Rais wa Uswisi, soma Mwananchi Jumapili.
Mwananchi.

Read More »

Huyu ndiye Producer wa " Number One" ya Diamond


Ukiingia ndani ya studio ya Burn Records iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam, huwezi kuamini kama ndiyo sehemu ‘zinakopikwa’ kazi za baadhi ya wasanii zinazowafanya kuwa maarufu na kuwaingizia kipato, kupitia shoo na mialiko ya ndani na nje ya nchi.
Studio hii iliyopo maeneo ya ‘uswahili’ imezingirwa na nyumba nyingi kiasi cha kushindwa kuijua njia kwa uharaka zaidi pale mtu anapotaka kufika kwa prodyuza huyo. Studio hii ni ndogo yenye vifaa vichache tu vya kimuziki lakini yenye prodyuza makini na mwenye kipaji.
Shadrack Willced Mongi maarufu ‘Sheddy Clever’ ndiye prodyuza wa studio hii iliyotengeneza wimbo wa ‘My Number One’ unaomilikiwa na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’, wimbo uliofanya vizuri katika levo za kimataifa.
Hata hivyo sehemu ya mahojiano na mwandishi wa Starehe ni kama ifuatavyo;
Swali: Mbona Studio yako ipo uchochoroni hivi?
Jibu: Unasema uchochoroni!  Wasanii wengi wamekuja hapa na wanatumia muda mwingi kuwepo ndani ya studio hii huku wakitumia vyakula vya hukuhuku kwetu uswahili, si jambo la ajabu. Lakini ni mazoea tu kwetu tunaona sawa na kwa upande wangu inanipa hamasa kwani najisikia huru kufanya kazi nikiwa maeneo haya.
Swali: Ndiyo kusema Diamond alikuja kurekodi kwenye studio hii?
Jibu: Ndiyo alikuja kurekodi katika studio hii na alikuwa akikaa hapa kutwa nzima. Yule jamaa anafanya kazi sijawahi ona kutoka kwa wasanii wengine akija hapa anatumia muda mwingi kujenga mashairi, hata hivyo anatumia akili kubwa sana katika kufanya kazi si sawa na vile watu wanamwona. Korasi ya wimbo wa My Number One tulitumia zaidi ya saa 12 kuitengeneza na saa nyingine 12 kuirekebisha, yupo makini sana. Ilichukua miezi sita kukamilika.
Swali: Ilikuwaje akapajua hapa?
Jibu: Diamond alinitafuta yeye mwenyewe, ilikuwa saa mbili asubuhi akanipigia na kunifahamisha jina lake akasema anakuja, kwa kuwa namba niliyokuwa nayo alishaacha kuitumia nilidhani si yeye lakini baada ya muda nikashangaa amefika. Alinitaka nimsikilizishe midundo nami nilifanya hivyo hatimaye akapenda mmoja wapo, basi tulipeana mikakati kazi ikafanyika.
Swali: Kazi uliyoifanya imeweza kumwingizia kitita kikubwa cha pesa mwanamuziki huyo vipi kwa upande wako inakuneemesha vipi?
Jibu: Hapana nilimfanyia kazi akanilipa ujira wangu mzuri tu, hivyo huko mbele ni kazi yake. Lakini katika upande wa hatimiliki hivi sasa tupo mbioni kuhakikisha chama chetu cha maprodyuza  cha Tanzania TSPA kinasajiliwa ili kuweza kutetea kazi zetu na hatimiliki.
Inaendelea katika Mwananchi

Read More »

"Sipo tayari kumvulia nguo bwana Misosi, labda anibake." Amanda


Staa  wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi  ‘Amanda’ amefunguka kuwa hawezi kurudia  makosa tena kwa kumvulia  nguo  aliyekuwa mpenzi wake, Joseph Rashau ‘Bwana Misosi’.

Akiongea  na  mwandishi wetu muda mchache baada ya wadau kibao kumtaka mwanadada huyo arudiane na mpenzi wake huyo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Amanda alisema tayari ameshapenda kwingine hivyo hapendi kumzungumzia mtu aliyeachana naye pia hana tabia ya kurudia matapishi yake.

"Sipo  tayari  kumvulia  nguo  bwana Misosi, labda  anibake,  kwani  nikishaachana  na  mtu  huwa  namtoa  moyoni  kabisa  na  ndio  maana  sipendi  hata  kusikia  lolote  juu  yake"..Alisema  Amanda
 


Read More »

"Sijawahi kufanya map3nz! na mwanaume yeyote tangu niachane na Diamond"...Jokate Mwegelo


Mtangazaji  wa Channel O mwenye mvuto wa aina yake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa tangu amwagane na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ hajawahi kungonoka  na mwanaume mwingine.

Penzi la Jokate na Diamond lilichanua kwa takriban miezi miwili mwaka jana wakati Kidoti alipomwagana na aliyekuwa mpenz wake, mcheza kikapu wa Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabit.

 Alipoulizwa anamudu vipi hisia za matamanio ya  kufanya  map3nz!, Jokate alisisitiza kuwa kazi pekee ndiyo silaha kubwa ya kumuepusha na vishawishi ingawa anatambua upo umuhimu wa kuwa na mpenzi.

 “Akitokea mkweli, nipo tayari ingawa hadi sasa hata sijajua nani anaweza kuwa kama alivyokuwa Hasheem, nilimpenda sana,” alisema.





Read More »

Aunt Lulu atangaza kuachana na biashara ya Ukahaba.....Awataka wateja wake waache kumtafuta kwa sasa


Msanii  Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ ameibuka na kusema kuwa sasa hawezi kurudia biashara ya kujiuza na kuwataka wanaodhani kuwa bado yuko na tabia hiyo waondoe hisia hizo kwani kwa sasa si Lulu wa zamani tena.

Akizungumza na mwandishi wetu, Anti Lulu alisema sasa hivi amejipanga kuyaendesha maisha yake kihalali na kwa kiasi kikubwa amefanikiwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wanaotaka kumrudisha nyuma.

“Watu wameniibia dukani kwangu ili kunirudisha nyuma lakini hawaniwezi, siwezi  kuurudia  ukahaba  tena.

"Nilikuwa  najiuza  kutokana   na  hali  ngumu  ya  maisha. Kwa  sasa  maisha  yangu  yamenyooka  na  sioni  haja  ya  kuitwa  kahaba  tena.

"Nataka  wanaume wanaodhani  bado  najiuza waelewe  hivyo.Mimi  ni  Lulu  mpya.Nimeshanunua  uwanja  Bunju  na  muda  si  mrefu  ntaanza  kujenga"..Aunt  Lulu
 



Read More »

Serikali yatangaza kuvihamisha vituo vya dala dala vya Ubungo na Mwenge jijini Dar


VITUO vya daladala vya Ubungo na Mwenge vinahamishwa kupisha Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart), ambao miundombinu yake inaendelea kujengwa.

Kituo cha Ubungo kitahamishiwa nyuma ya jengo la Mawasiliano lililopo Barabara ya Sam Nujoma, vivyo hivyo kituo cha Mwenge, kitatumika kwa ajili ya kushusha abiria pekee.

Ofisa Habari wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera amesema, magari ya Mwenge, yatakuwa na uamuzi wa ama kuishia kwenye stendi ya Makumbusho ;au kwenda hadi kituo hicho kitakachohudumia magari ya Ubungo kilichoko Mawasiliano.

Kwa mujibu wa Mhowera, wakati wowote kuanzia sasa vituo hivyo, vitabomolewa kupisha mradi huo.

Hata hivyo, hakuelezea kwa undani juu ya maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho kipya. Alisema hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi, kuhusu hatua zinazochukuliwa na manispaa, kuwezesha wafanyabiashara ndogo kupata maeneo ya kuendesha shughuli zao.
Alisema baada ya kituo cha Ubungo kuhamishiwa katika eneo hilo jipya, hakutakuwa na mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza bidhaa zozote kama ilivyo sasa.

Alisema kuhamishwa kwa vituo hivyo, kutatoa nafasi kwa wafanyabiashara kwenda katika maeneo waliyopangiwa kwa kuwa hakutakuwa na nafasi, kwani yote yatatumika kwa ajili ya barabara.

“ Kwa hiyo ni bora wakaanza kujiondosha wenyewe mapema kabla hatua ya kuondolewa na ujenzi kuwafikia,” alisema.
Kwa mujibu wa ofisa habari huyo, yapo maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kazi hiyo katika masoko mbalimbali likiwemo laKijitonyama.

-Habari leo




Read More »

Burna Boy Apanda Stejini na Chupi Tu kisha Kumkombatia Miongoni mwa Wanenguaji wake wa Kike, Angalia Video.


Burna Boy akijiachia Stejini.

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria wiki iliyopita katika tamasha la kumuenzi Marehemu Fela alifanya kioja baada ya kutumbuiza nyimbo yake ya "Run My Face" akiwa amevaa chupi tu, na katika kuonesha msisitizo zaidi alimkamata mmoja wa wacheza shoo wake wa kike na kumsugua sugua kwa nyuma akiwa na nguo hiyo tu ya ndani.
Fela, Enzi zake katika moja ya matukio yake.

Angalia Video hapa chini:-


Read More »

Vatican yamsimamisha askofu Mjerumani kwa kupenda raha


Kumekuwa na kelele za waumini nchini Ujerumani wakishinikiza askofu huyo afukuzwe kwa kukiuka taratibu.
Vatican City. Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani (Vatican) yamemsimamisha kazi Askofu wa Jimbo la Limburg, Ujerumani Franz-Peter Tebartz-van Elst anayekabiliwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha kwa shughuli za kifahari.
Vatican ilieleza jana kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuridhika kuwa Askofu van Elst amekiuka maadili yaliyowekwa na Papa Francis kwa viongozi walioko chini yake akiwataka waishi maisha ya uchaji, umaskini.
Hadi sasa, kumekuwa na kelele nyingi miongoni mwa waumini nchini Ujerumani wakitaka askofu huyo afukuzwe kazi.
Miongoni mwa matumizi yake makubwa ni ujenzi wa makazi yake binafsi yaliyogharimu Euro 2.9 milioni (Dola 3.9 milioni), ukumbi wa chakula wenye mita za mraba 63 ambao ni pamoja na mesi na bafu yenye thamani ya Euro 15,000.
Askofu van Elst (53) amekuwa akituhumiwa kuendesha miradi hiyo kwenye mji wa kihistoria wa Limburg, ikiwamo makumbusho, kumbi za mikutano, kanisa dogo na nyumba ya makazi yake binafsi.
Fedha hizo zinatokana na mapato ambayo ni misamaha ya kodi kwa vikundi vya kidini nchini Ujerumani kwa mujibu wa sheria.
“Baada ya uchunguzi wa awali, Vatican imeamua kuchukua hatua kumsimamisha na kumwondoa kwenye usimamizi wa jimbo,” ilieleza taarifa hiyo.
“Baba Mtakatifu (Francis) amekuwa akifuatilia kwa karibu mambo yote yanayoendelea katika Jimbo la Limbuerg,” iliongeza taarifa hiyo.
“Hali hiyo imefikia mahali ambako kiongozi huyu hawezi kuendelea kusimamia kazi zake za kitume kama askofu wa jimbo.”
Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza ni kwa muda gani Askofu van Elst amesimamishwa kazi, ila iliongeza kuwa itategemea na kukamilika kwa uchunguzi, tathmini ya hali ya fedha ya jimbo na mambo mengine.
Wiki iliyopita, Askofu van Elst alisafiri hadi mjini Rome, Italia kwa ndege ya shirika la gharama nafuu, Ryanair kujieleza mbele ya Papa Francis – kutokana na madai kuwa alisafiri mwaka jana kwa ndege ya daraja la kwanza kwenda India na pia kutumia vibaya fedha.
Taarifa za matumizi hayo makubwa ya kiongozi huyo zimelitikisa Kanisa Katoliki la Ujerumani huku wengi wakitaka uwazi katika matumizi ya fedha -- mageuzi ambayo Papa Francis amekuwa akiyapigia kelele na kutaka kanisa maskini kwa watu maskini. Miradi hiyo kwa pamoja ambayo iliidhinishwa na mtangulizi wake awali ilikadiriwa kutumia Euro 5.5 milioni, lakini iliongezeka kwa kiasi cha kutisha na kufikia Euro 31 milioni ikiwamo bustani yenye thamani ya Euro 783,000.
Pia, Askofu Tebartz-van Elst anatuhumiwa kwa kutoa taarifa za uongo mahakamani kuhusu safari yake ya India kutembelea familia maskini.
Waendesha mashtaka wa Serikali wanaeleza kuwa askofu huyo alitoa taarifa za uongo chini ya kiapo kwenye mahakama ya mjini Hamburg dhidi ya gazeti la kila wiki, Der Spiegel akikana safari ya India anakodaiwa kutumia daraja la kwanza. Matumizi makubwa ya askofu huyo yameudhi walipa kodi wa Ujerumani wakidai kwamba wanakamuliwa huku fedha zikitumiwa vibaya na wengi wao kuandamana nje ya makazi ya askofu huyo.
Kansela Angela Merkel, binti wa kiongozi wa zamani wa Kipentekoste amesema kupitia msemaji wake, Steffen Seibert kwamba ana matumaini Kanisa Katoliki litamaliza tatizo hilo kwa jina la Yesu. Askofu Tebartz-van Elst hata hivyo ametetea miradi yote akieleza inalenga kudumisha mila na historia ya eneo hilo.
Tangu kuingia madarakani kwa Papa Francis, kumekuwa na kasi ya mabadiliko ndani ya kanisa.
Mwananchi.

Read More »

Cossy atupia picha ya kuonesha Matit* yake tena, huku akiwa na washiriki wa BBA.


Picha hiyo imepigwa Jumapili iliyopita maeneo ya Elegushi Beacha ambapo msanii huyo kutoka nchini Nigeria Alikuwa akila bata na washariki wa BBA The Chase Danrele pamoja na Bassey. Angalia kifua hicho Lol!!!!!!

Read More »

Mwanamke wa miaka 35, hajawahi kuwa na mwanaume wala hana hisia za mapenzi kwa jinsia yoyote



A 35-year-old woman has told how she has never felt sexually attracted to men or women.
Julie Sondra Decker from Tampa, Florida, revealed to MailOnline that she started describing herself as ‘nonsexual’ at the age of 15 and when she became aware of the term ‘asexual’, she changed it.
The outgoing blonde says that she’s had more offers of sex than she ‘wants to count’ over the years but, ‘without the feelings that usually go with that sort of thing, it’s kind of gross.’
Happy being single: Julie Sondra Decker, from Tampa, Florida, revealed to MailOnline that she started describing herself as ‘asexual’ at the age of 15 and has never been attracted to men or women
The writer, who lives alone in a two-bedroom apartment, states that she is not interested in dating or pursuing a domestic partner.
‘I have very close friendships but don’t want a significant other. I don’t want to find another asexual to be roommates with.
‘As far as I can tell I’ll be happy being single my whole life.’
In a YouTube video, Miss Decker says that as a young teenager she kissed and cuddled both boys and girls.

But she concluded: ‘I never found anything that floated my boat.’
She says that her family were convinced that she was a ‘closet lesbian’.
Before she went to college her mother even took her to the doctors because she wasn’t expressing ‘normal’ interest in the opposite sex.
Given the all-clear she carried on with her studies, graduating from the University of Florida in 2000 with a degree in elementary education and psychology.
She said despite there being more awareness about asexuality today, it still remains largely misunderstood.
She’s had male friends try and ‘fix’ her by kissing her against her will and many insist that she will ‘wake up one day’.
Since opening up about being asexual on the internet, via YouTube and her blog, Miss Decker says that she’s received death threats and been told by several commentators that she just needs a ‘good raping.’
‘When people hear that you’re asexual, some take that as a challenge,’ she told the Huffington Post.
‘We are perceived as not being fully human because sexual attraction and sexual relationships are seen as something alive, healthy people do.
‘They think that you really want sex but just don’t know it yet. For people who perform corrective rape, they believe that they’re just waking us up and that we’ll thank them for it later.’
Miss Decker says that asexuality presents itself in many forms. Some people, while lacking sexual attraction to any gender, may engage in purely romantic relationships.
However, she defines herself as ‘aromantic’, meaning she does not have any romantic feelings either.
Professor Bogaert, an associate professor at Brock University in Ontario, Canada, suggests in his book Understanding Asexuality, that around one per cent of the world’s population – 70million people – are ‘asexual.
He believes that this demographic are ‘under-studied’ and that they can feel excluded from our ‘very sexualised culture’.
Experts say a certain number of asexuals may have always existed but are only now starting to ‘come out’ as society becomes more liberal.
To her ‘haters’, Miss Decker concludes: ‘I’m not damaged, lonely or in need of a conversion because I’m not interested [in sex].’
She hopes to raise awareness about asexuality through her writing and public speaking.
‘[I want]  people who feel similarly to know they’re not alone.’

Source: Daily Mail

Read More »

Marekani yatuhumiwa kufuatilia kwa siri mawasiliano ya simu ya mkononi ya kansela wa Ujerumani.





Kwenye headlines za dunia sasa hivi miongoni mwa stori kubwa ni hii ya madai ya Ujerumani kwamba Marekani imekua ikifatilia kwa siri mazungumzo ya simu ya kiongozi wa Ujerumani,  Kansela Angela Merkel ambapo kwa mujibu wa DW Swahili, Ujerumani imemuita balozi wa Marekani nchini humo John B. Emerson kuzungumzia madai  hayo ya Idara ya usalama wa kitaifa ya Marekani kuyafatilia mawasiliano ya simu ya mkononi ya kansela.

Habari  hii  imekuja wakati Merkel na viongozi wengine wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kwa mkutano ambao unaonekana utagubikwa na habari za mawasiliano ya siri yanayodaiwa kufanywa na Marekani kwa washirika wake ambapo waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Thomas de Maiziere aliliambia shirika la habari la ARD  Ujerumani kwamba iwapo madai haya yatathibitishwa kuwa ya kweli basi litakuwa ni jambo baya sana.

De Maiziere amesema Marekani itabakia kuwa rafiki wa Ujerumani lakini jambo linalodaiwa kufanywa sio sahihi kabisa baada ya kupokea taarifa kwamba Marekani ilifatilia mawasiliano ya kansela Angela Merkel , hatua iliomfanya Merkel mwenyewe Jumatano kumpigia simu mara moja rais wa Marekani Barack Obama kutaka ufafanuzi zaidi kwa sababu aliamini kuna siku mawasiliano yake yatafatiliwa lakini sio na Marekani.


Baada ya haya madai ya Ujerumani, Marekani imekanusha kwa kusema haijayachunguza mawasiliano ya Kansela na haiwezi kufanya hivyo kamwe.

Haya madai yalitolewa kwa mara ya kwanza na mfanyakazi wa zamani wa idara ya kitaifa ya usalama nchini Marekani, NSA, Edward Snowden yaliyochapishwa na jarida la habari la Ujerumani, Der Spigel na sasa yameanza kuleta uhusiano mbaya kati ya Marekani na mataifa ya Ulaya yaliyokasirishwa na habari hizo za kufanyiwa uchunguzi wa siri na mshirika wao.


Mpaka usiku wa October 24 2013, taarifa mbalimbali ziliripoti kwamba mpaka sasa imefahamika ni viongozi wa  nchi 35 kubwa wameshafatiliwa kwenye mawasiliano yao ya simu za mkononi bila wenyewe kufahamu.



Read More »

Wastara Juma afichua siri.....Adai kioo kilimfanya amvulie nguo Sajuki


Wastara   amefichua  siri kwamba kioo ndicho kilisababisha aanzishe uhusiano wa mapenzi na marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki Januari 2, mwaka huu..
 
Wastara aliweka bayana kuwa marehemu Sajuki ambaye alikuwa mumewe, hakuwahi kumtongoza lakini kioo ndiyo kilikuwa chanzo kilichosababisha wajikute wameingia dhambini kwa mara ya kwanza.
 
Akizungumza na gpl, Wastara alisema kuwa siku hiyo walikuwa wakifanya mazoezi ya filamu moja (hakutaja jina) nyumbani kwake na Sajuki alikuwa muongozaji wa sinema hiyo.
 
“Ilikuwa ni usiku wa manane tukiwa nyumbani kwangu tukifanya mazoezi ya filamu moja, sasa ilikuwa ni scene ya mapenzi tukawa mbele ya kioo huku tumekumbatiana.
 
“Tukaendelea hivyoo, mmh! Sasa tulivyokitazama, tukahisi tunaendana. Tukaendelea kujifanyia tathmini na ghafla tukajikuta tunafanya kweli, kioo kilisababisha tukajikuta tunafanya mapenzi,” alisema Wastara kwa uso wa aibu..



Read More »

Baadhi ya Picha za kiwanda cha OK PLASTIC LTD kilipokuwa kikiwaka moto jana asubuhi




Jana majira ya saa 5 asubuhi, malighafi za kiwanda cha kutengeneza kandambili cha OK Plasctic Limited zimeteketezwa kwa moto na mtu ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

Kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuuzima moto huo lakini tayari malighafi nyingi zikiwa zimeshateketezwa kwa moto huo.


Aidha polisi walijitahidi kumsaka na kufanikiwa kumtia mbaroni ambapo mpaka sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.


Tazama  video  hapo  chini...




Read More »

Mwanafunzi wa kidato cha nne huko Iringa atandikwa viboko 100 na mwalimu baada ya kuiba simu....Kwa sasa yupo hoi hospitalini


Mwanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilayani Iringa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa madai ya kupigwa viboko zaidi ya 100 na mtu anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo na kufungiwa katika bweni kwa siku 3 ili kuificha siri hiyo.

Tukio hilo linakuja wakati harakati mbalimbali za kijamii na asasi za kiraia zikipiga kelele kupinga vitendo vya ukatili wakati jeshi la Polisi likianzisha dawati la jinsia kwa ajili ya kutokomeza masuala hayo.

Ni mwanafunzi Lusinde Nyaulingo, wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Idodi, ambaye anaugulia maumivu makali katika Hospitali hii ya rufaa ya mkoa wa Iringa, word namba tano ya majeruhi, kutokana na ukatili uliosababisha majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa maeneo ya mapaja, makalio na mgongo, baada ya kupigwa kwa tuhuma za kuchukua simu ya mwanafunzo mwenzie, jambo linalomfanya mwanafunzi huyu apoteze muda mwingi wa masomo wakati akipatiwa matibabu ili kurudisha afya yake.

Lusinde anasema baada ya kuangushiwa kipigo hicho kikali, kilichodumu kwa zaidi ya masaa tatatu, alipoteza fahamu na kisha kufungiwa katika bweni kwa siku tatu, huku wanafunzi wenzie wakipigwa marufuku kufikisha taarifa ya ugonjwa kwa wazazi wa Lusinde.

Hata hivyo jeshi la polisi kupitia kamanda wake mkoa wa Iringa ACP Athmani Mungi limesema  kuwa  wanafuatilia tukio hilo ili kuhakikisha haki inatendeka, kwa kumchukulia hatua za kisheria mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kumfikisha Mahakamani.




Read More »

Ziara wa Waziri Mkuu huko china imezidi kuzaa matunda....Leo wamesaini mikataba 7 ya shilingi trilioni 2.7


SERIKALI ya Tanzania leo imeingia mikataba saba na makampuni sita ya Kichina yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.7 (Sh. trilioni 2.72) ambazo zitawekezwa kwenye ujenzi wa miradi ya umeme na nyumba za makazi na biashara.

Makubaliano ya uwekezaji huo mkubwa yameshuhudiwa leo (Alhamisi, Oktoba 24, 2013)  na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wengine wa Serikali baada ya kusainiwa kwa mikataba saba ya uwekezaji katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Utiaji saini huo ulifanywa mara baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano la Uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na China (Tanzania China Business Forum) uliofanyika kwenye hoteli ya Dong Fang, jijini Guangzhou jimboni Guangdong, China. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Baraza la Biashara la China Afrika (China Africa Business Council-CABC) linashirikisha wafanyabiashara wa China na Tanzania.

Mikataba iliyosainiwa leo ni kati ya Shirika la Umeme (TANESCO) na Kampuni ya Tabiau Electric Apparatus Stock Co Ltd (TBEA) ambao ni kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme ya msongo mkubwa wa 400kV katika Gridi ya Taifa inayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini Mashariki hadi Arusha.

Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO, Bw. Felchesmi Mramba ndiye aliyesaini mkataba huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 692.7. Bw. Mramba pia alisaini mkataba mwingine na kampuni ya Shanghai Electric Power ambayo ndio itajenga mtambo wa Kinyerezi III.

Mkataba mwingine uliotiwa saini na Mramba ni kati ya Tanesco na kampuni ya China Gezhouba Group Corporation (CGGC) ambao wamekubali kuendeleza mradi wa umeme unaotokana na nguvu ya maji wa Rumakali ambao uko katika mikoa ya nyanda za juu kusini. Miradi hiyo miwili bado iko kwenye ngazi ya upembuzi yakinifu hivyo gharama zake bado hazijajulikana.

Kampuni ya Mkonge Energy Systems Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara wa Tanzania, Bw. Salum Shamte  ilitiliana saini mkataba na kampuni ya Sino Hyro Resources Ltd kwa ajili ya kuendeleza umeme wa nguvu za maji wa Masigira. Mradi huo unagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 136.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Nehemia Mchechu aliweka saini mkataba baina ya NHC na kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE) kwa ajili ya kuliwezesha kifedha shirika hilo liweze kujenga nyumba mbalimbali za makazi na biashara nchini. Mradi huo una thamani ya dola za Marekani milioni 500.

Bw. Mchechu pia aliwekeana saini mkataba mwingine na kampuni ya Poly Technologies  (POLY) wa kuwa na uhusiano kifedha na kiufundi kati ya kampuni hizo ya kichina na NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi na biashara  huko Masaki  wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Gharama za mradi huo ni dola za Marekani milioni 200.

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo (NDC) Bw. Gideon Nassari kwa niaba ya shirika lake aliingia mkataba na kampuni ya China ya Dalian International Economic & Technical Gooperation Group (CDIG) na Kampuni ya Hydro China Kunming Engineering Corporation kwa ajili ya kujenga kituo cha utafiti na mafunzo ya nishati mbadala. Mradi huo una thamani ya dola za Marekani milioni 136.

Mramba na Mchechu kwa nyakati tofauti walisema kwamba utekelezaji wa miradi hiyo utaanza wakati wowote kwani mambo mengi walishayakamilisha kwenye mazungumzo.

Wakati utambulisho, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bibi Julieth Kairuki alisema jumla ya Makampuni na Taasisi 46 zinazowekeza na kufanya biashara Tanzania zinashiriki katika Kongamano hilo ambapo  kwa upande wa China, CABC wameandikisha makampuni 44 yatakayoshiriki kwenye kongamano. Katika Kongamano hilo, TIC imewasilisha mada ya mazingira ya uwekezaji Tanzania na Bodi ya Utalii na Shirika la nyumba la Taifa wamewasilisha mada zinazohusu uwekezaji kwenye sekta ya Nyumba na fursa za utalii nchini Tanzania

Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya nane ya ziara yake ya kikazi kwa mwaliko wa Serikali ya China bado anaendelea na mikutano mbalimbali na leo usiku atazungumza na Watanzania waishio Guangzhou.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.


Read More »

Spika wa Bunge la Tanzania adai kuwa Mishahara ya wabunge ( Milioni 11 kwa mwezi ) ni midogo sana na ndo maana wanateseka wakistaafu





Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema mishahara ya wabunge wa Tanzania siyo mikubwa kulinganisha na wanayolipwa wabunge wa mabunge mengine duniani.

Makinda alitoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka ufafanuzi kuhusu kauli yake juu ya mpango wa Bunge wa kuwaokoa wabunge dhidi ya hali mbaya ya maisha, ambayo huwakabili wanapokuwa wamestaafu ubunge.

Kauli kuhusu mpango wa Bunge kuwaokoa wabunge wastaafu dhidi ya hali mbaya ya maisha, ambayo huwakabili, ilitolewa na Spika Makinda, wakati wa mazungumzo kati yake na Spika wa Bunge la Uswisi, Maya Graf, aliyetembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana.

Katika ufafanuzi wake, Spika Makinda aliitaja mishahara wanayolipwa wabunge katika orodha ya sababu zinazochangia hali mbaya ya maisha kuwakabili wabunge wanapostaafu ubunge.

Sababu mojawapo aliitaja kuwa ni mabadiliko ya malipo kwa wabunge baada ya kumaliza kipindi chao cha ubunge au kustaafu kazi hiyo, yaliyofanywa katika kipindi cha Bunge lililoshirikisha vyama vingi vya siasa nchini, kuanzia mwaka 1995.


Alisema katika kipindi chote cha Bunge lililokuwa na wabunge kutoka chama kimoja cha siasa (CCM), kulikuwa na utaratibu wa kuwalipa pensheni wabunge wanaostaafu ubunge.

Lakini alisema utaratibu huo uliondolewa baadaye baada ya Bunge la vyama vingi vya siasa kuanza mwaka 1995.


Alisema baada ya Bunge hilo kuanza, uliwekwa utaratibu mpya, ambao wabunge wanaomaliza kipindi chao cha ubunge au kustaafu kazi hiyo hulipwa kiinua mgongo au bahashishi (gratuity).


Alitaja sababu nyingine inayochangia wabunge wastaafu kukabiliwa na hali mbaya ya maisha kuwa ni mishahara midogo wanayolipwa wakati wakiwa kazini.


Alisema licha ya mishahara ya wabunge kutokuwa mikubwa kulinganisha na ile wanayolipwa wabunge wa mabunge mengine duniani, pia hutakiwa katika kile kidogo wanacholipwa wachangie majimboni.

“Mishahara yetu siyo mikubwa kama wenzetu, pia (mbunge) unatakiwa uchangie jimboni,” alisema Spika Makinda.

Wakati Spika Makinda akisema hayo, mbunge mmoja hulipwa mshahara wa Sh. milioni 11 kwa mwezi.


Hiyo ni mbali na posho ya Sh. 330,000 anayolipwa mbunge kwa kuhudhuria kikao kimoja kwa siku. Posho ni Sh. 80,000 za kujikimu akiwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao Sh. 200,000 kwa siku na mafuta ya gari Sh. 50,000, jumla kuwa Sh. 330,000 kwa siku.


Aidha, mbunge mmoja hulipwa ‘gratuity’ (kiinua mgongo au bahashishi) ya Sh. milioni 72 baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano cha ubunge.


Posho ya Sh. 330,000 anayolipwa mbunge kwa siku inazidi kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa serikali wa Sh. 150,000 kwa mwezi.


Aidha, wabunge hupewa fedha za Mfuko wa Jimbo Sh. milioni 30 kila mwaka kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo katika majimbo yao.


Serikali hadi sasa imeshindwa kuongeza kima cha chini kufikia Sh. 350,000 ambacho kilipendekezwa na Shirikisho Huru la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), hali ambayo imekuwa ikisababisha mivutano ya mara kwa mara kati yake na vyama vya wafanyakazi.


Kuhusu kuwaokoa wabunge dhidi ya hali mbaya ya maisha wanapostaafu, Spika Makinda alitangaza mpango maalumu wa Bunge wa kuwaokoa dhidi ya hali hiyo.


Alitangaza mpango huo wakati na baada ya mazungumzo kati yake na Spika wa Bunge la Uswisi, Graf jana na kusema Bunge lina mpango wa kuanza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wabunge.

Alisema lengo la mafunzo hiyo, ambayo yataanza wakati wowote ni kuwajengea uwezo wabunge ili watakapostaafu au vipindi vyao vya ubunge vitakapofikia ukomo wasitetereke kimaisha.

Makinda alisema mafunzo hayo yatatolewa wakati wowote na kwamba, programu hiyo itakuwa ya hiari kwa wabunge, hasa wenye kujishughulisha na biashara na shughuli nyinginezo.

Alisema ni vigumu kwa mbunge kuona hali mbaya ya maisha, ambayo huwakabili baadhi ya wabunge wanapokuwa wamestaafu ubunge.


Lakini alisema hali hiyo ameishuhudia mwenyewe baada ya kuchaguliwa kuwa Spika.

“Ukiona waliostaafu ubunge, wana hali mbaya sana, wengine wamekufa,” alisema Spika Makinda.

Alisema baada ya kukalia kiti cha Spika, baadhi ya wabunge wastaafu wamekuwa wakienda ofisini kwake (Spika) ‘kumlilia’ hali mbaya ya maisha na kuomba awasaidie.

Makinda alisema ofisi ya Spika haina bajeti, hivyo amekuwa akilazimika kutumia fedha kutoka mfukoni mwake kuwasaidia wastaafu hao wanaokwenda ofisini kwake ‘kumlilia’ shida za kimaisha.

Alisema kuna siku waliwahi kwenda ofisini kwake wabunge watano wastaafu kumlilia shida.

Lakini alisema kwa bahati mbaya siku hiyo aliweza kuwasaidia baadhi tu.

Alisema hali hiyo iliwafanya wale waliokosa msaada wake siku hiyo kuondoka, huku wakinung’unika.

Makinda alisema Bunge limefikiria kutoa mafunzo hayo kwa wabunge kwa sababu mbalimbali.

Mojawapo ni wabunge wengi wa sasa kuwa vijana na wengine wameingia bungeni wakiwa wametokea shuleni, hivyo wanaweza wasichaguliwe tena ubunge na hivyo, kukabiliwa na hali mbaya ya maisha.

“Ukishakuwa mbunge kazini huendi. Ndiyo maana tukafikiria kufundisha, hasa wabunge wenye biashara na shughuli nyinginezo,” alisema Spika Makinda na kuongeza:

“Tunataka mbunge awe na kazi, aingie bungeni. Ni nidhamu tunataka tuirudishe. Tunataka ifike mahali siasa isiwe ni kazi.”

Alisema athari ya kufanya siasa kuwa ni kazi, ni chaguzi kugeuzwa kuwa ni msimu wa watu kugombana.

“Ndiyo maana chaguzi zetu zimekuwa kama ugomvi, zinakuwa ni kufa na kupona. Tunataka isiwe nongwa,” alisema Makinda.


Naye Graf aliyekuja nchini kwa ziara binafsi, ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi inayofadhiliwa na nchi yake, katika mikoa ya Morogoro na Dodoma, aliunga mkono hoja ya Spika Makinda kuhusu mafunzo kutolewa kwa wabunge kwa kuwa hakuna uhakika kwa mbunge kuchaguliwa tena kushika nafasi hiyo.

CHANZO: NIPASHE


Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger