Polisi Nigeria wamtetea Bosi wao aliyekamatwa Ugoni.


Picha hiyo iliyosambaa katika mitandao mbali mbali ya kijamii nchini Nigeria inamuonesha Kamishna Msaidizi wa Polisi akiwa kamkumbatia na Kumminya Tit* binti mmoja.

Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinasema kwamba picha hiyo so ya kweli na kwamba wajanja wameitengeneza kupitia program za "photoshop" Ingawa kiukweli yaonekana picha hiyo ilipigwa na Binti huyo na wala si ya kutengeneza.

Maelezo yao haya hapa:-




Read More »

Criss Brown kwenda jela miaka 2


Taarifa kutoka Mtandao wa MTO zinasema msanii Criss Brown huenda akaenda jela miaka miwili na hukumu rasmi kutolewa Jumatatu ya leo.

Taarifa kutoka chanzo kinachoaaminikia na mtandao huo kimesema kuwa uamuzi umeshafikiwa na hukumu imeshaamuliwa, kilichobaki ni kumalizia taratibu za mwisho tu za tukio hilo. Si mwanasheria wa Criss au yeye mwenyewe anaweza kuzuia hukumu hiyo, labda Jaji abadilishe uamuzi wake, kitu ambacho hakitarajiwi.

Read More »

Dr. Mvungi avamiwa na majambazi na kucharangwa mapanga usiku




MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje  kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi aitwaye Dk. Natujwa Mvungi ameeleza kuwa baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani ambapo amepatiwa huduma ya kwanza kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baadaye alipelekwa kwenye wodi katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu.

Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.







Read More »

Bibi kizee mchawi adondoka wakati akiwanga, aambulia Mkong'oto Mkali toka kwa Wananchi


Bibi mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika amesadikika kudondoka kichawi maeneo ya Tabata Kinyerezi Kisiwani baada ya wenzake aliodai  kuwa nao kumuacha.

Bibi huyo ambaye amechezea kipigo toka kwa raia  waliomtuhumu  kuwa  ni mchawi , amedondoka asubuhi ya leo  katika maeneo hayo huku akionekana kutokuwa na kumbukumbu nzuri


Read More »

Huddah Monroe Amfagilia Wema kwa Diamond, awaponda wapita njia.....


 Mwakilishi huyo wa Kenya kwenye BBA mwaka huu, amefunguka kupitia Instagram kuwa anampenda Wema Sepetu na anamuona ndiye mwanamke wa kweli kwa Diamond Platnumz.
 Akiweka picha yake Wema, Huddah ameandika: I love her pants…..Too fresh @diamondplatnumz ,huyu Dame wako ,kipenzi chako.For life ,let nobody tell u otherwise.Hao wengine wapita njia tuu .God bless the two of u.RIP to her dad,I know how it feels to lose someone so dear to u.Take heart Ms Boss.I heart you.”

 Kauli hiyo ya Hudda imekaribisha mjadala mkubwa hasa kwa mashabiki wake wa Tanzania.



Read More »

Mbunge wa CCM mwenye miaka 60 aliyeolewa na kijana wa miaka 26 ajitetea na kudai kuwa kijana huyo ndo Alimng'ang'ania wafunge ndoa



Hatimaye Mbunge Rosweeter Kasikila (60), aliyefunga ndoa na kijana mwenye umri wa miaka 26, amefunguka kwa kusema aliyeng'ang'ania kufunga ndoa hiyo ni kijana mwenyewe licha ya kumtahadharisha tofauti ya umri wao.

Kasikila alitoa kauli hiyo jana, baada ya kutakiwa kujibu shutuma zilizotolewa na mumewe huyo, Michael Christian (26) ya kung'ang’ania vyeti vyake vya elimu kwa lengo la kumtaka arudi nyumbani.

Christian aliyefika katika ofisi za NIPASHE jana alitoa nakala ya barua aliyoituma kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuomba atumie uwezo wake wa kisheria ili mbunge huyo amrudishie vyeti vyake alinavyovishikilia.

Kufuatia maelezo hayo, NIPASHE ilimtafuta Dk. Nchimbi kwa njia ya simu ili athibitishe kupokea nakala ya barua hiyo lakini simu yake ilikuwa imezimwa.

Nakala nyingine za barua hiyo zilitumwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Binadamu kwa jamii-Madhehebu ya dini nchini, Askofu William Mwamalanga, Mchungaji wa Kanisa la Assembilies of God, Mikocheni B, Mchungaji Getrude Rwakatare na vyombo vya habari.

Akijibu shutuma hizo, mbunge huyo alisema hajawahi kung'ang'ania vyeti vya kijana huyo wala kulazimisha ndoa kama anavyodai Christian.

"Nahisi kuna watu wanamtumia ili wanichafue, siwezi kung'ang'ania vyeti, kwanza vya kazi gani kwangu, ukweli ni kwamba Michael, shida yake anataka nichafuliwe, kwangu aliondoka wakati sipo, sasa hivyo vyeti nimeving'ang'ania saa ngapi," alisema na kuongeza:

"Mwaka jana nikiwa Dodoma nilipata taarifa ameondoka nyumbani, kweli nilivyorudi nilikuta amechukua vitu vyake vyote kasoro tu vile nilivyomnunulia, hivyo vyeti anavyosema nimeving'ang'ania mbona hajawahi kutamka mbele yangu zaidi nimeona kwenye magazeti," alihoji.

Alisema baada ya kufika nyumbani alipata taarifa kuwa, mume wake huyo amepanga chumba na anaishi na mwanamke mwingine (askari) ambaye ni mjamzito.

Alisema utaratibu alioutumia kijana huyo wa kumchafua kwenye magazeti siyo sahihi na kumshauri angeenda mahakamani au kanisani kama aliona haitaki ndoa tena.

Aliongeza kuwa yeye na Christian walifahamiana mwaka 2009 baada ya kufiwa na mume wake aliyemtaja kwa jina moja la Mushi.

"Sikumtongoza kama anavyosema, alikuja katika hospitali ya Bagamoyo akitokea chuo cha Red Cross wakati huo nilikuwa Muuguzi Mkuu, aliponiona alinipenda alianza kunitongoza, nilimkatalia na kumwambia mimi ni mtu mzima sana kwake, " alisema na kuongeza:

"Alikuwa ananitumia email (barua pepe) za kunitaka, nilimwambia umri wangu ni mkubwa, lakini yeye alikuwa ananiambia kwenye vitabu vya dini kuna sehemu gani kumeandikwa umri," alisema.

Alisema alijikuta ametumbukia kwenye penzi la kijana huyo na kuanza mahusiano naye.

"Nina nakala zote za vidhibitisho ambavyo alikuwa akinitumia kunitongoza nimevichapisha kama vielelezo vyangu, tena wakati tumeanza uhusiano Taasisi ya Safina ambayo ilikuwa ikimsaidia katika masomo yake, ilinipigia simu," alisema na kuongeza:

"Safina walitaka kujua kama nina mahusiano na huyu kijana niliwajibu ni kweli, waliniambia kama ndiyo hivyo wanafuta kumsaidia kwa sababu wao huwasaidia wale ambao hawana uwezo, yatima, " alisema.

Alisema wakati taasisi hiyo ikimfuta, ilikuwa imemlipia Christian sehemu ya ada ya masomo aliyokuwa akiyachukua."

"Nililazimika kumlipia ada ya mwaka wa pili na watatu wa masomo yake pamoja na mambo mengine na ilifika kipindi aliniambia anataka kunioa, ndipo tulipofanya mchakato ambapo nilitolewa mahari na ndoa ilifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutangazwa mara tatu," alisema.

Alisema Christian alifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa mahari ya Sh. 200,000 na baada ya harusi alipelekwa Kondoa kwa ndugu wa kijana huyo.

"Huko tulienda kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka jana, tulifanyiwa sherehe za kimila na ndugu za mume wangu ambao ni baba mdogo, bibi mzaa baba yake na shangazi, pia ndugu zake wa Kimara na Dodoma wananijua, " alisema.

Hata hivyo, mbunge huyo alipoulizwa kama ndoa hiyo ipo sasa hasa kufuatia shutuma hizo, alisema hawezi kujua kwa sababu mume wake aliondoka bila kumuaga na kwa sasa anaishi na mwanamke mwingine toka Novemba mwaka jana.

Alisema wakati wa mahusiano yao wafanyakazi wenzake Christian walikuwa wakimhoji kwa nini ameamua kuwa na mtu mzima kama (mbunge), lakini yeye aliwajibu hakuna umri kwenye biblia.

Alipoulizwa kama ana mpango wa kuchukua hatua dhidi ya kijana huyo, mbunge huyo alisema hana mpango.

Mbunge huyo alijitetea kuwa, hakumlazimisha kufunga ndoa na kwamba wakati kijana huyo akimtongoza, alimweleza kuwa hawezi kuzaa kwa sababu umri wake umeshapita.  

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


Read More »

Binti wa Urusi Aiweka mnadani Bikira yake kwa Tsh Milioni 40


Binti huyu wa kirusi ameuza bikra yake kwa TShs Milioni 42. 
Mrembo huyo wa kiserbia anejulikana kwa  jina la Shatuniha alweka bikra yake kwenye mnada  na kujitambulisaha  kuwa ni  "mpya" (new) na "hajatumika" (not used)".
Shatuniha mwenye umri wa maika 18 alisema ana shida ya muhimu na haraka sana na pesa na ndo maana amefikia hatua ya kuuza kiungo chenye thamani katika mwili wake na kuongezea kuwa yuko tayari kukutana na mtu anetaka kununua bikra yake hiyo haraka iwezekanavyo akaongezea kwa kusema hata kesho, na yuko tayari kwenda na ushaidi wa kitaalam ili amhakikishe mteja wake huyo  kwamba kweli yeye ni bikra ili atolewe bikra hiyo na ili aptate hiyo pesa. Lakini alisisitiza malipo lazima iwe cash siyo cheque, card wala mkopo.
Baada ya watu wengi kujaribu kununua hatimaye mshindi akapatikana ambae ni Evgeniy Volnov  na aliinunua kwa hela za kirusi 900,000.00 ambazo ni sawa sawa na hela ya kiingerea eflu 17 na karibia milioni 42 za kitanzania.
Hapa ndipo mnada huo ulipokuwa unafnayika
Binti huyu alijielezea kwamba ni mtoto mzuri na hana tabia mbaya.
Kweli duniani kuna mambo tena ya ajabu sana na ndo waswahili walisema ukistaajabu ya Musa utaona ya.......

Read More »

P Squire Ndani ya Jumba la Kifahari, Samani za Dhahabu, walipokwenda msibani kwa mama wa Rais wa Nigeria.


Wanandugu wawili ambao ni mapacha Peter Okoye na Paul Okoye, leo hii wameushangaza ulimwengu mara baada ya picha zao wakiwa kwenye sebule na dinning room iliyonakshiwa na dhahabu kwenye samani zake kuzagaa mitandaoni huku zikisindikizwa na maneno yenye kujiamini ndani yake. 
3799cde443d611e3be7422000a9e0172_8
Maneno kama:-‘Goldenworld #blessed.’, ‘#2kings…… Work hard,play harder.’ na ‘A king in my own world…. #Blessed.’ yalitumika kusindikiza picha hizo wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti.
8300d71043da11e399e522000a9e28c4_8
7493d06843dc11e3a21b22000ae913ab_8
KENGETE

Read More »

Shehena ya Pembe 706 za Ndovu zakamatwa kwa Wachina Dar.


Siku moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.
Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.
Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung .
Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.
Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.
Mbali ya kushuhudia shehena ya pembe hizo, alionyeshwa gari maalumu aina ya Toyota Noah ambalo watuhumiwa hao hulitumia kutoa pembe porini na kuyaingiza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika eneo la tukio mara baada ya kuwakamata alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na matokeo ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imesitishwa na Serikali juzi baada ya wabunge kuilalamikia.
Waziri Kagasheki alisema kwamba katika harakati za kutaka kuwakamata watuhumiwa hao walitoa Sh30 milioni kwa ajili ya kujaribu kuwahonga askari.
“Walitaka kuwahonga askari ili wasikamatwe,” alisema huku akionyesha noti za fedha hizo.
Alisema wabunge wanaomtaka ajiuzulu kwa madai kwamba Operesheni Tokomeza Ujangili imesababisha mauaji ya watu na mifugo wanapoteza muda kwa kuwa mwenye mamlaka ya kumtoa ni Rais Jakaya Kikwete pekee.
“Sasa mimi nasema kunitoa haitakuwa rahisi anayeweza kunitoa ni yule aliyeniweka,” alisema.
Alisema ipo mikakati inayofanywa na baadhi ya wabunge kutaka kuwang’oa baadhi ya mawaziri kwa masilahi binafsi ya kisiasa.
“Itakuwa ni jambo la ajabu kwamba kila mtu akiingia madarakani wanataka atoke, watatolewa wangapi?” alihoji na kuongeza kuwa operesheni hiyo ni muhimu kwa ajili ya kunusuru tembo wasiishe.
Alisema kwamba ni kweli kuna baadhi ya dosari zimejitokeza kwenye operesheni ikiwamo kuuawa kwa baadhi ya mifugo, lakini siyo kwamba zoezi zima halina manufaa.
Kagasheki alisema kama kasi hii ya kuuawa kwa tembo itaachiwa iendelee baada ya miaka 10 tembo wote watakuwa wameisha nchini.
Alisema hataki kuona utawala wa Rais Kikwete ukiondoka madarakani ukiwa na lawama ya kuachia majangili wawamalize tembo.
Mmoja wa watuhumiwa hao, Huang Qin alisema shehena yote ya pembe za ndovu iliyokamatwa nyumbani kwake ilikuwa ikiletwa kidogo kidogo na rafiki yake ambaye hakumtaja jina.
Akiongea kwa Kiswahili Qin alisema: “Mimi hii si yangu, kichwa yangu mbovu. Rafiki yangu alileta hii (pembe) kidogo kidogo.”
Januari mwaka huu, Gazeti La Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba Serikali ya Kenya imekamata shehena ya vipande 638 vya pembe za ndovu ambavyo ni sawa tembo 320 waliouawa.
Mzigo huo wa tani mbili ulikuwa kwenye kontena la mawe ya urembo (marumaru) kutoka Tanzania.
Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa tani nne za pembe za ndovu zenye thamani ya Dola za Marekani 3.4 milioni sawa na takriban Sh5.4 bilioni zilikamatwa Hong Kong Oktoba 20, mwaka jana, huku ikielezwa kuwa meno hayo yalikamatwa yakisafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.
Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na pembe za ndovu yenye thamani ya Sh18.4 milioni yaliyotengenezwa kama bangili tayari kusafirisha kwenda nje ya nchi.

Mwananchi.

Read More »

Binti wa Miaka 14 ajiua, Aacha Ujumbe Mzito, Achoshwa na Masimango ya Shuleni na Mtandaoni.


Kwa nchi za kwetu Africa hili si jambo kubwa sana ila yawezekana siku za usoni likaleta athari pia kwetu kutokana na mambo ya utandawazi na vijana wengi kutaka kuiga na kufuata mienendo ya Maisha ya watu wa Ulaya na America.





Msichana anayeonekana pichani kwa jina anaitwa Izzy Dix, aliamua kujiua mnamo tarehe 17 September kutokana na kushinikizwa kwa kuitwa majina mabaya na kutengwa na wanafunzi wenzake shuleni, mtaani na hata aliporudi nyumbani hawakumuacha apumzike kwani waliendelea kumtumia sms za kumuita majina mabaya kupitia simu yake ya mkononi na kupitia Facebook.

Angalia Ujumbe huo chini aliouacha kabla ya kujiua.



Read More »

Bongo Movie Wasusia Msiba wa baba mzazi wa Wema Sepetu.....Wadai Wema Sepetu huwa hahudhurii misiba ya wenzie


HUKU akiwa na majonzi ya kuondo-kewa na baba yake mzazi, Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki dunia Jumapili iliyopita kwa ugonjwa wa kisukari, baadhi ya wasanii wanaounda Klabu ya Bongo Movie (muvi) Unity wanadaiwa  kuchekelea  kifo  hicho  na kumsusia msiba mwingizaji mwenzao, Wema Isaac Sepetu.

Habari kutoka chanzo chetu makini zilidai kuwa hoja dhaifu iliyotumiwa na wahusika hao ni kwamba Wema huwa haendi kwenye misiba ya wenzake hivyo naye amzike baba yake mwenyewe.


MFANO; MSIBA WA SAJUKI
Ulitolewa mfano wa msiba wa aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2, mwaka huu ambapo Wema alidaiwa alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.

Wapo waliokwenda mbele zaidi na kudai kuwa hata ukifunua madaftari yao wanapopatwa na misiba huwezi kukuta jina la Wema akiwa amesaini wala kufika.

SHARO, KANUMBA
“Kwa njia moja au nyingine, Wema bwana huwa hashiriki sana katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti pale Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo Milionea (Hussein Mkieti) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake.

“Wanadai mara nyingi amekuwa akijitenga na misiba ya wenzake na wala huwa hatoi hata pole kwa wafiwa kama wafanyavyo wengine wanaposhindwa kufika msibani kutokana na sababu mbalimbali hasa za kimajukumu au kuwa safarini,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:


“Kuna habari za chinichini kuwa walikaa kikao na kukubaliana kutohudhuria msiba wa Wema. Ilitengenezwa meseji ikatumwa kwa memba wote.”

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa kiongozi wa kundi hilo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa uhamasishaji watu wasiende msibani kwa kigezo cha Wema kutojumuika na watu wengine katika matatizo yao.


WEMA ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo ya kususiwa msiba wa baba yake Wema alisema: “Nimesikitishwa na kitendo hicho. Nahisi siyo sahihi kwa kuwa nimekuwa nikihudhuria misiba ya watu mbalimbali.

“Hawakuwa sahihi kunifanyia hivyo katika kipindi hiki kigumu, hata hivyo, wangekuja kwanza tumzike baba ndiyo nijifunze ila kutokuja kwao hakujanipunguzia chochote.”


Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni kama kumuongezea machozi mara mbili kwani tayari alikuwa na chozi la kuondokewa na baba yake kipenzi na la pili likawa ni kususiwa msiba.

Baada ya habari hizo kujaa tele, wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa wanaounda Bongo Muvi juu ya kumsusia msiba Wema ambapo kila mmoja alikuwa na utetezi wake;

Ray: Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba ya watu hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa kirefu.

Halima Yahya ‘Davina’: Sikwenda msibani kwa sababu na-shoot na nina mambo yangu ya kifamilia ila niliambiwa nisiende.

Steve Nyerere: Mi nilifiwa na mwanangu sikumuona Wema, tunaangalia kwenye kumbukumbu za wasanii wanaofariki dunia Wema hajawahi kuonekana. Mi’ naomba wasanii wapendane kikweli siyo kinafiki.

William Mtitu: Niko shooting wiki nzima ila kama Wema hakuonekana kwenye misiba ya watu hasa kwa Sajuki alikuwa anakosea sana. Pia alikosea kwa kuwakandia wasanii kwenye vyombo vya habari, kama walikosea angekaa nao akawaambia.

Kulwa Kikumba ‘Dude’: Nilikwenda msibani kutoa pole kwa sababu wale ni ndugu zangu lakini nilivyofiwa na mama yangu Wema hakuonekana wala hakunipa pole na huwa haonekani kwenye misiba ya wengine kama ilivyotokea kwa Sajuki ingawa mimi siwezi kulipa kisasi.

ZANZIBAR; DIAMOND NDANI
Kutoka visiwani Zanzibar alikozikwa baba Wema Jumatano iliyopita, ripota wetu alimshuhudia mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiungana na wasanii wengine waliokuwa bega kwa bega kumfariji mrembo huyo.

Habari za kina zilidai kwamba kwa kuwa Diamond hakufika kwenye msiba nyumbani kwa akina Wema, Sinza-Mori, Dar ilibidi aungane na mrembo huyo visiwani Zanzibar kwani naye amekuwa akimendewa na kashfa hiyo ya kuhudhuria misiba mikubwa na kupotezea ya watu wa kawaida.

Aidha, wasanii wengine walioamua kwenda msibani bila kujali onyo la kutokwenda ni pamoja na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Elizerbeth Michael ‘Lulu’, Kajala Masanja, Mahsein Awadhi ‘Dokta Cheni’, Salumu Mchoma ‘Chiki’ na Jaqueline Wolper.

Balozi Sepetu alifariki dunia Jumapili iliyopita baada ya kusumbuliwa na kisukari na kupooza ambapo juzi Jumatano alilazwa kwenye nyumba ya milele huko visiwani Zanzibar.

GPL




Read More »

Hukumu ya Agness Masogange yapingwa, Makamanda wasema ni ndogo sana ikilinganishwa na kosa lake.



MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.

Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.

WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.

“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.
                                                                     
WATAKA HUKUMU KWA NCHI WANACHAMA IWE MOJA
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.

“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.

MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.

Baadhi ya watu, wakiwemo marafiki zake wamekuwa wakisema kwa mkato staa huyo yupo Dar huku wengine wakisema baada ya kutua Dar alikwenda kwao Mbeya kwa sababu hataki kujulikana kuwa amesharudi Bongo.

Mwenyewe anapopatikana kwenye simu na kuulizwa amekuwa akijibu bado yupo Afrika Kusini lakini siku yoyote atatua Dar.

NZOWA ATOA UFAFANUZI
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusu mkutano huo alijibu kuwa yupo safarini kikazi akiwa katika mazingira mazuri atatoa ufafanuzi.

“Nipo safarini kikazi, naomba unitafute siku nyingine nitakupa ufafanuzi mzuri sana,” alisema Kamanda Nzowa ambaye naye ilidaiwa alikuwepo kwenye kikao hicho.

KUMBUKUMBU
Masogange na Mellisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg  nchini humo wakidaiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

Hata hivyo, mahakama kuu nchini humo ilidai madawa hayo si ya kulevya bali ni malighafi haramu iitwayo Ephedrine ambapo kwa sheria za Afrika Kusini mtu akipatikana na hatia ya kuyaingiza nchini humo ni kifungo cha miezi 32 jela au faini ya shilingi milioni 4.8 kama alivyohukumiwa Masogange ambayo ni ndogo.

GPL




Read More »

Minaj ndani ya Instagram Leo Leo



Haya Nick Minaj Karudi Tena kama Kawaida yake, ndani ya Instagram muda mchache uliopita, Mimi yangu macho, sitii neno.



Read More »

Angalia Keki ya Birthday ya Msanii Iyanya, ni Full Ngon*0.



Miongoni mwa wasanii kutoka nje waliopamba Tamasha la Fiest kwa pande za Dar es salaam ni msanii Iyanya Mbuk, juz ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa na katika kuonesha ni jinsi gani jamaa anapenda na kuhusudu "mambo" flani basi keki yake ilikuwa ni ujumbe tosha.

Read More »

Video ya Mdogo wa Diamond akisimulia enzi za Wizi, Pombe na Bangi za Diamond Platinumz




Unalikumbuka  sakata  la  dogo  S. Kide  anayejiita  mdogo  wake  Diamond? Ni dogo  ambaye  ameamua  kuyaanika  maisha  ya  Diamond  enzi  zile  akiwa  underground.....

Simulizi  lake  linaeleza  jinsi  Diamond  alivyokuwa  akishindia  vichupi  vilivyotoboka  nyuma  na  kuokota  makopo  dampo....

Dogo  anadai  kuwa, Diamond  ni  kaka  yake, ila  tofauti  zao  ni  Midomo  tu.

Tazama  video  hapo  chini





Read More »

MWANAMKE ALIYEPIGWA RISASI ARUSHA AMPA WAKATI MGUMU RPC WA ARUSHA


Toka jana jioni wakazi wa jiji la Arusha wameendelea kuwa katika taharuki na minong'ono hapa na pale kutokana na tukio la kupigwa risasi binti mmoja aitwaye Violeth Mathias katika ofisi za TRA Arusha.


Mwanadada huyu aliyeonesha jeuri ambayo haikutegemea si tu Arusha bali katika Taifa hili hasa lile la kwenda na kuchukua Bastola na kutaka kummaliza askari aliyekuwa akitimiza wajibu wake katika Bank ya CRDB. Kitendo hiki kimelfanya wakazi wa jiji hili kuwa na Maswali mengi kuliko majibu. Hasa juu ya anakota jeuri ama kiburi mwanadada huyu.


Viola alikwenda CRDB kuchukua pesa na kilichotokea yeye alipaki gari eneo lisiloruhusiwa kwa mazingira yale ya Bank. Hivyo askari Polisi alimfuata na kumwelekeza kwamba haruhusiwi kupaki gari eneo hilo ila yeye (Mwanadada) huyu hakutaka kusikiliza alichokuwa akiambiwa. Akashuka na kwenda bank ndani.


Hata hivyo Polisi alimfuata ndani ila cha kushanga mwanamke huyu akagoma tena. Ndipo Polisi kwa ajili ya usalama alirudi nje na kutoa upepo matairi yote ya gari kwa tahadhari. Cha kustaajabisha ni pale binti huyo aliporudi na kukuta hali hiyo alipoulizwa alijibiwa polisi ndiye aliyefanya hivyo. Alichofanya alienda kwenye gari lake na kutoka na bastola ati akitaka kumlenga yule askari polisi ndipo yule askari alipoaamu kujihami na kumshug begani.


Baada ya watu kuchunguza wakajua kuwa kiburi hicho anakitia kwa RC wa Arusha Bwa. Magesa Mulongo kwa kuwa anajipumzisha kwake. Wakazi wengi wa hapa wameshangazwa sana namna RC anavyozidi kuchafua nafasi yake hiyo na hata yule aliyempatia.


Cha kusikitisha zaidi ni RPC kuamua kukimbia waandishi wa habari baada ya waandishi kumfuata na kumtaka atoe maelezo juu ya hilo tukio. RPC kuona waandishi wa habari alimwamuru dereva kugeuza gari na kuondoka jambo lililopelekea waandishi wa habari kuamini kuwa RPC atakuwa amepokea maeleekezo toka kwa RC.


RPC alipopigiwa simu aliishia kusema anaelekea Hospitali kwa kuwa Sukari yake haiko sawa hili limepelekea kuaminika kuwa Mulongo anawaweka viongozi wenzie katika wakati mgumu kutokana na tabia zake hizi.

-Jamii Forums


Read More »

Mwizi wa Power Windows Adakwa Huko Sinza, Angalia Alivyochakaa na Kipigo.



MKAZI mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Jumanne iliyopita alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka kwa watu wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina ya Toyota Harrier, Ijumaa limeinyaka. 
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema Mbaga na wenzake wanne wanaodaiwa kuwa ni vinara wanaounda mtandao wa kuiba power window kwenye magari walifika eneo la tukio wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Noah.
Mbaga akisulubiwa na wananchi.
“Lengo lao lilikuwa ni kuiba kwenye gari la mteja wa Hospitali ya Marie Stop lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali hiyo,” alisema shuhuda huyo.
Gari aina ya Toyota Harrier walilotaka kuiba power window Mbaga na wenzake.
Shuhuda huyo alisema Mbaga na wenzake walifanikiwa kulitoboa gari hilo na kuchukua simu mbili pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.
Wananchi wakiwa wameandaa tairi tayari kumtia kiberiti Mbaga kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kumnusuru.
Inadaiwa watuhumiwa wengine walifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari walilofika nalo lakini mlinzi aliwahi kumng’ang’ania Mbaga na kuanguka naye chini.
Wakati mlinzi akipambana na Mbaga wananchi wenye hasira walifika eneo la tukio na walipopata maelezo walianza kumpa kichapo cha kufa mtu mtuhumiwa huyo wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.
Kipondo kikiwa kimepamba moto kwa Mbaga.
Wakati akipewa kichapo hicho, Mbaga alijitetea kwamba hakuwa mwizi bali ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu.
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.


Mbaga akiwa hoi baada ya kichapo.
Mbali na kusema hivyo, Mbaga alidai kwamba ameoa na mkewe anaitwa Fausani na kabla ya kufika hapo alikuwa na rafiki yake wakinywa pombe Mlimani City.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
“Nilikuwa nakunywa Pombe na Leonard pale Mlimani City, jamani naomba mnionee huruma, wale jamaa walinipa lifti tu,walikuwa wako wanne ila nawafahamu,” alisema Mbaga.

Polisi wakijaribu kuchukua maelezo ya mtuhumiwa baada ya kuwasili eneo la tukio. 

Polisi wakimbeba Mbaga kumpeleka kwenye difenda.
Mbaga aliokolewa na askari waliotokea na kumbeba msobemsobe hadi katika Kituo cha Polisi cha Mwananyamala.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.

Mbaga akiingizwa kwenye difenda. 

Safari ya kuelekea Mwananyamala ikaanza.

Read More »

Wacha Waendelee kukusanya hizo Sign, Siogopi kung'olewa.



Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hatishwi na mchakato wa kumng’oa katika nafasi yake ambao umeanzishwa na Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangalla kutokana na tuhuma za kukiuka kanuni za Bunge.

Kadhalika Spika Makinda amepuuza hoja za Dk Kigwangalla akisema kuwa yeye hajavunja kanuni yoyote, lakini akaweka bayana kuwa mbunge huyo wa Nzega ana haki kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kuendelea na kile anachokifanya.

“Kanuni si zinamruhusu, utaratibu upo kwenye kanuni za Bunge kwa hiyo aendelee na mchakato lakini mimi ninachosema sitetereki maana hakuna kanuni yoyote ambayo nimeivunja,” alisema Makinda katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake jana.

Wakati Spika akitoa kauli hiyo, jana, Dk Kigwangalla alianza harakati zake za kukusanya saini za wabunge, akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani naye kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni.

Miongoni mwa madai ya Dk Kigwangalla ni hatua ya Makinda kufanya uteuzi wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na kanuni zinazotaja wenyeviti kuchaguliwa na wajumbe wa kamati.

Hoja nyingine ni kamati hiyo ya bajeti kulipwa posho ya Sh430,000 wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000 pamoja na kumteua Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba kuingia katika kamati hiyo ya bajeti wakati mbunge huyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu.

Jana Dk Kigwangalla aliwasilisha hoja yake kwa Katibu wa Bunge na kuongeza madai mapya yakiwamo ya kuagiza kwa mabavu majedwali ya mabadiliko ya sheria kwenda kwenye kamati ya bajeti, kuvunja masharti ya kanuni ya 48 inayotoa maelekezo ya namna ya kuwasilisha na kujadili jambo la dharura na kutumia madaraka yake vibaya kwa kuvunja masharti ya Sheria ya The National Assembly (Administration) Act (Cap.115) ya mwaka 2008.

Makinda akijibu hoja hizo jana alisema alifanya uteuzi wa Chenge kuongoza Kamati ya Bajeti kwa sababu kamati hiyo ni mpya na haikuwapo katika kamati za awali, hivyo ni wazo ambalo lilitokana na mawazo ya Bunge la sasa.

“Tulikuwa tunafikiria jinsi Bunge linavyoweza kuisadia Serikali ipate vyanzo vipya vya mapato. Kwa hiyo tumehitimisha wazo hili kwa kuamua kuwa na Kamati ya Bajeti. Kamati hii haikuwapo na wala utaratibu wake wa kikanuni haukuwapo. Niliamua na kanuni zinanipa uwezo huo kwamba niteue mtu ambaye ninaamini anaweza kuisimamia katika hatua za mwanzo ili tuone uzoefu utatufikisha wapi,” alisema Makinda na kuongeza:

“Kamati hii hata Serikali ilikuwa haikubaliani na sisi, lakini katika muda mfupi wa utendaji wake umefanya kazi kubwa na kama tusingekuwa na Mzee Chenge ambaye ni mzoefu na anafahamu vizuri utendaji wa Serikali basi tungeshindwa na mimi siko tayari kuanzisha kitu halafu nikashindwa”.

Kuhusu posho, Spika aliungana na kauli ya Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah kwamba si wakati wote Kamati ya Bajeti imekuwa ikipewa malipo zaidi, bali ni pale tu wanapofanya kazi nje ya siku na saa za kazi tena kwa kibali chake.

“Lazima walete maombi na waeleze kwa nini wanapaswa kufanya kazi kwa muda wa ziada au siku za mapumziko na mimi nikisharidhia basi wanalipwa mara mbili ya viwango vya kawaida na hiyo ni kwa mujibu wa taratibu na Kanuni zetu,” alisema.

Read More »

Simba Wakwaa Kisiki, Mashabiki wafanya fujo kubwa.




MBIO za Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara zinazidi kuwa ngumu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar jana, lakini habari mbaya zaidi ni kuwa mashabiki wa timu hiyo walijeruhiwa kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mechi hiyo.
Vurugu hizo zilitokea katika mechi hiyo ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya Kagera kusawazisha bao katika dakika ya 95 kutokana na mkwaju wa penalti uliopigwa na Salum Kanoni, mara baada ya beki wa Simba, Joseph Owino kumchezea vibaya Daudi Jumanne.

Mara baada ya bao hilo la kusawazisha, mashabiki wa Simba walianza kuvunja viti, kitendo kilichosababisha askari wa kutuliza ghasia kurusha mabomu mawili ya machozi kwenye jukwaa la mashabiki hao, ndipo mtifuano ukawa mkubwa.
Tukio hilo lilitokea sekunde chache kabla ya mwamuzi wa kati, Mohamed Theofile wa Morogoro kumaliza mchezo huo, ambapo askari waliendelea kurusha mabomu kadhaa.

Gazeti hili lilishuhudia viti zaidi ya 50 vikiwa vimevunjwa na kuzagaa, huku baadhi ya mashabiki wakiumia na wawili kupoteza fahamu, huku wachezaji wakitoka mbio kuelekea vyumbani mara baada ya kipenga cha mwisho.
Mmoja wa mashabiki aliyepoteza fahamu ni wa Simba aliyetambulika kwa jina la Fii Kambi, ambaye hali yake ilikuwa mbaya lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa Msalaba Mwekundu, alirejewa na fahamu, lakini mpaka gazeti hili linaondoka uwanjani hapo, alikuwa bado hajarejea katika hali yake ya kawaida.

Akizungumzia juu ya kilichotokea uwanjani hapo, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, alisema:

“Tumeingiwa na hofu na yawezekana tunatengenezewa mazingira magumu ya kutwaa ubingwa kutokana na kuonewa.”
Upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope, alisema: “Asilimia kubwa ni matatizo ya waamuzi wetu wa Tanzania, aliongeza muda mwingi wakati dakika zilikuwa zimemalizika.”

Naye nahodha wa Simba, Said Nassoro ‘Chollo’ naye alisema: “Kitendo cha mabomu kulipuliwa wakati tukiwa uwanjani mechi ikiendelea ni jambo baya na wanatakiwa kulichukulia hatua kali.”

Katika mechi hiyo Simba ndiyo ilianza kupata bao katika dakika ya 45 kupitia kwa Amissi Tambwe ambaye ameendelea kuwa kinara wa mabao kwa kufikisha mabao tisa na kumzidi Hamis Kiiza wa Yanga mwenye mabao nane.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni, akisema: “Naishauri TFF mpya iangalie juu ya suala la waamuzi kwa kuwa wao ndiyo tatizo.”

Upande wa Kocha wa Kagera, Jackson Mayanja, alisema: “Mwamuzi alifanya kazi inavyotakiwa kwa kuwa aliona mchezaji alifanyiwa faulo, ndiyo maana akatoa penalti halali.”

Kituko katika mchezo huo, ni mashabiki wa Simba kushangilia uamuzi wa Abel Dhaira kuwekwa benchi katika mechi, badala yake langoni akasimama Abuu Hashim ambaye alidaka dakika zote 90.

gpl


Read More »

BABU SEYA, PAPII KOCHA WAPATA MATUMAINI YA KURUDI URAIANI


MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ pamoja na ndugu zao, Jumatano iliyopita walitoka kwa vicheko katika Mahakama ya Rufaa Tanzania baada ya kuridhishwa na utetezi uliotolewa na wakili wao, Mabere Marando, anayepinga hukumu ya kifungo cha maisha jela, waliyopewa wanamuziki hao.

Mbele ya majaji watatu wa Mahakama hiyo, Marando alikabiliana na timu ya mawakili watano waandamizi wa serikali ambao ni Jackson Brashi, Angaza Mwaipopo, Imaculate Banzi, Joseph Pande na Apimark Mabruk.

Miongoni mwa hoja ambazo Marando alionekana kuwabana mawakili wa serikali ni jinsi Jamhuri ilivyowatia hatiani wateja wake kwa kutumia ushahidi uliotolewa na watoto katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar, akisema zipo taratibu za kuchukua katika ushahidi kwa mtoto ikiwemo kurekodiwa, jambo ambalo halikufanyika.

Marando alizidi kuweka wazi kuwa katika ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ulionesha nyumba iliyodaiwa kufanyiwa uhalifu huo ilikuwa na mlango wa siri uliotumiwa na watoto hao kupenya hadi ndani pasipo kuonekana jambo ambalo baadaye lilidhihirika si kweli kwani nyumba hiyo haikuwa na mlango mwingine zaidi ya wa uani na barazani.

Hata hivyo, jopo la mawakili wa Jamhuri licha ya kukumbana na wakati mgumu kutoka kwa wakili Marando, liliendelea kusisitiza kuwa hukumu iliyotolewa dhidi ya washitakiwa hao ilikuwa sahihi.

Baada ya mawakili hao kusisitiza hivyo Marando alipewa nafasi nyingine ya kutoa utetezi wake, ambapo aliendelea kufafanua makosa mbalimbali yaliyofanyika kuwahukumu wateja wake kwa kutaja vifungu vya sheria ambavyo vilionekana kama kuwasafishia njia wateja wake hao hali iliyozua tabasamu na vicheko mahakamani hapo.

Baada ya kupitia marejeo ya kesi hiyo kwa pande hizo mbili, jopo la majaji akiwemo, Salum Masatti liliahirisha kesi hiyo na kusema litapanga siku ya hukumu huku wafungwa hao wakirejeshwa gerezani wakiwa na vicheko vya furaha huku ndugu na jamaa nao wakikumbatiana kwa shangwe.

GPL

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger