Mtoto Azaliwa Bila Macho huku Akiwa na Jinsia Mbili Huko Tunduru




Mganga mfawidhi wa Hospitali ta Wilaya ya Tunduru Dkt. Joseph Ng'ombo akimuangalia mtoto huyo aliyezaliwa akiwa hana macho, pua na Shavu linalo shika mdomo wa juu, kushoto ni mkunga wa zamu katika Hospital hiyo Rukia Nguo akiwa akiwa amekishika kichanga

 Huu ndiyo muunekano wa kichanga hiki usoni.
Mkono wa mkunga huyo ukionyesha maungo ya kichanga hicho kilichozaliwa kikiwa na sehemu nyeti mbili ikiwepo ya kiume kwa juu na ya kike kwa chini.


Na Steven Augustino, Tunduru
MAJONZI na Simanzi zilitawala kwa wanafamilia na Wauguzi katika hosipitali ya Wilaya ya Tunduru baada ya ndugu yao mkazi wa Kijiji cha Kadewele Mjini hapa aliyetambuliwa kwa jina la Rehema Safi (42) kujifungua Mtoto wa ajabu mbaye pamoja miongoni mwa maajabu hayo nipamoja na kuzaliwa akiwa na Jinsia Mbili.

Aidha Kichanga hicho ambacho kimezaliwa kikiwa na uzito wa kilo 1.8 pia kimezaliwa kikiwa hakina Pua,macho na Shavu ambalo hushikilia mdomo wa juu.  

Tukio hilo ambalo lilisababisha mshtuko na taaharuki kwa wataalamu wanaotoa huduma ya kiafya limetokea katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Agosti 5 mwaka huu.

Mkunga wa zamu katika Wodi ya wazazi iliyopo katika hospitali hiyo Rukia Nguo alisema kuwa pamoja na uzowefu wake wa muda mrefu katika kada hiyo hajawahi kuona kiumbe cha aina hiyo.

Alisema baada ya tukio alilazimika kuwaita waganga na wauguzi wenzake ili wamsaidie kutazama kichanga hicho ili kujiridhisha juu ya tukio hilo akidai kuwa awali akiwa peke yake akishindwa kukitambua kiumbe hicho kama ni binabamu ama la ingawa kilionekana kuwa na viungo vingine vya kibinadamu.

Kufuatia hali hiyo Mkunga huyo akatoa wito kwa wanawake wenzake kuachana na tabia ya kutumia dawa za kienyeji na badala yake waende hospital kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa tabibu.
“unajua sisi wanawake wengi tumekuwa na tabia ya kuchukua na kuanza kuzitumia dawa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki “ alisema Nguo na kuongeza kuwa matumizi ya dawa za aina hiyo zinaweza kusababisha madhara makubwa yakiwemo yanayo sababisha kuzaliwa kwa watoto wenye upungufu wa viungo.    

Akizungumza kwa unyonge juu ya tukio hilo mama mzazi wa Mtoto hoyo ambaye hadi sasa hajapatiwa jina, Reheme Safi ambaye uzazi huo ni wa tano alisema kuwa hana budi kulipokea tukio hilo kama changamoto ya maisha kwani mtoaji nimungu na kwa hatua hiyo hawezi kubishana na uumbaji huo.

  ukilinganisha na tukio la Kutunza mimba ya Mtoto kwa Miezi 9 huku ukiwa na matumaini ya kupata mtoto atakaye kusaidia maishani,sijisikii vizuri kupata Mtoto wa aina hii lakini sinanjia ya kuyabadilisha matokeo hayo “ alisema Reheme na kuongeza kuwa yeye anamuachia mungu juu uumbaji huo.

Akizungumzia histolia ya jinsi ulivyo patikana ujauzito huo alisema kuwa kwanza yeye hakutarajia kuupata kwavile kwa zaidi ya miaka miwli alikuwa akitumia Dawa za uzazi wa Mpango aina ya (DEPO PROVELA) ya sindano ambayo wanawake wengi wanaopanga uzazi huitumia kwa kuchoma sindao moja kila baada ya miezi mitatu.

Alisema akiwa katika hali hiyo ghafla alishangaa kuona tumbo lake linakuwa zito na baadae kitu kikaanza kucheza tumboni na alipokwenda hospitali na kupimwa alishangaa kuelezwa kuwa huo ni ujauzito na kinachocheza ni Mtoto.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya serikali ya Wilaya ya Dkt. Joseph Ng’omboa amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa maafisa tabibu wanaendelea kufanya utafiti wa chanzo cha tukio hilo kwa kumpima mama huyo kama ana magonjwa ya kuambukiza ama la.

Alisema mtoto kuzaliwa akiwa katika hali hiyo kunaweza kusababishwa na mambo mengi yakiwemo magonjwa ya zinaa, kukosekana kwa virutubisho Fulani wakati wa uumbwaji wa viungo mwilini ama mama mzazi kutumia madawa wakati akiwa na mimba changa.

Aidha Dkt. Ng’ombo pia akatumia nafasi hiyo kuwahamasisha akina mama wajawazito kuhudhulia Kliniki katika kipindi chote baada ya kupata ujauzito na kwenda kujifungulia hospitali kwa ajili ya kupata msaada wa maafisa tabibu wakati wote.  
Mwisho


Source: Demasho News Blog

Read More »

Baada ya Ukimya wa zaidi ya Miaka 10, Mkanda wa Uhusiano wa Kimapenzi wa Clinton na Monica Lewinsky Wavuja.


Mkanda ambao unaonesha Meseji za kimahaba ambazo Monica Lewensky alikuwa akimtumia Rais wa Marekani wa kipindi hicho, Bill Clinton Umeibuka baada ya miaka 15 kupita huku ikisemekana ya kwamba miongoni mwa waliotakiwa kuufuta ushahidi huo, walitoa nakala nyingine. Yafuatayo ni baadi ya Maneno yanayopatikana ambayo Monica alikuwa akimtumiwa mheshima president.


  • “I could take my clothes off and start … well … I know you wouldn’t enjoy that? I hope to see you later and I hope you will follow my script and do what I want.”
  • “Since I know you will be alone tomorrow evening, I have two proposals for you, neither of which is you not seeing me.”
  • “Now the first thing that has to happen is that you need to pre-plan with Betty [Currie, Clinton's secretary] that you will leave the office at, I don’t know, at 7, 7:30 so that everyone else who hates me that causes me lots of trouble goes home.”
  • “Then you quickly sneak back and then in the meantime I quickly sneak over and then we can have a nice little visit for, you know, 15 minutes or half an hour. Whatever you want.”
  • “Maybe we could go over and watch a movie together and just have kind of, I don’t know, boxed dinners or something like that.”
  • “And then that way we don’t have to deal with the problem of me … of there being a record of me going upstairs and we can spend some time together and see a good movie.”
  • “So I don’t know, those are two proposals and you can’t refuse me because I’m too cute and adorable and soon I won’t be here anymore to pop over.”
  • “I’m hoping you will hear this and you will choose which one you want to do and go tell Betty and then she can call me and let me know so I don’t have to stress out all day and I don’t have to call her every two hours and bug her because — I know you will find this very hard to believe — but I can be a pain in the ass sometimes.”
 Unaonaje hapo?

Read More »

Mwanamke Almanusura Amuue Mp3nz! wake baada ya kumbana Mwanaume huyo katikati ya maziwa wakati wanafanya Mapenzi.


Mahakama Moja Huko Ujermani ilikuwa na kazi ya kusikiliza kesi ya malalamiko kutoka kwa mwanaume ya kutaka kuuliwa na mpenzi wake.

Tim Schmidt,30, amesema Mpenzi wake Franziska Hassen,33, alijaribu kumuua wakati wakifanya map3nz kwa kumkandamiza kupitia maz!wa yake makubwa.

Kwa Upande wake, Franziska amekana madai hayo na kusema yote hayo yalikuwa ni manjopnjo tu katika kupeana maraha sema mpnz wake huyo ametafsiri tofauti.

Schmidt amesema siku ya tukio alikuwa amekaa huku akiwa anambusu mpnz wake huyo na ndipo alipo mvuta kichwa chake na kukipachika kati ya maz!wa hayo na kumshikilia kwa nguvu kwa sekunde kadhaa, Alikosa Pumzi kiasi kilichomfanya aanze kuwa wa Blue.

Alipofanikiwa kujitoa alikimbia akiwa uchi hadi kwa jirani ambaye alimpa nguo za kujisitiri na kumshauri awapigie polisi.

Read More »

Mmh, Angalia 10 Hot Photos za Super Model Mika Shay



Msichana huyo ambaye ni Model ana Mvuto wa Ndani na nje, ni Mwanamke ambaye binafsi naimani kila mwanaume ana wish awe mke au awe mtu wake angalia hizo Photos halafu uniambie unaonaje. 
Mika Shay eewMika Shay treMika Shay 54Mika Shay r4Mika Shay tttMika Shay 55Mika Shay 5Mika ShayMika Shay
PHOTOSHOW- Model Mika Shay
Model Mika Shay

Read More »

Mfanya Biashara wa Madini Apigwa Risasi na Kuuliwa baada ya Kutokea "Mtobozano"


Na Mwandishi Wetu, Arusha
JIJI la Arusha na Mkoa wa Manyara, hali ya hewa ilishachafuka, wingu zito limefunika kufuatia kuuawa kwa kupigwa risasi, mfanyakazi wa Kampuni ya Tanzanite One, Onesmo William Mushi.
Marehemu Onesmo William Mushi enzi za uhai wake.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ni bilionea wa madini, mkazi wa Arusha, Joseph Mwakipesile ‘Chusa’ ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki migodi, Mererani wilayani Simanjiro, Manyara.
Mtuhumiwa wa mauaji, Joseph Mwakipesile ‘Chusa’.
ONESMO ALIVYOUAWA
Habari zimedai kwamba Onesmo akiwa eneo lake la kazi, mgodini chini, alipigwa risasi mbili kifuani ambazo ziliondoa uhai wake.
Tukio hilo lilitokea saa 8 usiku, Julai 20, mwaka huu, chanzo kikitajwa kwamba ni mgogoro wa kugombea madini.
Imedaiwa kuwa Onesmo, akiwa na wafanyakazi wenzake wa Tanzanite One ambao wamefahamika kwa jina mojamoja, Kennedy na Leonard, walikutana na wachimbaji wadogowadogo hivyo kutokea mvutano wa kimaslahi.
Habari zimedai kwamba miongoni mwa wachimbaji hao wadogo, alikuwepo Chusa ambaye ndiye anadaiwa kufanya mashambulizi dhidi ya Onesmo.
Wafanyakazi wa Tanzanite One wakiwa na mabango.
FAMILIA YALIA KUMPOTEZA ONESMO
Julai 25, mwaka huu, Onesmo alizikwa kijijini kwao, Uswaa, Machame, Hai, Kilimanjaro hivyo kuhitimisha safari yake hapa duniani.
Vilio na huzuni vilitanda kipindi chote cha mazishi ya Onesmo, huku sikitiko kubwa likielekea kwa mjane wa marehemu ambaye ameachiwa watoto wawili ambao atawalea bila baba.
Mke wa marehemu, watoto wake na ndugu wengine walikuwa wanyonge muda wote wa mazishi, kuonesha namna walivyoguswa na kifo hicho.
MERERANI YATIKISIKA
Wiki moja baada ya Onesmo kuuawa, wafanyakazi wa Tanzanite One wapatao 200, walilitikisa eneo la Mererani na kusimamisha shughuli zote za uchimbaji madini mpaka wapate tamko la serikali.
Kishindo cha wafanyakazi hao kilisababisha shughuli kusimama hata katika migodi ya wachimbaji wadogo, kwani hasira zilikuwa kali mno.
Awali, wafanyakazi wa Tanzanite One waligoma kufanya kazi wakiitaka menejimenti ya kampuni hiyo kufuatilia haki zote, ikiwemo mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa na kufikishwa kortini.
Baadaye, wafanyakazi hao walikusanyika na mabango kisha kushinikiza sheria kuchukua mkondo wake, vilevile wakaituhumu serikali kufumbia macho suala hilo.
Aidha, wafanyakazi hao walibeba mabango yenye ujumbe ambao uliwatuhumu moja kwa moja baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi pamoja na wale wa madini Kanda ya Kaskazini kwamba hawaaminiki katika kutenda haki.
MIGODI YAFUNGWA
Kutokana na kifo cha Onesmo, Wizara ya Nishati na Madini, imeifunga kwa muda migodi minne inayozunguka eneo la mgodi wa Kampuni ya Tanzanite One ili kusafisha hali ya hewa iliyochafuka.
Wizara imefanya hivyo kufuatia malalamiko ya wafanyakazi wa Tanzanite One kwamba kifo cha Onesmo kimesababishwa na serikali kulea mgogoro wa mipaka kwa muda mrefu.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Benjamini Mchwampaka, alisema kuwa migodi iliyofungwa ni ile inayomilikiwa na wafanyabiashara Joseph Mwakipesile ‘Chusa’, Jackson Simon, Abdulhakim Mula pamoja na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Maning’oo.
SERIKALI YACHUKUA HATUA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Akili Mpwapwa, aliliambia gazeti hili kuwa Chusa alikamatwa yapata wiki mbili zilizopita, baada ya jeshi lake kujiridhisha na tuhuma dhidi yake.
“Tuliona tuhuma dhidi yake zina nguvu ndiyo maana tukamkamata,” alisema Mpwapwa na kuongeza: “Siku tatu zilizopita (kutoka Jumapili iliyopita), alifikishwa mahakamani, akasomewa mashtaka kwa mara ya kwanza na sasa hivi yupo gerezani.
“Sijajua atarudishwa lini mahakamani lakini hii ninayokupa ni taarifa ya uhakika kwamba huyo bwana yupo gerezani. Tulimkamata na kumfikisha mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji, siyo kwa ajili ya kuisaidia polisi.”
TATIZO LA MGOGORO
Kwa mujibu wa taarifa za Mererani, mgogoro wa mipaka kati ya wachimbaji wadogo na Kampuni ya Tanzanite One ni wa muda mrefu.
Imeelezwa kwamba mara kwa mara, wafanyakazi wa kampuni hiyo wamekuwa wakikutana na wachimbaji wadogo mgodini chini, hivyo kuibua mvutano.
Kitendo cha wachimbaji wadogo kukutana mgodini chini na wafanyakazi wa Tanzanite One, kinajulikana kama Mtobozano.
Kwa upande mwingine, imekuwa ikidaiwa kuwa Mtobozano ni lugha ya kulainisha mambo, kwani ukweli ni kwamba ni kitendo cha wachimbaji wadogo kuvamia mgodi wa Tanzanite One na kupora madini.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki migodi Mererani, hujipatia fedha haramu, kwa kuiba madini ya tanzanite katika migodi ya Tanzanite One.
Kufuatia hali hiyo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Uswaa Machame, Robinson Manga, alisema wakati wa ibada ya mazishi ya Onesmo kwamba lazima serikali itafute ufumbuzi wa kudumu kuhusiana na mipaka Mererani.
Mchungaji Manga alisema: “Tatizo la migogoro kati ya wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite na wawekezaji wakubwa limekuwa la miaka mingi, serikali inatakiwa kuangalia upya mipaka na kupata ufumbuzi wa kudumu.”

Source GAZETI LA UWAZI (GPL)

Read More »

Video ya Jambazi Lilloinusurika Kuuliwa na Raia wenye Hasira Huko Mbezi Dar Es Salaam



KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam. 


Kijana huyo pamoja na mwenzake wakitumia pikipiki walikuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati na kuanza kupambana nao. 



Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo kutokana na majibizano ya risasi kati yake na polisi. 


Baada ya jambazi lililokuwa linaendesha pikipiki kuona mwenzake anaelekea kukamatwa lilitokomea wakati mwenzake akiangukia mikononi mwa wananchi wenye hasira kali waliomshushia kipondo cha nguvu.

TAZAMA  VIDEO  HAPO  CHINI....


Source: Mpekuz

Read More »

Msichana Mwingine Auliwa, Face Book yamponza

;">

Wito umetolewa kwa watoto wa kike kupunguza kwenda sehemu kukutana na watu wasiowafahamu au kwa kuwajua kwa uchache kupitia mitandao ya kijamii, hususan Face book ili kuepuka madhara ambayo siku za hivi karibuni yamekuwa yakiwakuta wengi.

Mwanafunzi huyo wa Shahada ya Sheria kutoka Abuja amefikwa na Umauti baada ya kula kinachosadikiwa kuwa sumu. Imeelezwa kuwa binti huyo alitoka chuoni na akamuaga room mate wake kwamba anakwenda kukutana na jamaa ambaye walikuwa wana chat kupitia face book, ingawa alikatazwa lakini aliamua kwenda tu.

Asubuhi yake ndo mwili ukagundulika ukiwa umetelekezwa barabarani.


Read More »

Kutana na Tom Staniford, Mgonjwa wa Utapiamlo Aliejikubali na KUishi kawada, naye apata Mpenzi.


Tom Staniford, 24 ni mzaliwa wa Uingereza Anayesumbuliwa na Matatizo ya Utapiamlo kwa Steji ya Pili. Kutokana tatizo hilo Mwili wa Tom Hauruhusu kuhifadhi Mafuta katika sehemu za ngozi yake hususan ya Usoni na Mikononi na Miguuni.

Tom Ambaye amejitoa kutimiza ndoto zake za kuwa Bingwa wa Kimataifa wa Mbio za Baiskeli anaishi Maisha ya Kawaida ingawa kuna kipindi watu humshangaa kutokana na hali yake lakini yeye halijali hilo. Mwili wake una Asilimia 40 tu ya misuli na nyma za mwanadamu wa kawaida.

Tom amekuwa akisumbuliwa na magonjwa nyemelezi kutokana na hali yake ambapo mpaka sasa an Kisukari cha aina 2 tofauti na pia uwezo wake wa kusikia ni mdogo mno hivyo yamlazimu aweke vifaa maalum masikioni ili kusikia vizuri.

Pamoja na Matatizo yoote, Tom alifanikiwa kukutana na Alice Miller 23, mwanamke aliyemkubali kama alivyo na wanaishi woote mpaka sasa. Alice anakutana na changamoto nyingi katika kuishi na Tom hususan katika suala la vyakula na mizunguko ya kawaida ya wapendao.

Ugonjwa Abaugua Ton ni watu Wnau tu wanaumwa hivyo duniani.

Mr Staniford is one of only eight people in the world with MDP syndrome, which means that since the age of 12 he has been unable to store fat under his skin or even the soles of his feet

Kimichezo Zaidi

Surprisingly, Mr Staniford also suffers from type 2 diabetes - a disease usually associated with obesity - because he has unusually high fat levels in his blood

Ms Miller says the pair are just like any normal couple - apart from the fact that they don't go clubbing or out for late night drinking sessions because Mr Staniford has to concentrate on his cycling career

Mr Staniford (right, at the age of nine) recently learned that his condition stems from a genetic mutation thanks to a breakthrough by scientists at Exeter University

Enzi za Ototo wake, Tom, 9,(wa kulia) Alikuwa akiungua taratibu taratibu
Mr Staniford (pictured at the age of five) was born at a normal weight, but throughout his childhood and teenage years lost all the fat around his face and limbs
Akiwa na miaka 5
Ms Miller said: 'When I look in to my future I see Tom there. We've been together so long that we know each other very well. I don't think there would ever be anything that would get in the way of that'


Read More »

50 Cent Kwenda Jela Miaka 5 kwa Kosa la Kumshambulia Mpenzi wake na Uharibifu wa Mali.


Rapper na Muigizaji 50 Cent Amekana Mashtaka yanayomkabali ya Kumjeruhi na Kuvunja mali za aliyekuwa Mpenzi wake Dapne Narvaez. 50 Cent ambaye Jina Lake Kamili ni Curtis Jackson Alisimamishwa Kizimbani katika mahakama ya Van Nuys, California Jumatatu Asubuhi.

Ikiwa mahakama itampata na hatia kwa makosa hayo, Mwimbaji huyo wa In Da Club atatakiwa kutumikia Kifungo cha Miaka Mitano Jela na Kulipa Faini ya Dola za Kimarekani 46,000.


I'm innocent: 50 Cent plead not guilty to a domestic violence charge during an arraignment at a Van Nuys Courthouse in Los Angeles on Monday
50 Akiwa Mahakamani Jana Asubuhi.

Kutokana na Mwenendo wa Kesi za Mashambulio kama hiyo, 50 Cent anatakiwa Asimkaribie Anaye Mshtaki kwa Futi 100, wala kuwasiliana nae au familia yake kwa kipindi chote ambacho kesi itakuwa Ikiunguruma. Mbali na hayo Curtis ameambiwa asalimishe Bastola yake na Silaha nyingine anazomiliki ndani ya Masaa 24.

Daphne anamshtaki 50 Cent kwa kumvamia nyumbani kwake, kumpiga na kusababisha uharibifu wa mali zenye thamani ya Dola za Kimarekani 7,000.


Read More »

Mtanzania wa Miaka 14 Aibuka Bingwa wa Kuruka Kamba Duniani, Ampa Faraja Rais Kikwete.

-->

 Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 
 Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani
 Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
 Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
 Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Sport  Training Centre (TSTF), Dennis Makoi
amesema  kuwa walipotambua kuwa kijana
huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. 
Alisema kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki
kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani
Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili
huyo  alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika
Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480
kutoka  timu 44 kutoka nchi 14 ambapo
jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo
alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa
amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa
usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania
ili kuukuza  ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini
kwao  na kuitangaza Tanzania.
Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika
kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea
katika kukiendeleza kipaji chake.


Read More »

Rais Barack Obama Atimiza Miaka 52, Bila Kuzima japo Mshumaa mmoja Hadharani.


Rais wa Marekani Barack Obama Ametimiza Miaka 52 Jumapili ya Jana.Hakukuwa na Sherehe Rasmi za kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo zaidi ya kuonekana siku ya Jumamosi akicheza Golf na Rafiki zake huko Camp David.

Ikulu ya Marekani haikusema ni vipi Amiri Jeshi huyo amesherehekea siku hiyo muhimu kwake. Alirudi majira ya Saa 8 Mchana Akiwa na Marine One, Akaingia ndani. Wakati akikaribia kuingia ndani ilisikika sauti kubwa ikisema "HAPPY BIRTHDAY" kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyejitokeza kushuhudia kama kutakuwa na lolote.

Kiongozi huyo aligeuka, akatabasamu kisha akawapungia mkono. Hapakuwa na dalili za sherehe tena.



Read More »

Salamu ya Heshima Toka kwa Rais Banda kwenda kwa Rais Kikwete


Katika Jambo Ambalo Mwanamke huyu analizingatia ni Mila za Heshima za Kwao, Ijapokuwa ki Utawala wana nafasi sawa na Rais Jakaya Kikwete, lakini Rais huyu wa Malawi aliweza kumpigia Magoti na kutembea mpaka alipo Kikwete Kumsalimia.

Mwanamama huyu machachari aliwahi kutajwa na Forbes kuwa anashikilia nafasi ya 71 Dunia katika orodha ya Wanawake Majasiri Mnamo mwaka 2012 na akapanda hadi nafasi ya 41 Mnamo mwaka 2013.

Read More »

Man's Private Parts Gone missing for 3 days After he was given a Cigarette to smoke.

Elias Peter
A Resident of Mwananyamala Msisiri Dar Es Salaam going by the name of  Elias Peter, had found himself in an awkward situation a couple days ago after the disappearance of His Manhood Parts soon after he had been given a cigarette by a fellow man known as Salehe.

After smoking some few rounds he felt so cold, suddenly with no sex organs. He kept the situation to him self hopping that his thing would return, with no luck Elias decided to tell Salehe and he directed him to a highly respected local man, Mr Kishengwae Mfinanga who told Elias that he was witch crafted and the sex organs shall return though with limited powers.

After 3 days he went back to see Mfinanga who told him to continue to wait and there the Organ Returned but it has no powers at all.

Read More »

Amvunja Mikono na Kumtoa macho mama yake Mzazi, Alimfananisha na Paka.


Tukio la Unyama wa aina yake umefanywa na Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Ferna Quesner, 34 amemjeruhi mama yake mzazi baada ya kumkokota kupitia nywele, kumvunja mikono na pua na kisha kumtoa macho kwa kutumia kisu.

Macho ya  mama huyo bi. Blonia Quesner, 59, yalikutwa karibu na bwawa la damu pembeni yake pamoja na kisu hicho. Polisi walipigiwa simu na majirani huko Lake Worth na walipofika walimkuta Fena amesimama akiwa katapakaa damu na mama yake akiwa chini hana fahamu huku damu zikimtoka.

Ferna amepelekwa katika kituo maalua cha kumchunguza kuhusu matatizo ya akili ambayo aliwahi kuwa nayo mnamo November 2001. Bado hali ya mama yake ni mbaya huko hospitali.

Read More »

Tahadhari za ATM Pins ambazo zinagundulika Kirahisi, Angalia Namba Hizi hapa.



Utafiti Uliofanywa na (PNI) Huko Washington Marekani umebaini Udhaifu katika matumizi ya Namba za Siri za watumiaji wengi wa mashine za kutolea Fedha za ATM.

Kwa Mujibu wa Utafiti huo, Pin ambayo inashika nafasi ya kwanza na rahisi zaidi kubahatishwa ni 1234, Kwa Mujibu wa Jarida la Huffington, kuna Pin namba za kufanana zipatazo 10,000, pia 11% ya Pin zinzotumika ni rahisi kuziotea.

Katika Utafiti huo imegundilika namba za Pin ambazo hutumika sana ni 1234,1111, 0000, 1212, 7777, 1004, 2000, 4444, 2222, 6969.

 Ripoti hiyo ilisisitiza Ubaya wa Pin zinazoanza na 19, yaani zina bahatishika kirahisi mno ikiwa ni miaka ya kuzaliwa ya watu. 

Huku namba ambazo hazitumiki sana au zinatumika na wachache ni zenye Mtiririko huu:- 8068, 8093, 9629, 6835, 7637, 0738, 8967,9480 na 8957.


Tuwe Makini na Namba zetu za PIN.


Read More »

Mrembo Jack, Ajutia Ndoa yake, Asema Alikurupuka.


Super Model wa Bongo, Jacky Patrick amefunguka na kusema ya kwamba kilichopelekea ndoa yake kudumu kwa kipindi kifupi ni kukosa tathmini ya kina na kutofanya maamuzi ya busara juu ya suala la ndoa.

Jack ameongea na gazeti moja hapa nchini na kusema ya kwamba, laiti wangekaa angalau miaka miwili katika uchumba basi angeweza kumsoma vizuri mumewe huyo kitabia na anaimani asingedumbukia katika shimo hilo.

Jack aliolewa na mfanayabiashara maarufu hapa Bongo ambaye kuna kipindi aliwahi kukamatwa kutokana na skendo za madawa ya kulevya Abdulatif Fundikira Maaruf kama "Tiff"


Read More »

Mwanzo Mpya Kwa Feza Kessy Baada ya Oneza Kufungasha Virago BBA The Chase.


Katika Eviction ya wiki hii tumeshuhudia shemejiii yetu Oneal akiyaaga mashindano yao huku akimwacha mkewe, Mshiriki na mwakilishi aliyebaki mjengoni humo baada ya Nando kuondolewa kwa sababu za kiusalama.

Ingawa Feza amekuwa disappointment machoni kwa mashabiki wengi wa Tanzania kutokana na kusahau kilichompeleka huko, naimani hii itakuwa fursa ya kipekee kwake kujipanga na kurudisha akili yake katika Shindano Hilo.

Mshiriki Nando ambaye alienguliwa katika shindano hilo ndo alikuwa anapewa nafasi kubwa ya ushindi, nna uhakika kilichomkuta kitakuwa fundisho kwa wawakilishi watarajiwa katika Mashindano yajayo.

Read More »

Martin Kadinda Awajia Juu wanao mchafua Wema Sepetu



Meneja wa msanii Wema Sepetu, Martin Kadinda apesha sauti yake hewani na kuwashukia wanao mzushia mrembo huyo skendo za ajabu ili kumchafua huku akisisitiza Wema hayupo kama Wanavyomdhania.

Kupia Blog yake ya Mvuto Kwanza Martini Ameandika:-
"KATIKA PITAPITA ZANGU NIMEKUTANA NA HII STORI MTANDAONI  ETI WEMA SEPETU ATAPELI LAPTOP... KWELI KABISA MTU UZUSHE JAMBO KAMA HILI? TUNAKOELEKEA BASI UTASIKIA AMEMTAPELI RAISI WA NCHI.... HIVI KWANINI BINADAMU HATUWEZI KUWAONEA HURUMA BINADAMU WENZETU....

BEING MANGER WA WEMA SEPETU ITS NOT KUWA NAPATA CHOCHOTE, AM JUST THE SAME MARTIN MWENYE MAISHA YA KAWAIDA KABISA KAMA MTANZANIA MWINGINE THE ONLY THING ILINIFANYA NIFANYE KAZI NA WEMA WAS THE REALITY.

 UKWELI ULIO WAZI.. WEMA NABAHATI YA KUPENDWA NA WATU SANA SANA NA NIKAGUNDUA KUNA MENGI ANAWEZA KUYAFANYA KUPITIA FAME YAKE, THATS THE REASON I MADE SURE ANASEHEMU NZURI YA KUISHI, GARI ZURI LA KUTEMBELEANA NA REALITY SHOW INAYOANZA MWISHONI MWA MWEZI AUGUST... NA KUFANYA NAE KAZI NIMEJIFUNZA MENGI.. WEMA LOVES ATTENTION, VERY MUUUUCH AND KIUKWELI ANAUMIZWA SANA NA SKENDO ZAKE MWENYEWE...

KWAKUWA ANAFANYA MENGI MAZURI LAKINI YANAYOJULIKANA NA KUUZWA NA MAGAZETI NI MABAYA AMBAYO AMEYAFANYA KUTOKANA NA JAZBA AU MAZINGIRA ALIYOPO. KWA ASILIMIA MIA MOJA NAWEZA KUSEMA WEMA HAYUPO VILE MAGAZETI YALIVYOMPOTRAY... REALITY SHOW YAKE IKIANZA MTAAMINI MANENO YANGU...  BACK TO HAYO YA UTAPELI WA LAPTOP..

 SIJAWAHI KUSIKIA SWALA LA KUOMBA LAPTOP KWA YOYOTE KWASABABU SIPO NAE MUDA WOTE AU MAYBE KWAKUWA NAJUA SIO MPENZI WA LAPTOP KIUKWELI... SASA LEO HII NAKUTANA NA STORI ETI AMETAPELI NA MIMI NIMEKUWA NIKIZUNGUMZA NA WAMILIKI WA LAPTOP HIYO.. WE KAKA SIJUI DADA NI LINI UMEZUNGUMZA NA MIMI SWALA LA LAPTOP HEBU MUOGOPE MUNGU WAKO BASI...

 I TRULY HATE STUDIP PEOPLE WHO TAKES ADVANTAGE OF OTHER PEOPLE JUST TO MAKE THEMSELVES HAPPY.... WEMA WILL ALWAYS BE WEMA KWA WEMA WAKE NO MATTER WHAT.... U BETTER TRY HARD TO BEAT HER UP MAANA SHE AINT JOKE."

Hayo ndo yake Kadinda.

Read More »

Video ya Hisia, Kwanini Jack Ulimtenda Mwanamke Mwenzio hivi, tena Rafiki yako?







Ama kweli kikulacho kinguoni mwako, maana Mariam ambaye aliibiwa Mwanaume na Muigizaji wa Filamu Bongo Movie Jack Pentezel wakati akijua ya kwamba mwanaume huyo ni wa rafiki yake na tayari ameshamzalisha mtoto mchanga kiasi kilichopelekea mwanaume huyo kumtelekeza.

Angalia video ya Take One ambapo mmlalamikaji anafunguka vizuri na kwa undani zaidi.


Read More »

Pombe zilinifanya Nimbusu Harrysong, Ajitetea Mrembo.


Muigizaji wa nollywood asiyeishiwa Scandals, Uche Ogbodo, amejitetea baada ya kuvuja picha zikimwonesha anambusu mume wa mtu, msanii wa muziki, Rapper Harry Song. Katika kujitetea huku alisema ya kwamba yeye na Harry ni watu wa karibu na marafiki wa kawaida tu wa muda mrefu.

"Hakuna jingine kati yetu, na hilo busu lilikuwa la kirafiki tu kwani siku hiyo ilikuwa Birthday ya Harry, hivyo tuli kiss kama kuonesha furaha ya siku hiyo" Alisema Uche.

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger