PICHA YA MTOTO WA KIM NA KANYE BAADA YA MIEZI 6


Nyota wa vipindi vya uhalisia, Kim Kardashian hivi karibuni aliamua kushea na jamii picha ya mtoto wake mzuri wa kike, North West.

Picha hiyo ya karibu ya mtoto wake wa kwanza aliyezaa na rapa Kanye West, inamuonyesha mtoto huyo akiwa mwenye furaha huku akiwa anacheka.

Read More »

MCHAGA AICHOMA NYUMBA YAKE MOTO BAADA YA KUBAINI MKEWE ANAISALITI NDOA YAO HUKU SEGEREA DAR.



Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.

Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea Jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.

Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali

Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo.

Mpaka Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.

Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.


Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa



Read More »

MKURYA HUYU AISHI NDANI YA HANDAKI KWA ZAIDI YA MIAKA MINNE HAPA DAR



DUNIA haiishi vituko! Chacha Makenge (36)  mzaliwa wa Kijiji cha Kisangula, Mtukula, Serengeti mkoani Mara anaishi jijini Dar lakini ndani ya handaki aliloligeuza chumba kwa miaka minne sasa, ni ajabu lakini ni kweli.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni nje ya handaki hilo lililopo mita chache kutoka majengo ya biashara ya Mlimani City, Makenge alisema alichukua uamuzi huo baada ya rafiki yake (jina linahifadhiwa) kumchomea nyumba na kuteketeza samani zote.

“Ilikuwa mwaka 2009 mwanzoni rafiki yangu huyo ndiye alinipa sehemu ya kiwanja chake nijenge nyumba. Nikawa  naishi hapo huku nikiendelea na shughuli zangu za kila siku.

“Siku moja akabadili mawazo, akanitaka nihame katika eneo lake bila kunipa sababu, nilimwomba anipe muda nitafute pa kwenda.

“Julai 2009 akaja na polisi, akanikamata na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Stakishari, nilipowauliza kosa langu, hawakunieleza.
“Baada ya siku mbili majirani walikuja kuniona na kuniambia kwamba nyumba yangu imechomwa moto na kila kitu kilichokuwa ndani kimeteketea, aliyefanya hivyo ni rafiki yangu. Nilijisikia vibaya sana.

“Siku iliyofuata majirani walikuja tena kituoni wakaniwekea dhamana. Nilipofika kwangu nilikuta majivu tu, iliniuma sana, nililia lakini sikupata ufumbuzi. Kwa vile nilikuwa sina pa kwenda ilibidi niwe nalala palepale nilipochomewa nyumba nikisaidiwa chakula na majirani.

“Siku iliyofuata, saa nne usiku nilivamiwa na watu wanne, wakiwa na mapanga na marungu, nilipambana nao mpaka wakaondoka. Kesho yake nilikwenda kwa mwenyekiti wetu wa serikali ya mtaa, Jumanne Malima kumweleza yaliyonipata, alisikitika, akaniandikia barua kwenda Polisi Stakishari.

“Nilipofika kituoni sikusikilizwa, badala yake walinikamata tena na kuniweka ndani wakidai kwamba nimefunguliwa kesi ya kumjeruhi mtu kwa panga. Hawakukubali niwekewe dhamana.

“Julai 31, 2009 nilifikishwa Mahakama ya Mwanzo Ukonga na baadaye nilipelekwa Mahabusu ya Gereza la Keko, nikawa napelekwa mahakamani hadi Septemba mwaka huo ambako nilihukumiwa kwenda jela miezi 9.

“Nilitumikia maisha ya jela hadi Desemba 10, 2009 nikatolewa kwa msamaha wa Rais Jakaya Kikwete. Nilikwenda kuishi kwa ndugu zangu huku wakifuatilia sababu ya kufanyiwa vitendo hivyo bila mafanikio.

“Maisha ya kwa ndugu hayakunifurahisha kwani hata wao walikuwa na majukumu mengi, niliamua kuendelea na kazi zangu za sanaa pia utunzaji wa mazingira na bustani kwa watu wakawa wananilipa fedha.

“Ndipo nilipoamua kutafuta sehemu iliyotulia ili niweze kuishi, nikapata hapa, ni jirani na Mlimani City. Nilichimba handaki kubwa kama unavyoliona, kwa chini kuna kitanda ninacholalia.

“Kwa hakika hapa sipati shida, wala kelele. Kwanza ni tulivu sana, nimefikia hatua ya kuishi kama mnyama kutokana na mateso na bugudha nilizopata, wengi hawajui nilipo, nipo katika pori hili kwa miaka minne sasa,”alisema Makenge.

GPL

Read More »

BILIONEA AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI DAR, ASEMEKANA KAJIUA MWENYEWE


NI jambo lililotoa mshtuko kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani ambapo Desemba 10, mwaka huu, walikuta mwili wa binadamu ukiwa ndani ya gari lililopinduka, pembeni mwa Barabara ya Kisarawe - Mwaneromango.

Mbali na mwili, ndani ya gari hilo aina ya Toyota RAV 4 (milango mitatu new model) lenye namba za usajili T 273 AKP kulikutwa bastola moja, risasi 85 na magazini mbili.

Utata ukaanzia hapo, polisi wa wilaya hiyo wakiongozwa na mkuu wao (aliomba jina lisitiriwe kwa sababu si msemaji) wakajiuliza ni nani mtu huyo ambaye alikuwa amefariki dunia? Kumbe alikuwa Suleiman Muhema (42), bilionea kijana mkazi wa jijini Dar es Salaam.

polisi waliuchukua mwili wake na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Wilaya mpaka ndugu walipokwenda kuuchukua kwa mazishi.

SULEIMAN MUHEMA NI NANI?
Suleiman Muhema ni mkazi wa jijini Dar, amejenga jumba la kifahari Kijitonyama ambako aliishi na mke wake, Zihji Mvungi (42).

Mpaka kifo chake alikuwa mfanyabiashara wa magari kutoka Japan akiyauza Dar, pia alikuwa na kampuni ya usafirishaji, sifa zote kwa pamoja zinamfanya aitwe bilionea.

MAISHA SIKU CHACHE KABLA YA KIFO
Habari zinadai kuwa, marehemu alikuwa ndani ya mgogoro wa kifedha na mtu ambaye hakutajwa jina lakini ni wa karibu naye.
Inadaiwa kuwa, mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulikuwa ukisuluhishwa na Dawati la Jinsia, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar.

SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio inadaiwa marehemu alikuwa Magomeni na watu (idadi yao haikujulikana). Baada ya hapo aliondoka  kwenda kusikojulikana lakini baadaye alimpigia  simu ndugu wa karibu na kumwambia kuwa yuko mahali (hakupataja) ametekwa na sauti anayoitoa inaweza kuwa ya mwisho kisha akakata simu.

MAELEZO YA POLISI SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Kisarawe, Desemba 10, mwaka huu,  usiku wa saa nane,  marehemu alionekana akiwa ndani ya gari jeusi umbali wa kilomita saba kutoka Kisarawe Mjini lakini aliondoka baada ya kuliona gari la ‘patroo’ ya polisi.

Chanzo hicho kikasema kuwa dakika chache mbele polisi waliokuwa katika shughuli za ulinzi usiku huo waliliona gari hilo likienda pembezoni mwa barabara na kupinduka.

“Tulilifuatilia, tukalikuta limepinduka, ndani ya gari tulimkuta mtu amekufa kwa kujipiga risasi kwani sehemu ya kidevuni na kwenye utosi kulikuwa na tundu la risasi,” kilisema chanzo hicho.

MAREHEMU ALIDHANIWA MHALIFU
Habari zinasema katika upekuzi wa awali ambapo polisi walimkuta marehemu akiwa na bastola, risasi 85 na  magazini mbili walidhani alikuwa mhalifu aliyetaka kutekeleza uhalifu mahali ndani ya walaya hiyo.

NDUGU WA MAREHEMU WANA NENO
Kwa upande wao ndugu wa marehemu ambao waliomba majina yao yawekwe pembeni, walisema kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu kifo cha ndugu yao huyo kwa sababu hata kifo chake hawakielewielewi.
Akizungumza kwa hisia ya uchungu, ndugu mmoja alisema katika maisha ya jijini Dar, yeye ndiye baba wa marehemu lakini hakuna alichojua toka kifo hadi kuzikwa.

Alisema hata mazishi ya marehemu alishtukizwa  kwamba anazikwa siku hiyo jambo lililompa wakati mgumu kufikiria.
 “Sisi kama ndugu wa marehemu, tulipenda akazikwe nyumbani, Makete   (Njombe), lakini ghafla tukaambiwa anazikwa hapahapa Dar tena siku hiyohiyo tuliyopewa taarifa,” alisema ndugu huyo.

MKE WA MAREHEMU NAYE
Kwa upande wake mke wa marehemu Zihji alipoulizwa na mapaparazi wetu juzi kuhusu sakata la kifo cha mumewe alijibu kuwa kila mtu anaweza kuongea jambo lolote.

Aliongeza kusema anachojua yeye ni kwamba kifo cha mumewe kilitokea kama ambavyo mtu mwingine angeweza kufa.

KAMANDA WA POLISI ANASEMAJE?
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, ACP Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu alikutwa akiwa na jeraha la risasi moja hali ambayo ilionesha alijipiga risasi mwenyewe pengine kutokana na mambo yaliyokuwa yakimsonga kichwani.

BILIONEA AZIKWA DAR
Marehemu Muhema alizikwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Makaburi ya Sinza jijini Dar. Ameacha mke na watoto watatu wa kike. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.

MASWALI TATA
Kifo cha Muhema kina maswali tata mengi. Kwanza, kama kweli alipanga kujiua kwanini alikwenda mbali na Jiji la Dar es Salaam?

Pili, kwa nini damu ndani ya gari ilikuwa kidogo wakati uzoefu unaonesha kuwa, mtu anayepigwa risasi ndani ya gari huacha damu nyingi?

Tatu, ndugu mmoja wa marehemu alikiri kuwa, Muhema alinunua bastola mwaka huu ili kujilinda, sawa kabisa. Je, kwa nini akutwe na risasi nyingi kiasi hicho kama alikuwa anakwenda kufanya uhalifu?

Nne, ilidaiwa alimpigia simu ndugu mmoja akidai ametekwa na huenda asisikike tena. Polisi walikuta simu kwenye gari lake, kwa nini waseme alijipiga risasi mwenyewe?

GPL

Read More »

BIFU LA HEMED NA YUSUPH MLELA LAZIDI KUPAA



Hemed (kushoto) akimtishia bastola Mlela
Hemed na Mlela wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya kuumizana huku mama yao akiwaangalia kwa huzuni…
Ni katika Filamu yao Mpya ya I KNOW YOU.

Read More »

PICHA ZA MATUKIO KATIKA UZINDUZI WA AZAM TV


Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Yusuf Bakhresa (kushoto) akifungua rasmi Azam Tv  mbele ya Mtendaji Mkuu wa Azam Media Rhys Torrington.
Mmoja wa watoa huduma kwa wateja akiwa tayari kuwahudumia wateja.…
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Yusuf Bakhresa (kushoto) akifungua rasmi Azam Tv  mbele ya Mtendaji Mkuu wa Azam Media Rhys Torrington.
Mmoja wa watoa huduma kwa wateja akiwa tayari kuwahudumia wateja.
Kutoka kushoto ni Maulid Kitenge,  Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi Saleh Ally na mmoja wa wafanyakazi wa Azam Tv.
Keki maalum zenye jina la Azam Tv kwa ajili ya wadau.
Kikundi cha burudani cha ngoma za asili kikitoa burudani kabla ya ufunguzi.
Wateja wakipata huduma muda mfupi baada ya ufunguzi.



Wasanii mbalimbali wa Filamu nchini nao walikuwepo kwenye shamrashamra hizo za ufunguzi wa Azam Tv.

Read More »

YOUNG DEE AKAUNUSHA KUHUSU SKENDO YA KUFUMANIWA NA LULU WAKILA RAHA ZA UKUBWANI NDANI YA GARI




Juzi kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds FM chini ya bwana Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na fununu kali iliyokuwa inamuhusu mwanadada wa Bongo Movies na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D 'Young Dar es Salaam' kama mwenyewe anavyojiita baada ya wawili hao kukutwa kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya mdada na mkaka kufunga ndoa.
Young D
                                                                                              

Kwa mujibu wa Sudi Brown 'Gossip Cop' wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezi Beach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada Lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.

Habari zainasema baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongea na Polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.

Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majiu ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds Fm.
GPL

Read More »

MWALIMU MKUU AFARIKI KIFO CHA UTATA, USHIRIKINA WATAWALA.




Mwalimu Gloria Tarimo ‘Ticha Gloria’ (29) aliyekuwa akifundisha katika Shule ya Mbezi High School ya jijini Dar, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakidai kifo chake ni cha kimiujiza.
Ticha Gloria ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo, alifariki dunia Desemba 6, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar huku wengi wakihisi kuna mkono wa mtu nyuma ya kifo hicho.
                                                      Marehemu Glory A Tarimo enzi za uhai wake.
USHIRIKINA WAHUSISHWA
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa ndugu wa marehemu aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa familia alisema, kifo cha Ticha Gloria kinahusishwa na ushirikina kwa kuwa kabla ya mauti kumfika alikumbana na mambo mengi ya ajabu.
“Ni kifo cha ajabu kwa kweli na kimemshangaza kila mmoja wetu. Nakumbuka ilikuwa Juni, mwaka huu ambapo alienda kazini na alipofika kwenye mlango wa ofisi yake alikuta nazi imevunjwa.
“Licha ya kushangazwa na uwepo wa nazi hiyo, aliiruka kisha akaingia ofisini kwake. Kuanzia hapo alianza kuumwa mguu, kuna wakati akawa anahisi unawaka moto. Tulimpeleka Hospitali ya Muhimbili, akapatiwa matibabu na akapata nafuu,” alisema ndugu huyo.

AKUTA NJIWA KWENYE KITI OFISINI
Ndugu huyo alizidi kueleza kwa masikitiko kuwa, baada ya tukio hilo la kukuta nazi imevunjwa kwenye mlango wa ofisi yake, mambo hayakuishia hapo kwani hivi karibuni alipoingia ofisini kwake alikuta Njiwa kwenye kiti chake.
“Alipiga kelele sana, walimu na wanafunzi wake wakaja  kushuhudia huku kila mmoja akishangaa na kuogopa kumtoa njiwa yule kwenye kiti.
“Mwalimu mmoja aliyefahamikwa kwa jina la Fadhili ndiye aliyemuondoa njiwa yule. Bila kujua kuwa roho yake inasakwa, Gloria akakaa kwenye kile kiti na kuendelea na shughuli zake,” alisema ndugu huyo na kuongeza:
“Haikuchukua muda mrefu akahisi kama anachomwa na kitu chenye ncha kali kwenye makalio yake huku kichwa kikimuuma sana. Walimu wenzake walimchukua na kumrudisha hospitalini.”

AANZA KUZIONA SIKU ZAKE MFULULIZO
 Ilielezwa kuwa, baada ya mwalimu Gloria kufikishwa hospitalini, hali ilizidi kuwa mbaya na akaanza kutokwa na damu ya hedhi mabongemabonge huku damu nyingine ikitokea puani.
Ndugu wa Marehemu.
“Hali ilikuwa hivyo, akawa anateseka sana huku wakati mwingine akilalamikia baadhi ya walimu wenzake kuwa ndiyo wanaotaka kumtoa roho.
“Kuna siku alimuita daktari aliyekuwa akimhudumia na kumwambia anamshukuru kwa kujitahidi kuokoa uhai wake lakini anaamini hatapona kwani anajua kuna walimu wamedhamiria kumuua ili wakalie kiti cha ualimu mkuu, baada ya hapo alikata roho,” alisema ndugu huyo ambaye ndiye aliyekuwa akiwasiliana na marehemu mara kwa mara.

WALIMU WANASEMAJE?
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya walimu wa shule hiyo walisema wamesikitishwa sana na kifo cha Ticha Gloria, wakasema licha ya kwamba kila kifo kinapangwa na Mungu lakini hiki cha mwenzao kimeacha utata.
“Kwa kweli kifo cha Gloria kimenifanya niamini kuwa Mungu yupo lakini pia ushirikina upo. Amekufa kifo cha kimiujiza sana, mambo yaliyomtokea kabla ya kufariki dunia yanaashiria kabisa kuna mkono wa mtu,” alisema mwalimu mmoja wa kike aliyeomba hifadhi ya jina lake.
MSIKIE MWENYE SHULE
Mkurugenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Said Mgude alielezea masikitiko yake juu ya kifo cha mwalimu Gloria kwa kuwa alikuwa mchapakazi sana ila akataka watu wasihusishe kifo hicho na mambo ya kishirikina.
“Kila mmoja lazima aumie kwa kifo cha Gloria, lakini nawasihi watu wamuamini Mungu na waachane na dhana za kishirikina. Shule yangu ni taasisi kubwa sana, minazi ipo mingi hivyo kama alikuta nazi imevujwa mlangoni inawezekana ilianguka tu na kupasuka.
“Kuhusu Njiwa hapa Dar es Salaam siyo jambo la ajabu kwa sababu wapo wengi sana, mimi siwezi kukubaliana na mambo hayo ya kishirikina na hakuna kitu kama hicho,” alisema.
Mwili  wa mwalimu Gloria uliagwa Desemba 10, mwaka huu katika Kanisa Katoliki Mbezi Mwisho jijini Dar na baadaye ulisafirishwa kwenda  Moshi Rombo mkoani Kilimanjaro na kuzikwa siku iliyofuata ya Desemba 11.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amin.

GPL

Read More »

RAIS KIKWETE ATOA HOTOBA KATIKA MAZISHI YA MANDELA HUKO QUNU AFRICA YA KUSINI




Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika mazishi ya Nelson Mandela kijijini Qunu, Afrika Kusini.
Jeneza lenye mwili wa Hayati Nelson Mandela likiwa mbele ya waombolezaji katika kijiji cha Qunu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehutubia kwenye shughuli ya mwisho ya mazishi ya Nelson Mandela katika Kijiji Cha Qunu ambapo ndipo maziko yanapofanyika hapo baadaye.
Rais Kikwete amesimulia uhusiano wa karibu uliokuwepo enzi za utawala wa Mandela na Mwalimu Nyerere.
Mwili wa hayati Mandela utazikwa kwa tamaduni za Xhosa, ambapo ng’ombe dume atachinjwa na jeneza la Mandela kufungwa kwa ngozi ya Chui.

GPL

Read More »

UGOMVI WA KIMAPNZ WASABABISHA MUME KUUA MTOTO WA KAMBO HUKO IRINGA




Mwenyekiti wa mtaa wa pangani kata ya Makorongoni mjini Iringa Salum Kibaya akiutazama mwili wa mtoto Raymond Ben Mangungu (2) aliyeuwawa kwa kukabwa shingo na baba wa kambo wakati wa ugomvi wa kimapnzi kati ya mwanaume huyo na mama wa mtoto huyo usiku wa leo.
Askari  polisi akitazama mwili wa mtoto  huyo.
Hali  ilivyokutwa ndani ya chumba  hicho  baada ya  tukio.
Wananchi wa Makorongini wakimtazama mwanamke huyo wakati akihojiwa na kaka wa mtuhumiwa wa mauwaji hayo.
Mama  wa mtoto Raymond katikati  akimsimulia shemeji  yake jinsi ambavyo mpnzi  wake  alivyoua mtoto ,kushoto ni mama mzazi wa mwanamke  huyo.Huyu  ndie mzazi wa mtoto aliyeuwawa  Bi Kudra Kahemela (23)Wanawake wa mtaa wa Pangani Iringa  wakiuhifadhi mwili wa mtoto Raymond leo.
KATIKA  hali  isiyo ya kawaida mwanaume  mmoja mkazi  wa mtaa wa Pangani kata ya Makorongoni  katika Manispaa ya  Iringa Hamis Said maarufu kwa jina la Mwarabu amemuua  kinyama mtoto Raymond Ben Mangungu (2) kutoka  na ugomvi wa kimapnzi  kati  yake na mama  wa mtoto  huyo ambae kwake ni mpnzi wake .
Imedaiwa  kuwa  mtuhumiwa  huyo  wa mauwaji ya  mtoto  huyo  alikuwa amelewa  pombe  kupita  kiasi na si mara ya kwanza  kulewa kiasi  hicho na  kutishia kufanya mauwaji dhidi ya mtoto  huyo wa kambo kwa kile alichokuwa akidai  kuwa ni fedhea kwake  kuishi  na mwanamke ambae ana  watoto  wawili ambao si damu yake.
Wakizungumzia  juu ya  tukio hilo mashuhuda wa  tukio  hilo kwa sharti la  kutotaja majina yao  walisema  kuwa imekuwa ni kawaida  kwa Mwarabu kumpiga mwanamke  huyo na  familia yake kwa madai kuwa hataki kuwaona  watoto hao  wakiendelea  kuishi katika  nyumba hiyo ambayo ameipanga  yeye .
" Huyu  bwana Mwarabu alikuwa akifanya kazi ya kuuza korosho  mitaani na akirudi  usiku amekuwa  mkali kwa mwanamke  huyo ambae  alikuwa akidai kuwa bado amekuwa na mahusiano na baba  wa  watoto  hao  wawili .....hata  hivyo sisi kama majirani  tumekuwa  tukishindwa  kuwaamua kutokana na mwanaume  kuwa na tabia ya kulewa  pombe  kupita  kiasi na hata  tukio  hili tulijua ni kawaida  yao "
Mtoto  Tinito Mangungu (6) ambae  ni kaka  na  marehemu alisema  kuwa  baba yao  huyo mdogo alifika usiku na  kuwataka  wote  kuamka kitandani na  kuwa hakuna mtu atakayelala katika  chumba  hicho kama si  damu  yake.
"Baba mdogo  (Mwarabu) alirudi  usiku akiwa amelewa na kusema hakuna mtu  kulala kitandani na kuanza  kumpiga mama kwa meza na viti  huku sisi  tukilia kumtaka asimpige  mama yetu....baada ya hapo alimchukua mdogo  wangu na kuanza kumkaba  shingo na kumwacha  kitandani akiwa amelama bila kuamka  hadi  sasa mama anasema amekufa"
Akielezea  juu ya mkasa  huo  uliosababisha mauwaji  ya mtoto Raymond mama mzazi  wa mtoto  huyo Bi Kudra Kahemela (23) alisema  kuwa kwa upande  wake baada ya  kutishiwa kuuwawa kwa  kipigo alifanikiwa  kukimbia katika  chumba  hicho  na kwenda  kujificha  nje na baada ya muda mwanaume  huyo alianza  kutapika na pale  alipoingia kutana kumsaidia ndipo alipopigwa na kuamua kukimbia kwenda kulala nje ya nyumba  hiyo kwa  kujiegesha katika nguzo ya umeme  iliyopo nyumba ya pili karibu na nyumba ya  shekhe wa  mkoa Juma Alli Tagalile 
Alisema  kuwa asubuhi  aliingia katika  chumba  hicho baada ya mwanaume  huyo  kutoka kwenda katika kilabu  cha pombe za kienyeji  cha Tulivu  kuendelea  kunywa  pombe na  kumkuta mtoto  huyo akiwa amelala bila  kutikisika .
" Mimi  nilijua kama mtoto  amelala tu ama amezimia ila baada ya  kuwaita watu  wazima akiwemo mama yangu mzazi ndipo  nilipobaini  kuwa mtoto  wangu Ray amefariki  dunia na  ndipo  nilipomfuata na kumweleza juu ya tukio  hilo  ila bado  aliendelea  kunywa  pombe na kudai kuwa mtoto  huyo amezimia kwa  kelele za usiku ."
Alisema baada ya hapo mwanaume  huyo alikimbia hadi Ilala kwa wakwe  zake na kuomba msamaha na kusuluhishwa  ugomvi  wao  ila  wakati mtengo wa kukamatwa  ukiwekwa  ndipo alipokimbia kusiko  julikana.
Mwandishi  wa habari hizi  alishuhudia mtoto  huyo akiwa amekufa  katika  kitanda cha  wazazi  wake huku chini ya  chumba hicho  thamani mbali mbali pamoja na vyombo  vikiwa  vimevunjika kutokana na ugomvi  huo .
Mwenyekiti  wa serikali ya  mtaa  huo wa Pangani kata ya Makorongini Bw  Salum Kibaya  amethibitisha  juu ya  kifo  cha mtoto  huyo na kuwa baada ya  tukio  hilo ambalo  lilitokea  usiku wa kuamkia  leo jumamosi Desemba 14 mwaka  huu alilazimika kwenda  kituo cha polisi  cha stendi  kuu ya mabasi yaendeyo mikoani na kuwajulisha  juu ya tukio  hilo na kufika  eneo  la tukio .
Bw  Kibaya  alithibitisha  pia  kuwa ugomvi kati ya wapenzi hao  si wa kwanza  kutokea  japo kwa maelezo ya  mwanamke  huyo alikuwa mbioni  kuolewa na mwanaume  huyo na hivyo kuwa na wanaume  wawili akiwemo mzazi mwenzake ambae kwa  sasa anaishi  eneo la Don Bosco mjini hapa.
Mwili  wa mtoto   huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa  huku jeshi la polisi likiwahoji  mama  wa mtoto  huyo ,kama  wa mtuhumiwa wa mauwaji  hayo ambae ni mkazi wa Mlandizi Kibaha Jijini Dar es Salaam  na mama mzazi  wa mtoto aliyepoteza maisha.

source: Matukio Daima

Read More »

HEMED 'PHD' ALA SHAVU LA KUIGIZA FILAMU ZAMBIA.



Msanii wa filamu Hemedy Suleiman'PHD' amealikwa kufanya filamu iitwayo ‘Tangled Mess’ na mastaa wa Zambia akiwemo shiriki wa BBA 8, Sulu Banda,mwanamuziki mkongwe wa Zambia Moureen Lilanda na Dj mkongwe wa Zambia DJ Yahya Kiba kwa ajili ya kumuenzi Kanumba.

Bongomovies.

Read More »

SAFARI YA KUUGA MWILI WA MANDELA, ANGALIA PICS HAPA.



December 13.
A cheering man climbs up a fence after the casket of Mandela passed on its way to the Union Buildings on December 13.A cheering man climbs up a fence after the casket of Mandela passed on its way to the Union Buildings on December 13.
A rainbow forms over the Union Buildings in Pretoria on Thursday, December 12, after the public viewing of Mandela's casket. A rainbow forms over the Union Buildings in Pretoria on Thursday, December 12, after the public viewing of Mandela's casket.
Mandela's funeral procession drives toward the Union Buildings on December 12. Each morning his remains were transported from the mortuary to the government buildings. Mandela's funeral procession drives toward the Union Buildings on December 12. Each morning his remains were transported from the mortuary to the government…



The hearse carrying former South African President Nelson Mandela leaves the Union Buildings after the final day of his lying in state in Pretoria, South Africa, on Friday, December 13.The national flag-draped coffin of the former South African President is carried down steps of the Union Buildings at the end of the third and final day of lying in state on December 13.South African Naval personnel stand guard around Mandela's casket as he is carried to the Union Buildings on the final day of his lying in state on December 13.South African Naval personnel stand guard around Mandela's casket as he is carried to the Union Buildings on the final day of his lying in state on 

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger