Agness Aweka Picha nyingine za Utata Akiwa Uraiani



SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya, ‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha za utupu mtandaoni.

Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine.



Baada ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata, alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na maadili ya Mtanzania.


“Sasa huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni lazima sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi kiasi hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo.

Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.


“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.

Read More »

Mainda aipasua Bongo Movie....Ni baada ya kuwachanganya k!mapenz! vigogo wawili wa kundi hilo.


Imebainika kuwa chanzo kikubwa cha kundi lililokuwa na nguvu katika tasnia ya filamu hapa nchini la bongo unity kugawanyika ni Mwanaidi Suka 'Mainda'.

Chanzo cha habari kilichoomba kuhifadhiwa jina kimeeleza kuwa Mainda amekuwa chanzo kwa sababu wasanii wawili wa kundi hilo wenye nguvu kubwa walikuwa wakigombania  penzi lake.

Kimeendelea kusema kuwa, awali, Ray alikuwa akitoka na msanii huyo lakini ghafla upepo ulibadilika ambapo kiongozi wa ufundi wa kundi hilo alianza kulisarandia penzi la Mainda.

Inadaiwa kuwa kiongozi huyo wa ufundi ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa wa kuwafuata wafadhili wa kundi hilo alishindwa kumpata mainda ndipo akaamua kuacha kupeleka udhamini ndani ya kundi hilo na hivyo kusababisha kundi kupoteza mwelekeo.

''Jamaa alikuwa na nguvu kubwa sana  kuwashawishi viongozi na wafanyabiashara wakubwa kudhamini shughuli za kundi hilo lakini toka mtafaruku huo ulipotokea jamaa amejiweka pembeni'' alisema.

Aliendelea kusema kuwa,kujitoa kwa kiongozi huyo ndio sababu ya shughuli zilizokuwa zikifanyika na kundi hilo kushindwa kufanyika hivyo kupoteza mwelekeo kwenye jamii.

Hata sababu ya kutohudhuria msiba wa baba yake Wema Sepetu ni hiyo kwani wasanii wengi kwa sasa hawana umoja waliokuwa nao mwanzo chini ya Jacob Steven 'JB' ambaye alikuwa hana maringo na alikua mstari wa mbele kuliongoza kundi.

Isingekuwa Mainda kuwachanganya Ray na huyo jamaa ambaye alikuwa kinara wa kuwatafuta wadhamini wa kundi hilo lingekuwa na nguvu sana kwa sasa ambapo lipo chini ya TAFF,'' kilisema chanzo hicho.

Jitihada za kumpata Ray na Mainda kuzungumzia mpasuko huo zilishindikana kwa kilichoelezwa kuwa wasanii hao wako lokesheni wakiandaa filamu zao.






Read More »

Chup! ya kike, Sidir!a na kifulana cha kike vyadaiwa kuivunja ndoa ya Bob Junior


Ndoa ya mwanamuziki wa bongo flava, Raheem Nanji 'Bob Junior' na kinara wa filamu ya laptop, Halima Ali 'Ritha' imebainika kwenda mrama kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni muigizaji wa filamu za kiswahili wa Kenya, Ashuu Daniel 'Ashley Toto' mwenye makazi yake nchini ujerumani.

Kwa mujibu wa habari ambazo mwandishi  wetu amezipata, Ashley ambaye pia ni promota anayefanya kazi na wanamuziki wa afrika mashariki kwa kuwandalia maonesho nchini ujerumani, amekuwa akitajwa sana na mke wa Bob Junior kuwa ameingilia kati ndoa yake kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe.

Mgogoro huo ulikuwa ukisababisha migongano ya mara kwa mara kati ya wanandoa hao kiasi cha kujikuta wakigombana mara kwa mara karibu kila siku na hasa inapotokea Bob Junior kuwasiliana kwa simu na Ashley kwa mazungumzo ambayo  yalikuwa na ashirio la kubemelezana kimapenzi baina yao.

Aidha, hivi karibuni mgogoro wa wanandoa hao ulikolea zaidi baada ya Bob Junior kurejea kutoka Kenya alikokuwa na Ashley ambaye kwa sasa yupo mapumzikonu nchini kenya, ambapo baada ya kupekuliwa kwenye begi lake na mkewe  alikutwa  na   chupi ya kike, sidiria na kifulana cha kike.

 ''Bob Junior alikuwa ametoka  Kenya na akawa akijiandaa kwenda Mbeya kwenye shoo nyingine, sasa mkewe akawa anamuandalia nguo zake kwaajili ya safari ya Mbeya.... Sasa katika kupekua pekua, ndio akakutana na sidiria na chupi ya kike ambazo zilishavaliwa bila ya kufuliwa'' kilisema chanzo kimoja cha habari hii.

Imeelezwa, migogoro ulikolea zaidi kutokana na kifulana (top) kilichofumwa na  kutambuliwa na mke  wa Bob Junior  kuwa ni cha Ashley kutokana na kuwahi kumuona amekivaa katika moja ya picha zake katika tovuti ya facebook..

Hali  hiyo  iliibua  ugomvi  mzito  hadi mkewe akaamua kufunga mizigo yake na kurudi kwao Unguja.


Bob Junior  na  Ashley Toto

Aidha, mwandishi wetu alizungumza na mke wa mwanamuziki huyo na kukiri kutokea mgogoro baina yake na mumewe  kiasi cha kuamua kurudi kwao Zanzibar kwa muda na kusubiri kikao cha upatanishi ambacho hajui kitafanyika lini.

''Nimerudi Zanzibar na mwanangu, nasubiri hicho kikao cha kupatanishwa ila nasikitika sana kwa mume wangu kushindwa hata kujua hali ya mtoto na anajua wazi kama anaumwa, nahangaika nae peke yangu.. Sikutegemea kama mume wangu anaweza kufanya ushenzi kama huu,'' alisema.

Hata hivyo mwanamuziki huyo alipoongea nasi alikataa kutoa ufafanuzi wowote, lakini hivi karibuni alikaririwa na mtandao  mmoja akikana kuwa na mke kwa sasa.



Read More »

Sakata na Mwanafunzi aliyebakwa na Kupewa Mimba, hali yazidi kuwa ngumu kwani Ombi lake la Kufanya Mtihani wa Form 4 Lakwama



Kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na EATV kila siku ya Jumanne saa tatu usiku, umma wa Watanzania walipata kufahamu kilichomkuta binti Emma Roberts.

Kwa kukumbusha tu, Emma ni binti aliyefukuzwa shule kutokana na ujauzito. Ujauzito wa Emma ulikuja baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili cha ubakwaji.

 
Kwa mdomo wake mwenyewe, Emma ameelezea hali halisi na kusema kwamba hakupenda huo ndio uwe mustakabali wake wa maisha kwa kuwa alikuwa na ndoto nyingi sana katika maisha. Emma hakupenda  kubakwa.

Tukio hilo limemkosesha nafasi ya kupata haki yake ya msingi, elimu. Emma katika maelezo yake anasema elimu ndio ingemsaidia katika maisha yake yeye na mwanae.

 Akiwa na namba yake ya mtihani tayari kwa ajili ya kufanya mtihani wa kidato cha nne 2013, Emma alisubiria kwa hamu majibu ya ombi lake kwa Wizara ya Elimu imruhusu kufanya mtihani huo. Hata hivyo, Emma hakuweza tena kufanya mtihani kwa kuwa hakupewa ruhusa ya kufanya hivyo.

Kupitia Wanawake Live, Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Mathias Chikawe amezungumza na kueleza sheria ikoje katika masuala kama haya, na kumalizia kuwa 'Hakuna mimba za bahati mbaya'.


Picture
Waziri, Chikawe

Maswali ambayo wengi wanajiuliza ni pamoja na Je, sheria inayotumika kuongoza elimu nchini Tanzania, inawanufaisha wananchi au ni sheria iliyowekwa kukandamiza kikundi fulani cha watu?

Je, Emma Roberts hakupaswa kupigania haki yake ya kupata elimu eti kwa sababu Mhe Waziri wa Sheria na Katiba amesema kwamba 'Hakuna mimba za bahati mbaya'?




Read More »

Mjue Mtangazi mwenye Ushawishi na Anayeskilizwa Sana Tz


Habari kutoka Bongo5.com

Jana tuliitisha kura za maoni Facebook na Twitter kutaka kufahamu kutoka kwa wasomaji wetu kuwa ni mtangazaji gani wa radio nchini mwenye ushawishi mkubwa na anayesikilizwa zaidi kuliko wengine.

Tanzania imeongea, na tunamtambulisha mtangazaji anayependwa zaidi, mwenye ushawishi kuliko wengine na ambaye kipindi chake husikilizwa zaidi, kuwa ni Millard Ayo aka ‘Mtu wa Nguvu’, wa Clouds FM.

Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.

Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM. Kipindi hicho pia ni miongoni mwa vipindi vinavyoiingizia fedha nyingi redio hiyo na kumfanya Millard kuwa miongoni mwa watangazaji wa kituo hicho wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi.

Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 67,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 145,530.

Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki na yenye matangazo mengi.

Kwa mshahara anaoupata, kazi ya uripota wa DSTV, ubalozi wa Fastjet, website yake, deal za voice-overs na mambo mengine, Millard anaingiza takriban ama zaidi ya shilingi milioni 10 kila mwezi.

Millard ni zaidi ya mtangazaji, bali ni mwandishi mwenye ‘pua ya habari’ (nose for news) huku akiongoza kwa kuja na angle za kipekee za habari zenye mvuto kwa watu (human interest stories) zinazokifanya kipindi chake cha Amplifaya kuteka matangazo ya jioni siku za wiki.

Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.

Hakuna shaka kuwa, Millard ana mustakabali wa nguvu kwenye fani hiyo. Ni mfano wa kuigwa kwa watangazaji wengine na hazina kubwa kwa wazazi wake, Clouds Media Group na hata taifa kwa ujumla.
-Bongo5


Read More »

Wastara Awaomba Watanzania wamuache aishi, na yeye ni Binadamu Pia


MSANII wa kike katika filamu za Kibongo, Wastara Juma amewashukia watu wanaotafsiri kila kitu anachokifanya katika maisha yake na kusema: “Yaani nisipige picha nikaweka kwenye mitandao ya kijamii, tayari watu wanasema yao...jamani nami pia ni binadamu.”

Wastara ambaye ni mjane wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ameliambia gazeti hili wikiendi iliyopita kuwa, baada ya kuachwa mpweke na mumewe Sajuki, watu wanafuatilia sana maisha yake kiasi kwamba anakosa uhuru.

Alisema, wengine hutafsiri vibaya hata wanaume anaokuwa nao karibu kikazi au marafiki, akafafanua: “Nashangaa kila nitakachofanya kinaanikwa na kuonekana ni kibaya wakati nami ni binadamu ninao uhuru wa kufurahi na kujiachia nitakavyo ili mradi sijavunja maadili.”


Read More »

Kwa Staili Hii, Ali Kiba Atasubiri sana Mbele ya Diamond ikiwa hataki kubadilika.


Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.
Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.

Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.

Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!

Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa airtel hands across the world waliopiga wakina r.kelly,fall ipupa,2 face kama nafac ile angeipata diamond leo angekuwa wapi?
Diamond leo anatuletea remix ya number 1 f.t Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata kutuletea remix ya Dushelele f.t Fally ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anaejua biashara ya mziki ilivyo labda pengine ni management yake inayomsimamia.Diamond kaweza kuubadilia mziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa show.

Nampenda ali kiba,naipenda sauti yake,anajua mziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na kukubali soko la mziki linataka nini.

Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila usipokuwa makini utajikuta nyuma ya rich,barnaba,dimpoz na ben pol maana mziki sio kuimba peke yake mziki ni biashara pia


Read More »

Mchungaji Atoa Mapepo Sehemu za $iri


Katika mtazamo wa haraka yawezekana ikaonekana kama mchezo wa kuigiza vile au Filamu, la, hii ni kweli imetokea huko pande za Nigeria ambapo kuna Mtumishi mmoja amekuwa akijipatia umaarufu kwa kuwatoa wanawake Mapepo kunako sehemu za $iri.

Pia baadhi ya watu walidiriki kwenda mbali na kusema ya kwamba hata kama una magonjwa ya ngozi au zina@ na yenyewe yanaponywa.

Read More »

Picha 5 za Jamie Alexander na Kavazi ka Ut$pu* ndani ya Red Carpet



Hii ni Miongoni mwa Magauni ya kushangaza yaliyowahi kuvaliwa katika Red Carpet, Hii imefanya hadi mpiga picha kuweza kupata picha ya vyombo vya ndani kiulani baada ya kukaa katika ka angle ka aina yake. Muigizaji Jamie Alexander ndio aliyeamua kuvaa kivazi hiko cha ajabu usiku wa Jumatatu ya Juzi.

Angalia Picha zaidi hapo chini:-







Read More »

Body Guard wa Rihanna ateleza na Kumshika Z!wa Boss wake hadharani.


Katika hali isiyotarajiwa Mlinzi Binafsi wa Mwanamuziki Rihanna amejikuta akishikilia T!ti la mwimbaji badala ya bega lake katika harakati za kutekeleza majukumu yake ya kumlinda katikati ya purukushani ya mamia ya mashabiki.

Tukio hilo la aina yake liliweza kudakwa na kamera kama picha inavyojionesha hapo, hata hivyo huyu bi dada naye kazidi kukaa kihasara hasara ndo maana hata walinzi huona sawa tu kumshika popote pale.

Read More »

Wauza ‘unga’ sasa wabuni mbinu mpya



Wakati Naibu Spika, Job Ndugai akisema maelezo binafsi ya Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) kuhusu biashara ya dawa za kulevya na athari zake aliyoyatoa bungeni juzi jioni hayatajadiliwa, Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini kimeshtukia mbinu mpya zinazotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za hizo.
Ndugai alitoa ufafanuzi huo jana baada ya Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola kuomba mwongozo jana, akitaka Bunge likubali mjadala wa suala hilo kutokana na unyeti wake.
Akizungumza na Mwananchi Dar es Salaam jana, Kamanda wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa alisema wameshtukia mbinu mpya zinazotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, ambao sasa wanatumia barabara badala ya anga.

“Mfano mzuri, tumeshtukia usafirishaji wa epedrine na Juni 24 mwaka huu, Saada Ally Kilongo (26) alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kilo 11,000 za dawa za kulevya aina ya epedrine, ambazo ni mali ghafi za thamani zaidi ya Sh170 mil,” alisema.

Read More »

Mwanamke Aliyepigwa Risasi na Polisi Arusha alazwa ICU



Mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite,Vailet Matias (37), Mkazi wa Njiro Arusha aliyepigwa risasi na polisi Oktoba 31 mwaka huu mkoani Arusha, amehamishiwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Mfanyabiashara huyo alipigwa risasi baada ya kudaiwa kutaka kumpiga risasi polisi aliyekuwa lindoni, akitumia bastola yake kutokana na malumbano ya maegesho ya magari. Awali alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, akiwa chini ya uangalizi mkali.
Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Paulo Kisanga alisema jana kuwa Vailet alihamishiwa chumba cha wagonjwa mahututi tangu juzi kutokana na hali yake kuwa mbaya kutokana na jeraha.
“Ni kweli huyu mgonjwa yupo ICU, mimi nipo nje ya hospitali ila kabla ya kuondoka nilimwacha akiwa katika chumba hicho akipatiwa matibabu” alisema Dk Kisanga.
Taarifa ya Dk Kisanga ilitolewa wakati kukiwa na uvumi wa kufariki kwa mfanyabiashara huyo, ambao jana ulisambaa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana kuwa alikuwa hana taarifa kamili za afya ya mgonjwa huyo.
Alisema awali baada ya mfanyabiashara kuegesha gari hilo mbele ya lango kuu la kuingia katika Tawi la Benki ya CRDB, alitakiwa kulitoa na akagoma ndipo polisi walilitoa upepo na kwamba alipokuta limetolewa upepo ndipo alipoanza kulumbana na polisi hadi akapigwa risasi.
Hata hivyo wakati mfanyabiashara huyo akiwa mahututi, uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwa bastola aliyotumia ni mali yake.

Read More »

Ray C na Rachel wafanana Sauti hadi Sura, Angalia Hapa



Mara ya kwanza tu Recho alipoanza kusikika, sauti yake ilianza kufananishwa na ya Ray C. Kuanzia kwenye Kizunguzungu, Upepo na Nashukuru Umerudi, Recho alikuwa Ray C mtupu.

Hata hivyo hiyo haikumsumbua, Ray C ambaye alisema kuwa ni faraja kumsikia Recho akiimba kama yeye na tangu hapo wamekuwa marafiki.

Lakini wawili hawa, hawafanani sauti tu. Picha hii (hapo juu) iliwekwa na Ray C kwenye Instagram na wengi walidai kuwa, warembo hao wanafanana kama mapacha vile.

Read More »

Oprah Awakuna Wabongo kwa Kuandika Chai katika Tweet yake ya Jumapili iliyopita.



Mtangazaji Maarufu Kutoka Marekani Oprah Winfrey ameonyesha kuikubali lugha ya Kiswahili baada ya kupost Picha Akiwa ameandaa Chai kwa ajili ya kiburudisho cha  siku ya juma pili.
Oprah aliandika kupitia ukurasa wake wa Insta Gram ” CHAI READY FOR #SUPERSOULSUNDAY  WITH @REALROBBELL ” Huku akionekana kushika kikombe cha Chai na tabasam kubwa kabisa

wpid-IMG_20131103_211516.jpg

Haya ndio maneno ya Oprah aliyopost Instagram
Oprah Aliwahi kutembelea Tanzania katika Mbuga ya wanyama ya Serengeti na kupata Kifungua kinywa kati kati ya Mbuga, huenda huko ndipo alipopata neno CHAI

Read More »

Rais Kikwete na Kenyatta wa Kenya wakutana na kuteta jambo muhimu leo huko Afrika Kusini



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyemtembelea na kumsabahi hotelini kwake Sandton Sun jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, leo November  5, 2013 (picha: Ikulu ya Tanzania)


Read More »

Nay wa Mitego ana Historia ya Kumpiga Baba yake Mzazi


Nay wa Mitego ni moja kati ya wasanii wenye tungo zenye utata sana tangu anaanza kufanya muziki ambapo alikuwa akisikika kwenye baadhi ya ngoma akimchana hata baba yake mzazi kwa kushindwa kuwa responsible kwake.

Hit maker wa ‘Muziki Gani’ ambae anakiri kuwa zamani alikuwa mkorofi sana na kwamba sasa hivi amebaki kuongea tu kwenye muziki, amewahi kufunguka kuwa alimpa kichapo baba yake wa kambo/baba yake wa kufikia ambae alikuwa akimtunza kwa muda huo.
Kisa cha kumpa kichapo mzee wa watu.. ni kwa sababu alikuwa anampiga sana mama yake Nay wa Mitego kitu ambacho kilikua kinamuumiza sana yeye, na mwisho wa siku akachukua uamuzi wa kumpiga akimtetea mama yake.

Tukio hilo lilimsukuma Nay wa Mitego kuandika mashairi ya wimbo unaohusu wanawake akiwaambia wanaume wenye tabia kama za baba yake wa kufikia kwamba ‘Mwanamke hapigwi, anatulizwa na mapenzi.’

“Ule wimbo ulikuwa ni dedication kwa mama yangu mzazi, mama yangu mzazi alikuwa anaishi na baba yangu wa kufikia, yule baba yangu alikuwa mkorofi sana, alikuwa anampiga sana mama bila sababu, kiasi kwamba alisababisha mimi na mama tusielewane kwa sababu mimi nilikua sipendi vile alivyokuwa anamfanyia mama, mi nakumbuka kwa bahati mbaya nilishawahi kumpiga yule mzee and then mama yangu akachukua hatua ambayo mimi sikuitegemea kwa sababu mimi nilikuwa namtetea mama.

“Mi nikajifunza kwamba mwanamke hatakiwi kupigwa hata siku moja, na ndo maana nikaimba, so ilikuwa dedication kwa mama yangu na wanawake wote Afrika.” Alisema Nay wa Mitego.

Read More »

Bahati Bukuku Ampoteza Baba yake Mzazi.


MSIBA mkubwa umeikumba familia ya msanii wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku ya baba yake mzazi Mzee Paul Bukuku kufariki dunia baada kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amefia nyumbani kwa Bahati maeneo ya Tabata, jijini Dar es Salaam.

Akiongea na Mwandishi wetu, Bahati amethibitisha kifo cha baba yake kilichotokea asubuhi ya leo, pia amewataka Watanzania kumuombea katika kipindi hiki kigumu kwake. "Baba yangu amefariki leo baada ya kuugua kwa muda mrefu, nawaomba Watanzania waniombee kwa kipindi hiki kigumu kwangu," alisema Bahati.

GPL

Read More »

Lol, Angalia Alichokifanya Afr0 Candy hapa


Yule Muigizaji wa Sinema za Ng0n0 Kutoka nchini Nigeria ambaye amekuwa haishiwi vituko katika kuhakikisha jina lake lizidi kubaki midomoni mwa watu, Afro Candy ameweka picha hiyo katika moja ya Kurasa za Mitandao yake ya kijamii, sasa sijui ana mkaribisha mteja au anamaanisha nini, mimi yangu macho!!!!

Read More »

Watu 6 Mbaroni kwa Tuhuma za Kumshambulia Dkt Sengondo Mvungi


 WATU 6 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na tukio la kumshambulia Dkt. Sengondo Mvungi aliyevamiwa na majambazi nyumbani kwake Kibamba Msakuzi juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova amesema katika operesheni maalum iliyofanywa na jeshi la polisi, wamefanikiwa kuwakamata watu sita ambao majina yako yamehifadhiwa kwa sababu za usalama.

Aidha Kamanda Kova aliongeeza kuwa bado hawajapata uthibitisho kamili juu ya sakata hilo na uchunguzi unaendelea kuwabaini wahusika halisi wa shambulio hilo

GPL.

Read More »

Lowassa aitahadharisha Serikali na Matatizo ya Ajira kwa Vijana


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametahadharisha kuwa kama tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana halitapatiwa ufumbuzi, itakuwa chanzo cha serikali kupoteza madaraka.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2014/2015, uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira.

Lowassa alisema serikali inapaswa kuangalia kipaumbele muhimu na kinachowezekana kutekelezwa cha kuanzia na kufuatia kingine.

Alisema kama angekuwa yeye (Lowassa), angeanza na kipengele cha ajira. “Huwezi kuzungumza mipango bila kuzungumza habari ya ajira,” alisema Lowassa.


Alisema serikali inapaswa kukiri kwamba, kuna  Watanzania wengi waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na cha sita, walioko mitaani hawana ajira. Tusipoangalia watakuja kula sahani moja na sisi. Tusipowashughulikia,” alitahadharisha Lowassa.

Alisema iwapo serikali haitokuwa macho juu ya hilo na kulishughulikia, yale yanayotokea katika nchi mbalimbali barani Afrika, yanaweza pia kutokea hapa nchini.

Ingawa Lowassa hakufafanua maana ya kula sahani moja wala kutaja nchi za Afrika ambazo zimesumbuliwa na vijana, Tunisia na Misri ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na vuguvugu la mageuzi kiasi cha kusababisha watawala kuondolewa madarakani.

Vijana kwa maelfu waliingia mitaani katika nchi hizo wakipinga hali mbaya ya uchumi hasa kukosekana kwa ajira na mwishowe serikali zilizokuwa madarakani ziliangushwa.

 Lowassa alisema katika mkutano wa Benki ya Dunia (WB) uliofanyika mwaka huu kulizungumzwa habari kuhusu mdororo wa kiuchumi uliolikumba bara la Ulaya.

Alisema moja ya nchi zilizokumbwa na tatizo hilo ni Hispania, ambayo alisema katika kujinasua, ilimbana kila mwekezaji aliyekuwa akiingia katika nchi hiyo kwa kumpa sharti la kuwekeza ajira ya vijana.

 Kwa mujibu wa Lowassa, mkakati huo uliisaidia Hispania, ambayo katika miaka miwili mitatu iliyofuatia ilifanikiwa kujinasua kuondokana na tatizo hilo.

 “Lazima tuangalie suala la ajira, ni muhimu sana. Mipango mingine haiwezekani bila kutizama suala la ajira,” alisema Lowassa.

Alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwassa, na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, mkoani humo, Elibariki Kingu, ambao alisema wameanza kuhangaikia suala la ajira kwa vijana.  Alisema iwapo kila wizara ikiamua kushughulikia suala la ajira kwa vijana linawezekana.

“Yule mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wameamua kuchukuwa vijana waliomaliza Chuo Kikuu, wamewatafutia mashamba, wamewatafutia trekta. Wale vijana wamefanya kazi nzuri sana. Kwa hiyo, inawezekana,” alisema Lowassa.

Kadhalika, alisema mipango mingi ya maendeleo nchini imekuwa haifanikiwi kutokana na serikali kutokuwa na msimamo wa kufanya maamuzi magumu.

 Badala yake, alisema imekuwa ikiishia kupanga, lakini hakuna utekelezaji na hivyo kuungana na wananchi kulalamikia kukwama kwa mambo.

Alisema anapongeza sana uamuzi wa serikali kuanzisha kitengo maalumu kilicho chini ya Ofisi ya Rais, kijulikanacho kama ‘Presidential Delivery Bureau’ (PDB), kinachosimamia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kusema: “Hongereni sana.”

Hata hivyo, akaitaka serikali kujiuliza maswali kama kitengo hicho kina ‘meno’ ya kufanya maamuzi magumu?

 “Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo hakuna utekelezaji. Tunazungumza, lakini discipline (nidhamu) ya (nchi ya) Malaysia na hapa (Tanzania) ni tofauti. Hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua hamtekelezi,” alisema Lowassa.

Alishauri kuwapo na chombo, ambacho kinaweza kufanya maamuzi magumu na yakawa magumu yanayotekelezeka kweli kweli. Alisema tabia ya kujivika joho la kufanya maamuzi ya utekelezaji, lakini bila kufanya, ni kazi bure.

Kwa hiyo, akasema uamuzi wa kuwa na PDB ni mzuri, lakini akasisitiza kuwa usipoangaliwa itakuwa ni sawa kufanya kazi bure, hivyo akashauri ni lazima kuwapo na meno ya kuuma.

 “Tukikubaliana mambo yafanyike. Haiwezekani katika nchi kila mtu akawa analalamika. Kiongozi analalamika, mwananchi analalamika, haiwezi ikawa ni jamii ya kulalamika lalamika. Awepo mtu mmoja anayefanya maamuzi na anayechukua hatua,” alisema Lowassa.

Alisema bila kuchukua hatua, kazi ya serikali na wananchi itabaki kuwa ya kulalamikiana.

Alitoa mfano wa uhasama uliopo baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akisema hakuna haja kwa Tanzania kugombana na marais; Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya) na Yoweri Museveni (Uganda) kwa kuamua kushirikiana kiuchumi na Sudan Kusini na kuitenga Tanzania.

Alisema kwani Tanzania inaweza kushirikiana na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Goma, ambako alisema ni kuzuri zaidi ya Sudan.

 Lowassa alisema inachohitaji Tanzania kufikia hilo, ni kufufua reli ya kati ili kuzalisha kuliko nchi hizo.

VIPAUMBELE KATIKA MPANGO WA MAENDELEO
Kuhusu vipaumbele vilivyomo katika Mpango huo, alisema ni vingi na kushauri kwamba, vingechaguliwa vichache vikasimamiwa na kutekelezwa.
 
Alisema kupanga vipaumbele vingi kwa wakati mmoja ni vigumu kutekeleza vyote.

ELIMU
Alisema kipaumbele cha pili ambacho alishauri kipewe kipaumbele ni elimu. Lowassa alisema kinachozungumzwa juu ya elimu hakipaswi kupuuzwa na kusema lipo tatizo la msingi katika elimu ya Tanzania, kwani vitu vinavyochukuliwa havitoshelezi.

Alisema alitegemea kuwa Kamati ya Bajeti ingepata taarifa ya Waziri Mkuu iliyotolewa juu ya elimu kama ingetambua baadhi ya matatizo, serikali ikaangalia cha kufanya.

“Haitoshi kuchukua wanafunzi wengi wanaomaliza Chuo Kikuu wakati akienda sokoni uwezo wake wa kimasomo haupo sokoni” alisema Lowassa.

 Alisema hiyo inatokana na wanafunzi wengi wanaomaliza Chuo Kikuu kutokuwa na hakika ya ajira kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kushindana katika soko.

Lowassa alisema kelele zinazopigwa na wananchi juu ya elimu nchini, inafaa ukafanyika mjadala kuangalia tatizo lililopo katika elimu na nini cha uhakika cha kufanya.

Alisema vinginevyo serikali isipoangalia, Tanzania itaachwa nyuma na EAC, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na dunia kwa jumla, badala yake itabaki kuwa mbabaishaji katika soko la elimu.

“Tuwasaidie vijana wetu, tubadilishe mfumo wa elimu, tuangalie tunaweza kufanya nini vizuri zaidi,” alisema Lowassa.

AMSIFU WAZIRI MAGUFULI
Alisema kipaumbele cha tatu kwa maoni ni reli ya kati na kwamba, anamsifu sana Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa barabara aliyoifanya.

Lakini akasema barabara hizo zimeanza kuharibika kwa kasi ya hali ya juu sana.  “Tumetoka Singida juzi, barabara imeharibika vibaya sana. Ile ya Shinyanga, imeharibika vibaya sana. Kwa sababu malori yanayokwenda yanayopasa kutembea kwenye treni yanatembea kwenye barabara…Naomba reli ya kati muiangalie kwa haraka sana,” alisema Lowassa.

FOLENI DAR, AMSIFU WAZIRI MWAKYEMBE
Akizungumzia tatizo la foleni jijini Dar es Salaam, kwanza alimpongeza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na tatizo hilo.

Hata hivyo, alisema jitihada hizo za Waziri Mwakyembe pekee hazitoshi, kwani muda wa saa ambazo wakazi wa Dar es Salaam wanaoupoteza kwenye foleni zikipangwa kwa ajili uzalishaji ni nyingi sana.

Kwa hali hiyo, alisema serikali haiwezi kukaa hivi hivi, kwani hiyo ni hatari kwa uchumi wa nchi.

“Mtafute njia ya kuangalia tunafanyaje foleni ya Dar es Salaam, sasa si kungoja, it has to be done now (inatakiwa kufanyika sasa),” alisema Lowassa.

 MBUNGE AMUUNGA MKONO
Mbunge wa Pangani (CCM), Saleh Pamba, akichangia mjadala huo, alimuunga mkono Lowassa, kwa kusema urasimu uliomo serikalini ni wa kuchukua maamuzi na kusema kwa mwenendo huo kamwe nchi haiwezi kuendelea.  Alisema Malaysia wamefanikiwa na kupiga hatua katika maendeleo kwa sababu kuu moja tu ya kuchukua maamuzi kwa haraka.

CHANZO: NIPASHE




Read More »

Housegeli abakwa na kulawitiwa na bosi wake huko Arusha



VITENDO vya ukatili kwa watoto wenye umri mdogo vimeendelea kushamiri katika jamii, ambapo msichana wa kazi aliyetambulika kwa jina la Anna (13) mkazi wa ngaramtoni wilayani arumeru mkoaani arusha, ameharibika vibaya sehemu zake za siri kutokana na kitendo cha kunajisiwa na kulawitiwa na baba mwenye nyumba wake aliyejulikana kwa jina la Godifrey John(33).

Akizungumza na mwandishi wetu  baada ya kuokolewa na shirika la shaloom center for street children, linalojihusisha na utetezi wa haki za mtoto, mtoto huyo anaeleza kuwa, alianza kufanyiwa vitendo vya ukatili tangu April mwaka huu baada ya kutoka kijijini kwao masumbwe kilichopo wilayani kahama, mkoa wa shinyanga.

Alisema kitendo hicho kilikuwa kikimuumiza sana, lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga alilazimika kuzoea maumivu makali  aliyokuwa akiyapata kwani mwajiri wake alikuwa akishamaliza kumwingilia alikuwa akimtishia kumuua iwapo angethubutu kutoboa siri hiyo kwa mtu yeyote.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano, anaeleza kuwa, bosi wake huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa mazao, alikuwa akimnajisi na kumlawiti kwa kumziba mdomo ili asitoe sauti baada ya kumfungia mke wake chumbani majira ya usiku na mchana hasa kipindi ambacho mkewe alikuwa kwenye hali ya kujifungua.

Alisema bosi wake huyo alikuwa akimwacha mkewe kitandani na kumfuata sebuleni alikokuwa amelala na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile huku akiwa amemziba mdomo ili asitoe kelele wakati akifanyiwa ukatili huo.

''Alikuwa akiniingilia mara kwa mara, sikumbuki ni mara ngapi, na akianza kunifanyia mchezo mbaya alikuwa akiniziba mdomo na mkewe alikuwa akimfungia chumbani kwa komeo na kuna kipindi alikuwa mkali akinikaripia'' alisema.

Alisema kuwa, alifika mkoani arusha, mwezi februari mwaka huu, baada ya kuchukuliwa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la zawadi samuel ambaye ni rafiki yake na mtuhumiwa, ambaye alikuwa akihitaji msichana wa kazi kutokana na mkewe kuwa mjamzito.

"Huyo zawadi tulikutana nae kwenye basi nikitoka masumbwe kwenda kahama mjini, akaniambia kuwa anipeleke arusha akanitafutie kazi, nilikubali tukaondoka kesho yake, ila hadi sasa sina mawasiliano na wazazi wangu na sina ndugu yeyote hapa arusha,'' alisema anna.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi 8 alichofanya kazi kwa mtuhumiwa huyo, hakuwahi kulipwa mshahara ambao walikubaliana shilingi 20,000 kwa mwezi, ila aliwahi kumpa shilingi 10,000 na kumnunulia sketi mbili tu.

Alieleza kuwa mbali na kumfanyia unyama, alikuwa akimtesa kwa kumfanyisha kazi nyingi ikiwemo kumlazimisha kusomba maji umbali mrefu bila kupumzika, huku akishindwa kumsomesha kama alivyoahidi kufanya hivyo hapo awali.

 Kwa upande wa mwakilishi wa shirika la shaloom center, Enezael Joseph alisema kuwa wamefanikiwa kumwokoa mtoto huyo katika mazingira magumu baada ya kupata taarifa kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kinyume cha sheria.

Alisema kuwa shirika hilo lilipata taarifa kutoka kwa majirani wa mtuhumiwa ambao walichoshwa na vitendo vya manyanyaso anavyovipata mtoto huyo na kuamua kumfuata mtoto huyo na kuzungumza naye ndipo alieleza mambo mazito ya kulawitiwa na kunajisiwa naa mtuhumiwa kila kukicha.

 Joseph anasema kuwa baada ya taarifa hizo walitoa taarifa kituo cha polisi ngaramtoni na kupewa hati ya matibabu (PF3)  ambapo msichana huyo baada ya kupimwa katika hospitali ya seliani ya jijini arusha, aligundulika kuharibiwa vibaya sehemu zake zote za siri.

Alisema baada ya kupata majibu ya dakitari walirejea na kuwakabidhi polisi ambapo walifungua hati ya mashtaka ya kulawiti yenye kumbukumbu namba NGT/RB/1113/2013 ambapo mtuhumiwa alikamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaaendelea.

Hata hivyo mtuhumiwa wakati akitiwa mbaroni alisikika akidai kwamba anachofahamu kwa msichana huyo ni kwamba anamdai fedha zake za mshahara ila hayo madai mengine si kweli kwani amepandikizwa ili kumdhalilisha.





Read More »

Video Queen wa Kamugina ya Linex aangukia katika Penz* la Jux


Baada ya Kung'aa katika Video mpya ya Linex, mwana mitindo Jack Patric amenaswa na Kamera za Wadaku akiwa maeneo Tofauti tofauti katika mapozi ya kimahaba, hii ndio Couple Mpya ya Mjini.

Angalia Picha zaidi hapo chini:-




Vp wamependeza au Lah?!!!!

Read More »

Filamu ya KIGODORO ya Zamaradi Mketema, yamgharimu milioni 16


Mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema hivi karibuni aliingia msituni kuandaa filamu yake iitwayo ‘Kigodoro’ iliyoshirikisha mastaa wakiwemo Hemedy PHD, Kajala na Muhogo Mchungu.

Akiongea na mwandishi wetu, Zamaradi alisema aliamua kuandaa filamu hiyo baada ya kuona kuwa filamu nyingi za Tanzania zina hadithi zile zile hivyo alitaka kuja na kitu tofauti.

“Tuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea Tanzania ambayo yanaweza kukaa kwenye filamu yakachekesha, yakafurahisha, yakaelimisha. So nikafikiria, nikawaza yale maisha ya uswahilini, watu wanasutana, wanagombana, yale maisha ambayo unakuta chai ipo lakini vitafunio mnajitegemea, nimejaribu kuangaza familia ya aina ile,”alisema Zamaradi.

“Nikatoa idea, nikampa mtu aniandikie script, akaandika script vizuri ndo tukaingia mzigoni.”

Zamaradi amesema hadi sasa gharama aliyoitumia kutengeneza filamu hiyo ni zaidi ya shilingi milioni 16.





Read More »

Pamoja na skendo ya kuibiana Mume, Jokate ajitokeza na kumfariji Wema Sepetu baada ya kufiwa na baba yake mzazi.





LICHA ya kuwa waliwahi kupokonyana bwana (Nasibu Abdul ‘Diamond’), mwigizaji Wema Sepetu na  mtangazaji Jokate Mwegelo wamekutana katika msibani na kupiga stori.

 Kwa mujibu wa meneja wa Wema, Martin Kadinda, Jokate aliibuka Jumanne iliyopita usiku kwenye msiba wa baba Wema uliochukua nafasi nyumbani kwao Sinza-Mori jijini Dar na kumfariji hadi usiku mnene.

“Fani ya urembo na ubunifu ni fani za watu makini sana ambao chuki kwao ni mwiko, nimefurahishwa na kitendo cha Jokate kuja msibani kwani anaonyesha dhahiri kuwa ni mtu mwenye huruma na imani,” alisema Kadinda.




Read More »

Husna Idd na Maimatha wafanya shindano la Makalio yao...




MWIGIZAJI Husna Idd ‘Sajent’ na mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse wamenaswa wakishindana ukubwa wa makalio yao wakiwa wamelala kitandani.

Tukio hilo lililowashangaza wadau, lilitokea hivi karibuni wakati mastaa hao walipokuwa wanarekodi moja ya vipindi vya washiriki wa Shindano la Vigori katika Hoteli ya Kebbys Mwenge jijini Dar.

“Jamani mimi ninalo (wowowo) kuliko wewe, ukubwa dawa mimi na wewe wapi kwa wapi Sajent?” alisikika Maimartha.

-GPL





Read More »

Alichokisema Sintah baada ya Huddah Kumpa Pole Wema na Kutamani arudiane na Diamond ni Hiki hapa.


Baada ya Mwanadada Hudda kutoka nchini Kenya Kuandika katika ukurasa wa Instagram ni Jinsi anamkubali Wema na kumpa pole kutakana na kifo cha baba yake, Huddah alienda mbali zaid na kusema anatamani kumwona Wema na Diamond wakiwa pamoja na si wengineo maana hawaendani na Diamond.

Kazi Imemkuta Mwanadad wa kwetu Tanzania, alichoamua kukiandika ni hichi :-
"Hii kali kuliko na sijui katokea wapi huyu dada Hudda amekuja na haya mapya lolest, binaadam wanaweza wakafanya ukatafuta kamba walahiii, eeh sisi tuendelee kuangalia sinema hii na naongeza popcorn  maana sinema ni ya bureee kabisa, all in all Dimondo mwenyewe ataamua maana anajua nani anayempenda.... hata mama,mdogo nk hawezi kumshauri matters concerning the heart banaaa......"

Sijui anakusudia nini?!!!!!


Read More »

Cossy a share na Fans wake Pics Mpya ndani ya S*xy Red Dress


Mwanadada ambaye amekuwa aking'aa  katika screen kwa staili ya kulingishia kifua chake, Cossy Orjakor, ame share na Fans wake pics za hivi karibuni akiwa ana shoot video ya msanii mmoja nchini Nigeria akiwa Kimahab* zaidi ndani ya gauni jekundu

Angalia Picha zaidi hapo chini:-





Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger